Monday, July 16, 2012

RC MARA AFUNGUA SEMINA KUHUSU SENSA MKOANI MARA

              Baadhi ya wajumbe wakiwa ndani ya ukumbi wa CCM mkoa wa Mara
       Mkuu wa mkoa wa Mara Bw John Tuppa akifungua semina ya wakufunzi wa sensa mkoani Mara
                      Wajumbe wakiwa katika semina
                               Wajumbe wakiwa kwenye semina ya sensa
  Mkuu wa mkoa wa Mara Bw. John Tuppa akiwa na Mwakilishi wa walemavu katika semina hiyo mjini Musoma leo
            Mwana wa Afrika nikiwa na Mdau Shomary wa Binda
              George Marato wa ITVVVVVVVVVVVVVVVVVV
                      Wakuu wa wilaya Mkoani Mara
 MUSOMA
SERIKALI mkoani Mara,imeviagiza vyombo vya dola na viongozi mbalimbali wa ngazi zote mkoani humo,kuhakikisha wanasimamia hali ya usalama kwa kuwachukulia hatua kali watu wote ambao wataonekana kukwamisha mafanikio ya zoezi la Sensa ya watu na makazi,ambalo linatarajia kufanyika nchini kote kuanzia Agosti 26 mwaka huu.
Kauli hiyo imetolewa mjini Musoma na mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ambaye pia ni mkuu wa mkoa wa Mara Bw John Gabiriel Tupa wakati akifungua mafunzo ya wiki mbili ya wakufunzi wa Sensa ya watu na makazi ngazi ya mkoa.
Alisema serikali haitakubali baadhi ya watu kuwa chanzo cha kukwamisha zoezi hilo muhimu kwa taifa na ambalo linatarajia kiasi kikubwa cha fedha,ambapo amesema ni wajibu wa kila kiongozi kufanya uhamasishaji kwaajili ya kuwezesha mafanikio katika zoezi hilo.
Hata hivyo mkuu huyo wa mkoa wa Mara,alitumia nafasi hiyo kuonya kwamba kamwe serikali hatasita kuchukua hatua kwa wakufunzi hao na kwamba haitakubali kupokea visingizio vya aina yoyote kutoka kwao baada ya kupata mafunzo hayo.
Kuhusu wasiwasi wa wananchi wa kupoteza muda wakati wa zoezi hilo,mkuu huyo wa mkoa wa Mara,alisema zoezi la sense halitaweza kukwamisha shughuli za wananchi kiuchumi na kwamba watoe taarifa sahihi kwa makarani bila ya hofu  kwa vile taarifa hizo mbali na kuwa za siri pia zitawezesha taifa kupanga mipango yake mbalimbali ya maendeleo.

No comments:

Post a Comment