|
HISTORIA:Chelsea
becomes the first English team to win all three major European Club
competitions, having already claimed the Champions League and the (defunct) Cup
Winner’s Cup!
Shujaa wa
Mechi hii ni Beki wa Chelsea, Branislav Ivanovic, ambae Mwaka jana hakucheza
Fainali ya Kombe la Europa League kwa kuwa Kifungoni, kwa kufunga Bao la Pili
na la ushindi kwa kichwa katika Dakika ya 92.
Hadi
Mapumziko Mechi hii ilikuwa 0-0 huku Benfica wakionyesha umilikaji mpira wa
hali ya juu lakini staili yao ya uchezaji ya kutaka ‘kutembea’ na mpira hadi
wavuni ndio iliwaangusha.
|
|
HISTORIA:Chelsea
becomes the first English team to win all three major European Club
competitions, having already claimed the Champions League and the (defunct) Cup
Winner’s Cup!
|
|
Goli la
mchezaji Branislav Ivanovic dakika ya
pili ya muda wa nyongeza kati ya tatu baada ya kutimu dakika 90 za kawaida
kumalizika , hapo jana (May 15,2013) limeipa Cheslea Kombe la Europa League
baada ya kuilaza Benfica ya Ureno mabao 2-1 kwenye Uwanja wa Amsterdam Arena
nchini Uholanzi.
Beki huyo wa
Serbia, alipaa hewani kwenda kuufuata mpira wa kona uliopigwa na Juan Mata na kuujaza nyavuni.
|
|
Shujaa wa
Mechi hii ni Beki wa Serbia, wa Chelsea Branislav Ivanovic, ambae Mwaka jana hakucheza
Fainali ya Kombe la Europa League kwa kuwa Kifungoni, kwa kufunga Bao la Pili
na la ushindi kwa kichwa katika Dakika ya 92.
|
|
Branislav
Ivanovic akipongezwa na hapo jana(May 15,2013 katika fainali ya Kombe la Europa
League baada ya Chelsea kuilaza Benfica ya Ureno mabao 2-1 kwenye Uwanja wa Amsterdam
Arena.
|
|
Torres
akimpiga chenga kipa wa Benfica kabla ya kufunga bao la kwanza kwa Chelsea hapo
jana(May 15,2013 katika fainali ya Kombe la Europa League baada ya Chelsea kuilaza
Benfica ya Ureno mabao 2-1 kwenye Uwanja wa Amsterdam Arena.
|
|
Gwiji Patrick
Kluivert akiwasilisha Kombe la Europa uwanjani hapo jana(May 15,2013 katika
fainali ya Kombe la Europa League baada ya Chelsea kuilaza Benfica ya Ureno mabao 2-1
kwenye Uwanja wa Amsterdam Arena.
|
|
Bango:Likisema’’Tunamtaka
Mourinho: Mashabiki wa Chelsea waliwasilisha hisia zao pia juu ya kocha atakayerithi mikoba Rafa Benitez ‘’
hapo jana(May 15,2013 katika fainali ya Kombe la Europa League baada ya Chelsea
kuilaza Benfica ya Ureno mabao 2-1
kwenye Uwanja wa Amsterdam Arena.
|
Ile balaa ya
Benfica kutotwaa Taji lolote Ulaya kwa Miaka 51 tangu enzi za Nguli wao
Eusebio, licha ya kutinga Fainali 7 sasa, linazidi kuendelea.
|
Rodrigo wa Benfica na Cesar Azpilicueta wa Chelsea.
|
Wapo
Mashabiki wa Benfica wanaoamini kuwa hiyo ni laana toka kwa aliekuwa Kocha wao,
Bela Guttmann, ambae ndie aliwapa Taji lao la mwisho Mwaka 1962 wakati Eusebio
akichaza walipoicharaza Real Madrid Bao 5-3 na kuwa Mabingwa wa Ulaya.
Baada ya
hapo, Bela Guttmann aliondoka Benfica kwa mzozo na kuapa na kulaani kuwa
Benfica haiwezi kutwaa tena Taji la Ulaya bila ya yeye.
Kwa bahati
mbaya, Bela Guttmann ni marehemu na licha ya Mashabiki wengi wa Benfica
kupeleka Maua Kaburini kwake na kuomba laana iondoke inaelekea mambo
hayajatengemaa.
No comments:
Post a Comment