Baadhi ya maduka eneo la Mashine tatu mjini Iringa yakiwa
yamefungwa kwa hofu ya kutokea vurugu ,ambazo hata hivyo hazijatokea
baada ya machinga kugoma kutumiwa kisiasa
Hali ilivyo eneo la Mashine tatu mjini Iringa
Haya ni maadishi yanayosomeka HATARI yaliyochorwa na watu
wasiojulikana usiku wa kuamkia jana kama sehemu ya kuwatisha wananchi
na kuhamasisha vurugu kabla ya jeshi la polisi kuweka ulinzi mkali
eneo hilo
Wafanyabiashara wa maduka ya mchele eneo la mashine tatu wakiendelea na biashara zao kwa utulivu zaidi leo
Hili ndilo eneo la mashine tatu kama linavyoonekana mchana huu baada
ya machinga kukubali kuheshimu sheria ya mipango miji na kuachana na
mvutano usio na tija kwao
Amani na utulivu warejea eneo la Mashine tatu mjini Iringa ,wananchi
waendelea na shughuli zao kama kawaida leo ,machinga wakubali kutii
sheria
Askari wa FFU akiwa katika ulinzi eneo la mashine tatu leo ambapo hali imetulia zaidi
Askari wa FFU mjini Iringa akipita eneo la mashine tatu ambako
machinga walipanga kufanya biashara na vurugu leo ila hali ya amani
imetawala zaidi eneo hilo
Askari wa FFU wakiwa kazini leo eneo la mashine tatu
Ulinzi waimarishwa eneo la mashine tatu ,machinga wakubali kufanya biashara eneo la Mlandege kama awali
Hivi ndivyo hali ilivyo eneo la mashine tatu leo ni amani na utulivu kwenda mbele hakuna mabomu leo
Leo ni amani zaidi Iringa hakuna vurugu zozote
Hali
ya amani na utulivu imerejea mjini Iringa baada ya machinga kukubali
kuendelea na biashara zao katika eneo la Mlandege ambalo uongozi wa
Halmashauri ya Manispaa ya Iringa iliwatengea wamachinga hao .
Uchunguzi uliofanywa katika eneo hilo umeshuhudia kuwepo kwa amani
zaidi na wafanyabiashara waliokuwa wamefunga maduka yao kuhofia
amani kuvurugika wameonekana wakifungua maduka yao huku machinga
ambao walihamasishwa na mbunge wa jimbo la Iringa mjini mchungaji Peter
Msigwa (Chadema) kurejea eneo hilo wakionyesha kupuuza ushauri huo
wa mbunge na kuelekea Mlandege kama Manispaa ilivyowataka .
Baadhi
ya machinga wamesema kuwa suala hilo la machinga kurudi eneo
hilo lipo kisiasa zaidi na kuwa kama si mbunge kuwahamasisha
machinga hao kupitia mikutano yake hakuna machinga ambae angerejea
eneo hilo kwani wengi wao kuwepo Mlandege walionyesha kukubali .
Hata
hivyo machinga hao wamesema kuwa hata waliofanya vurugu wiki
iliyopita si machinga ni wahuni kutoka maeneo mbali ambali ambao
walifanya fujo hizo na kuwa machinga kama machinga hana nafasi ya
kufanya vurugu zaidi ya kutafuta pesa.
Pia
uchunguzi unaonyesha jeshi la polisi mkoa wa Iringa kujipanga
vema kwa siku ya jana usiku na leo ikiwa ni pamoja na kuwakamata
baadhi ya watu ambao walikuwa wakitoa kauli za kichochezi katika
vijiwe mbali mbali .
Huku
askari wa FFU kwa mara ya kwanza usiku wa kuamkia leo walionekana
wakiweka ulinzi mkali katika maeneo mbali mbali ya mji likiwemo eneo la
soko la Kihesa ,Mlandege, Mashine tatu na maeneo mengine mengi hali
iliyopelekea vikundi vya vurugu kutoweka ghafla mjini Iringa na wale
waliokuwa wamepanga kuvuruga amani kuamua kusitisha mpango huo.
Wakati
huo huo mkuu wa mkoa wa Iringa Dkt Christine Ishengoma amewapongeza
machinga kwa kukubali kurejea eneo la Mlandege ambalo uongozi wa
Manispaa ya Iringa ulikuwa umewapangia na kuwa hekima iliyoonyeshwa
na machinga hao inapaswa kuigwa na makundi mengine ambayo yamekuwa
yakichochewa kufanya vurugu kutokana na matatizo yao.
"Kweli
napenda kuwapongeza sana machinga wametumia busara sana baada ya
kikao chao na mstahiki meya wa Manispaa ya Iringa kuhusu kutafuta
suluhu lao .....bila shaka wameonyesha kumsikiliza na kumheshimu
vema meya na mimi kama mkuu wa mkoa nawaahidi kuwa suala lao
litatafutiwa uvumbuzi wa kudumu nawaomba wawe na subira na kuepuka
kutumiwa na wana siasa katika suala lao"
na mtandao huu wa www.matukiodaima.com
No comments:
Post a Comment