Baadhi ya wananchi wakipakua badhi ya mizigo ambayo imesalia ndani ya basi hilo.
Watu 63 wamenusurika kufa
baada ya gari walilokuwa wakisafiria kutoka jijini Mwanza kwenda mkoani Kigoma,
kuwaka moto.
Tukio hilo limetokea leo
majira ya saa nne na nusu asubuhi katika kijiji cha Nyantakala wilayani
Biharamuro, Mkoani Kagera, likihusisha gari aina ya Scania lenye namba T 928
AVP, mali ya Kampuni ya Adventure ya jijini Mwanza.
Kwa mujibu wa taarifa
zilizopatikana kutoka wilayani Biharamuro, watu 8 kati yao wamejeruhiwa kwa
moto na wamepelekwa katika hospitali ya wilaya ya Bukombe, mkoani Geita, kwa
matibabu zaidi.
Chanzo ajali hiyo ni
hitilafu ya umeme iliyotokea katika betri ya Gari hilo, na mpaka sasa gharama
halisi ya mali za abiria zilizoteketea kwa moto bado haijajulikana.
Mwonekano wa basi la adventure kwa mbele baad ya kuungua.
Mizigo iliyokuwa ndani ya buti ikiendelea kuteketea.
Hii ndiyo hali halisi ya ajali ya Adventure
Poor bus, Thanks that there's no fatalities, there's lack of used cars, bus, and other vehicles - only few were injured!
ReplyDelete