Friday, July 20, 2012

RC AWATAKA WATANZANIA WAISHIO NJE YA NCHI KUWEKEZA NCHINI.

Dinna Maningo,Tarime

MKUU wa Mkoa wa Mara John Tuppa amewataka Watanzania waishio nje ya nchi na wale wenye uwezo wa kipato kusaidia katika Nyanja mbalimbali za maendeleo hususani watoto yatima na waishio katika mazingira magumu.

RC Tuppa alisema kuwa endapo watu wenye uwezo watajitokeza kwa wingi katika kusaidia watoto yatima na  wa mazungira magumu katika kuhakikisha wanapata elimu itasaidia kupunguza tatizo la watoto wanaolandalanda mitaani.

               Mkuu wa mkoa wa Mara Bw.John Tuppa

Hayo yalisemwa  jana na Mkuu wa Mkoa wa Mara Bw.John Tuppa wakati alipotembelea kituo cha kulelea watoto yatima na wale wa mazingira magumu kinachofahamika kwa jina la CITY OF HOPE kilichopo kijiji ncha Ntagacha kata ya Genyange Wilayani Tarime kilichoanzishwa na Docta John Chacha aishie nchini Marekani kwa kushirikiana na wadau mbalimbali.

“Watanzania wenye uwezo wa kipato wenye elimu na waishio nchini na nje ya nchi wawekeze hapa nchini ili kusaidia wananchi hususani katika maswala mbalimbali yakiwamo ya kuhakikisha watoto yatima na wamazingira hatarishi wanapata elimu hii itasaidia kupunguza umaskini kwani hao watoto watakuwa na elimu itakayowasaidia katika maisha yao ya baadae badala ya kuwa tegemezi”alisema Tuppa.

Anaongeza”Nampongeza Docta Chacha anaeishi Marekani kwa kuikumbuka nchi yake na kuja kuwekeza nyumbani kwa kuanzisha kituo cha kulelea watoto yatima na watoto hao wanapata elimu ya shule ya msingi inatotolewa kituoni,kwahiyo tunategemea kupata wasomi wengi hapo baadae kutoka kituo cha yatima CITY OF HOPE  natoa wito kwa Watanzania wengine kusaidia katika mambo mbalimbali ya kimaendeleo”alisema.

RC Tuppa aliwaasa yatima kusoma kwa bidii licha yakuwa hawana wazazi na kuwa wajitambue kuwa wao pia ni sehemu muhimu katika jamii nakwamba endapo watatoa fikra kuwa wao ni watoto yatima watajijengea maisha mazuri baadae kwani wengine watajitegemea kutokana na elimu walioipata shuleni.
“Watoto yatima na wamazingira magumu wasijichukulie kuwa ni watoto yatima,sisi Watanzania ndiyo walezi wenu sisi ni wazazi wenu msiwe wanyonge na mnapaswa kupata mahitaji yote kama binadamu wengine sisi ndiyo tunawaondoa uyatima msikubali kuitwa yatima kwa sababu wananchi wote wa Mkoa wa Mara ndiyo wazazi wenu mkitoa fikra kuwa ninyi si watoto yatima mtajijengea maisha mazuri.

Mwanzilishi wa kituo hicho cha watoto yatima Docta John Chacha anasema kuwa pamoja na kuanzisha kituo hicho wanakabiliwa na changamoto mbalimbali kama vile upungufu wa vitabu,madawa katika kituo cha kutolea huduma ya afya kituoni hapo na ukosefu wa madactari ambapo ameiomba Serikali kukisaidia kituo katika kuwapatia Wauguzi na madawa kwa ajili ya huduma ya tiba kwa watoto.

Docta Chacha alisema kuwa kituo hicho cha watoto yatima kinahudumia jumla ya watoto 416 ambao pia wanapata elimu kuanzia darasa la awali hadi darasa la saba na inawalimu wapatao 15 wakiume wakiwa 9 na wakike 6 nakuwa  kwa mwaka huu kwa mara ya kwanza watahitimu  wanafunzi darasa la saba wapatao 8 wavulana wakiwa 6 na wakike 8.

No comments:

Post a Comment