Mbunge akisalimiana na Refa wa Mchezo huo
Kikosi cha Bunda Sport Club
Kikosi cha timu ya Elimu Fc ambao ndiyo Mabingwa Bulaya Cup 2013
Umati wa wanabunda wakiwa Uwanjani
Kazi ilikuwa inaendelea
Kombe hiloooooooooooooooo
Jamaa hakutaka kuwa nyuma
Ulikuwa ni ubingwa wa Matuta
Na Augustine Mgendi,Bunda
Michuano ya
Kombe la Mbunge wa Viti Maalum Kupitia Vijana Mkoani Mara Esther Bulaya linalojulikana
kama Esther Bulaya Cup imemalizika wilayani Bunda Mkoani Mara ambapo Timu
inayoundwa na Wadau wa Elimu wilayani humo Elimu Fc ikiibuka Bingwa wa
Mashindano hayo kwa Mwaka 2013.
Michuano
hiyo ambayo ilikutanisha timu zaidi ya 30 kutoka wilayani Bunda ilimaliza kwa kuzikutanisha timu za
Bunda Sport Club na Elimu Fc, ambapo iliibuka bingwa wa Kombe hilo kwa Mwaka
2013 kwa Mikwaju ya Penati 3-1 baada ya
kufungana bao 1-1 ndani ya dk 90 na kujinyakulia kitita cha Shilingi milioni
moja pamoja na Kombe.
Mshindi wa
Pili alipata zawadi ya Shilingi laki Tano huku mshindi wa tatu timu ya Town
Star ambayo iliifunga timu Majengo Fc bao 1-0 ilipata kiasi cha Shilingi laki 3
na Seti ya Jezi ,ambapo baada fainal hizo Mbunge Esther Bulaya alikuwa na haya
ya kunena.
Akiongea
wakati wa kukabidhi Zawadi mbalimbali wa Washindi,Mbunge Esther Bulaya alisema kuwa kuna baadhi ya watu ambao
walikuwa wanapanga Mikakati ya kuhujumu
Mashindano hayo yasifanyike Mbunge ambapo alisema kuwa kufanya hivyo ni
kutowatendea haki Vijana wa Bunda ambao ndiyo walengwa wa Michuano hiyo.
Mh Bulaya
aliahidi kuendelea kudhamini Michuano hiyo Mpaka Mwisho wa Ubunge wake na
kuongeza kuwa kama atafanikiwa tena kuwepo katika hiyo nafasi ataendelea
kufanya Michuano hiyo mpaka kufa kwake.
“Mimi
nashangaa sana kuna baadhi ya watu wanataka kuhujumu
Mashindano haya kitu
ambacho hawatawatendea haki vijana wa Bunda maana ndiyo walengwa,napenda
kuwaahidi Vijana wenzangu nitaendelea kudhamini mpaka mwisho wa ubunge wangu na
kama nitaendelea kuwepo kwenye hii nafasi nitayadhamini Mpaka kufa Kwangu”alisema
Bulaya.
Aidha baadhi
ya Wadau wa Michezo wilayani humo walimpongeza Mbunge huyo na kusema kuwa
Michuano hiyo inajenga uzalendo wa Vijana wa Bunda huku wakimuomba kuiendeleza
Michezo hiyo kwani imeonyesha Mafanikio Makubwa tangu kuanzishwa kwake.
Walisema
wilaya ya Bunda ni mmoja ya wilaya Mkoani Mara ambayo iilikuwa nyuma katika
suala la Michezo lakini kwa Muda Mfupi sasa wilaya hiyo imeonekana kuwa kinala.
“Unajua hii wilaya ilikuwa nyuma sana
Kimichezo lakini tangu huyu Mbunge ameanzisha haya Mashindano sasa hivi Bunda
inaongoza kwa Michezo hasa Soka maana hata bingwa wa Mkoa na Makamu wake
wanatoka Bunda sasa hayo si Mafanikio”? alisema Juma Mbano
No comments:
Post a Comment