Serengeti
-MADHARA
ya kutoa zabuni kwa kampuni zisizo na
uwezo yameanza kujionyesha katika Mamlaka ya Mji wa Mugumu wilayani
Serengeti,kufuatia Kampuni ya Ujenzi Youth Group iliyopewa zabuni ya kuzoa taka
kushindwa na kupelekea mji kuzaa taka ,hali inayoibua hofu ya magonjwa ya
mlipuko.
Kampuni hiyo ilipewa zabuni hiyo kwa malipo ya sh,milioni 48
kwa mwaka wakati haina vifaa vya kufanya kazi hiyo,na kuacha kampuni nyingine
iliyoomba kwa sh,mil.38 ikiwa na vifaa vya kuweka mji huo unaotarajiwa kuwa
kitovu cha utalii safi.
Mtendaji wa Mamlaka hiyo Gedioni Obel mbele ya baraza la
madiwani halmashauri ya wilaya hiyo lililotaka maelezo kutokana na viwanja vya wazi kugeuzwa
madampo ikiwa ni karibu na nyumba za kulala wageni,alikiri kuwa mzabuni huyo
hana uwezo na ndiyo chanzo cha kuzagaa kwa taka.
Hata hivyo maelezo yake yaliibua maswali kutoka kwa madiwani
waliotaka kujua sababu za kumchukua mzabuni asiye na uwezo wala vifaa kufanya
kazi hiyo kwa gharama ya juu na kumwacha aliyeomba kwa gharama za chini akiwa
na uwezo wa kuweka mji safi.
Makamu Mwenyekiti wa halmashauri hiyo Jumanne Kwiro alisema
hali hiyo haiwezi kuvumiliwa kwa kuwa inapingana na jitihada wanazofanya za
wilaya hiyo kuwa kitovu cha utalii.
“Inasikitisha sana mji kuwa mchafu namna hii,maeneo yote ya
wazi yamegeuzwa dampo kwa madai kuwa ni sehemu ya kukusanyia ….mbona hazitolewi
zinakaa hadi wiki…ni mtalii gani atakuja mji huu na kulala hoteli akivuta hewa
chafu….tunatoa siku 21 taka zote ziwe zimeondolewa”alisema na kuungwa mkono na
madiwani wenzake.
Pia waliutaka uongozi wa hospitali ya Nyerere ddh kuhakikisha wanajenga
choo kipya kunusuru afya za wagonjwa wanaopata huduma hapo kutokana na kilichopo kujaa .
Naye Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo Goody Pamba
alikiri kuwepo na tatizo hilo la uchafu kuzagaa mji wa Mugumu na wakati
mwingine kukaa muda mrefu bila kuzolewa na kuelezea kuwa linashughulikiwa ili
kuhakikisha mji unakuwa msafi kwa kutumia sheria ndogo ndogo .
Mwisho.
TAKA HIZO HUKAA KWA MUDA MREFU BILA KUTOLEWA KWA KILE KILICHODAIWA NA WATENDAJI WA MAMLAKA HIYO KUWA MZABUNI ALIYEPEWA TENDA HIYO KWA SH,MIL,42 KWA MWAKA HANA UWEZO WALA VIFAA,LAKINI BODI YA ZABUNI ILIMWACHA ALIYEOMBA KWA SH,MIL.38 AKIWA NA VIFAA NA KUMPA ASIYE NA VIFAA.
WATOTO WANAOCHEZEA KATIKA VIWANJA HIVI WAKO HATARINI KIAFYA.
DAMPO LINGINE LIMEWEKWA KARIBU NA NYUMBA YA KULALA WAGENI YA GESASE,IKIWA NI KARIBU NA NYUMBA ZA NHC KUKAKO KAA VIONGOZI WA HALMASHAURI HIYO,IKIWEMO AFISA AFYA WA MAMLAKA HIYO.
NYUMBA ZINAZOONEKANA MBELE YA DAMPO HILO NI MAKAZI YA MAAFISA WA SERIKALI AMBAO WAMERUHUSU DAMPO HILO KUWEPO HAPO.
LICHA YA TAMBO ZA VIONGOZI WA KISIASA KUWA MJI HUO WANATAKA UWE KITOVU CHA UTALII,MAENEO YOTE YAWAZI YAMEGEUKA KUWA MAJALALA YA TAKA ,
No comments:
Post a Comment