Kikundi cha Elimika Musoma mjini kimeishukuru
Taasisi ya The Foundation for Civil Society ya jijini Dar Es Salaama kwa
ufadhili walioutoa kwa kikundi hicho katika Kujijengea Uwezo.
Akiongea ofisini kwake Mratibu wa Kikundi hicho Bi
Dora Maro alisema kuwa Taasisi hiyo ya The Foundation for Civil Society ilitoa
ufadhili wa kiasi cha zaidi ya shilingi Milioni Saba katika mradi wa kujijengea
uwezo kwa mwaka 2010/2011 ambapo mradi huo ulikuwa ukitekelezwa katika Kata za
Bweri,Nyakato na Nyasho
Amesema katika kutekeleza mradi huo kikundi hicho
kimepata faida kubwa kutokana na Viongozi na Wanachama wake kujua hali halisi ya uongozi,mapungufu
yaliyopo katika Kikundi chao na kuyafanyia kazi.
Bi Dora alisema kuwa Kumekuepo na mabadiliko makubwa
katika Jamii tangu wamepewa ufadhili huo ambapo alisema kuwa wameweza kujua
jinsi ya Kupanga Miradi ya Kibiashara na kuendesha biashara hizo.
Alisema mbali na hivyo wamejua pia kupanga miapango
mikakati na mipang kazi,kuwa wabunifu wa miradi,ufuatiliaji na usimamizi wa
fedha pamoja na utunzaji wa kumbukumbu.
Akiendelea kueleza faida walizozipata kutokana na
Mradi huo waliokuwa wakiuetekeleza kupitia ruzuku kutoka The Foundation for
Civil Society,Bi Dora alisema kuwa pia Mradi huo umesaidia kubadilisha Mtazamo
katika jinsi ambapo baadhi ya watu wameendelea kusema Mwanamke hawezi hivyo
Mradi huo umesaidia kuleta mabadiliko ya Kifikra katika Jamii.
Katika kukamilisha Mradi huo Mratibu wa Kikundi
hicho alisema kuwa wameweza kuwashirikisha watu mbalimbali katika kujengewa
uwezo ikiwa njia ya kuendesha Maisha yao,baadhi ya watu walioshirikishwa katika
Mradi huo ni pamoja na Waathirika wa Ugonjwa wa Ukimwi,Wajane na Walemavu
“Sisi
tuliamua kuwashirikisha hawa wenzetu kwasababu tuliona kuwa wanasahaulika na
pia tulifanya hivyo ikiwa ni njia ya
kuwasaidia kuendesha Maisha yao baada ya huu Mradi” alisema Bi Dora
Kuhusu
Ushirikishwaji wa Jamii katika Mradi huo Bi Dora alisema kuwa
walifanikiwa katika hilo kwani Viongozi waliowahitaji kushirikiana nao
walijitokeza na hivyo kuwasaidia katika kuhamasisha Jamii katika kukiunga Mkono
Kikundi hicho.
Bi Dora alisema kuwa kulikuwepo na hamasa kubwa kwa
Wananchi ambao Mradi huo ulikuwa umehusisha baadhi ya watu ikiwa ni njia ya
kuwajengea Uwezo wa Kimaisha,huku akisema kuwa wamefikia Malengo yao ya Sera ya
Ushirikishwaji katika Jamii kutoka katika Kikundi hicho.
Pamoja na kupata ruzuku kutoka The Foundation for
Civil Society ya jijini Dar Es Salaam,Mratibu huyo alisema kuwa kikundi chake
kina Mahusiano Mazuri na baadhi ya Makampuni na wafadhili kutoka ndani mfano
akiongelea Mgodi wa Dhahabu wa African Barrick Gold (ABG) ambapo umewahi
kuwasaidia.
Pamoja na kutekeleza Mradi huo kwa kiwango kikubwa
Bi Dora alisema kuwa kulikuwepo na changamoto mbalimbali katik kutekeleza Mradi
huo ikiwemo wanachama kuwa na uelewa mdogo juu ya ruzuku hiyo,kutokujua nini
maana ya Mpango mkakati na mpango kazi,Utunzaji wa Fedha na wananchi kudhani
kuwa ruzuku hiyo ni ya kutumia katika kuendesha Maisha yao.
Baadhi ya wanakikundi
Wakiongelea kuhusu Mradi huo baadhi ya wanachama
walionufaika na Mradi huo ni pamoja na Bi Judith Semen ambaye alisema kuwa
amenufaika kwa kiasi kikubwa na mradi huo kutokana na kuelewa mambo mengi
yanayohusiana na utunzaji wa Fedha.
“Mimi
nilikuwa sijui jinsi ya kutunza fedha kitaalamu lakini baada ya mradi huu wa
kutujengea uwe nimeweza kujua na nafurahi maana hata nikiamua kufungua biashara
naweza kufanya vizuri” alisema Bi Judith
Naye Jenipher Danga,Halima Mohamed na Debora Kopoka
walisema kuwa wamenufaika kwa kiasi kikubwa kwani ni mambo mengi ambayo
wamejifunza kutoka katika Mradi huo na hivyo kuwa kuna haja ya kuendesha mambo
kitaalamu na si kimazoea.
Katika upande wa Serikali kushirikishwa katika Mradi
huo,Mtendaji wa Kata ya Bweri Bw. Jamhuri Makongoro alisema kuwa Kikundi hicho
cha Elimika Musoma mjini kimeweza kushirikiana vyema na Serikali ya mtaa huo
lakini pia kimesaidia wanawake wengi ambao ni Wajane,waathirika na Walemavu
katika kuwajengea Uwezo wa kimaisha.
“Nashukuru
Kikundi hiki kimeweza kushirikiana na Serikali ya mtaa vyema na hasa kimesaidia
sana Wajane,Walemavu na watu walioathirika na ugonjwa wa Ukimwi” alisema
Mtendaji huyo.
Aidha akiongelea Faida ilizozipata kikundi hicho
kutokana na ufadhili wa The Foundation For Civil Society,Bi Dora alisema kuwa
kupata ruzuku hiyo imewasaidia kupata mafunzo ambayo yamesaidia kuendesha
Kikundi hicho kwa ufanisi mkubwa,kuimarika katika kubuni Miradi na
kuiendesha,matumizi sahihi ya Fedha,kusaidia Jamii ambayo ilihitaji msaada wa
kuwajenga kiuwezo,utunzaji wa kumbukumbu,kupanga Mipango mikakati na Mipango
kazi,ufuatiliaji na ukamilishaji wa miradi mbalimbali na kujua udhaifu wa
Kikundi hicho
Mbali na hivyo Bi Dora alisema kuwa kupata ruzuku
kutoka katika Taasisi hiyo imesaidia kuaminika kwa Asasi hiyo mbele ya Jamii na
Viongozi wa serikali kitu ambacho aliishukuru sana taasisi ya The Foundation
for Civil Society.
“ Kiukweli hii Taasisi imetupatia sana heshima kwa
kutupatia ruzuku maana tunaaminika kwa Jamii na hata kwa Viongozi wa Serikali
kitu ambacho ni lazima tuishukuru The Foundation for Civil Society” alisema Bi
Dora
No comments:
Post a Comment