Tuesday, July 17, 2012


                HABARI MBALIMBALI KUTOKA MARA

WATU watatu wa familia moja wamefariki dunia baada ya kugongwa na gari  katika kijiji cha Kusenye Kata ya Suguti katika halmashauri ya Musoma vijijini mkoani Mara


Afisa Mtendaji wa kata ya Suguti Bw Jackson Marwa akiongea kwa  njia ya simu kuwa  ajali hiyo imetokea  juzi majira ya jioni.


Amesema ajali hiyo inadaiwa kusababishwa na gari yenye namba za usajili T 752 BQR iliyokuwa ikiendeshwa na Bw Anthony  Kusaga wakati akitokea Manispaa ya Musoma kwenda katika kijiji cha Saragana.


Amesema ajali hiyo imesababishwa na mwendo kasi na hivyo kushindwa kuimudu wakati alipokuwa katika kona karibu na ya zahanati ya kijiji hicho.


Hata hivyo afisa mtendaji huyo amewaja watu waliokufa katika ajali hiyo ni Regina Mwelo mwenye umri wa mika 5,Nyakwesi Mwelo mwenye umri wa miaka 15 na Asha Mwelo mwenye umri wa miaka 17.


Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Mara Kamisha msaidizi Mwandamizi Abslom Mwakyoma amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kwamba Jeshi la Polisi linamshikilia dereva wa gari hilo

.................................


WATATU WAUWAWA NA WANANCHI WENYE HASIRA KALI.

Dinna Maningo,Tarime

WATU watatu WAKAZI WA Kijiji cha magena kata yaTurwa Wilayani Tarime Mkoani Mara wamewauwa kwa kupigwa hadi kufa na wananchi wenye hasira kali kwa madai ya kuhusika na wizi wa ng’ombe .

Akiongea na Waandishi wa habari ofisini kwake Kamanda wa polisi Mkoa wa kipolisi Tarime/Rorya Justus Kamugisha alisema kuwa watu waliouwawa wanatuhumiwa na wananchi kwa kujihusisha na wizi wa mara kwa mara  kijijini hapo ambapo wananchi walijichukulia sheria mkononi kuwauwa kwa madai ya kuiba ng’ombe.

Kamanda kamugisha alisema kuwa tukio hilo lilitokea juzi majira ya saa 6 .30 usiku huko kalibu na Mto Nyamiobo  katika kijiji cha Magena ambapo aliwataja  waliouwawa kuwa ni Ndiege Nyamhanga {25} Mang’iti Kamunu{30} na Nyaikore Simion {42}.

Alisema kuwa watu hao waliuwawa kwa kushambuliwa kwa silaha za jadi na kisha kuwachoma moto nakwamba chanzo cha mauwaji hayo ni wananchi kuwatuhumu watu hao kuiba ng’ombe ambapo miili ya marehemu imefanyiwa uchunguzi kwa mazishi na kuwa juhudi za kuwasaka waliohusika na tukio hilo zinaendelea.

Kamugisha aliwaasa wananchi kutojichukulia sheria mkononi kwa watu wanaowatilia mashaka na badala yake watoe taarifa katika vituo vya polisi ili sheria zichukuliwe dhidi yao.

,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,

 RORYA
 

SERIKALI imedaiwa kupuuza maelekezo na ushauri wa mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabe za serikali ya kutaka kukamatwa na kufikishwa katika vyombo vya sheria,maafisa kadhaa waandamizi wa halmashauri ya wilaya Rorya mkoani Mara kwa tuhuma za ufisadi badala yake imewahamishia vituo vipya vya kazi.


Maafisa hao ambao wamehamishia katika vituo vipya vya kazi na katika halmashauri za Kiteto,Rukwe,Karagwe,Kwimba na Mafia pamoja na makao makuu ya mkoa wa Morogoro ilipendekezwa na ripoti ya mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali katika taarifa yake ya ukaguzi maalum ya machi 2011 kuwa maafisa hao wasimamishwe kazi na kufikishwa katika vyombo vya dola.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo ya CAG,maafisa walikuwa wa wilaya ya Rorya ambao walipaswa kuchukuliwa hatua za kisheria kwa tuhuma za kusababisha ubadhilifu wa zaidi ya milioni 200 ikiwa ni pamoja na kutumia madaraka vibaya ni aliyekuwa mkurugenzi,mweka hazina,afisa raslimali watu mwandamizi,mhandisi wa ujenzi wilaya,afisa mipango wilaya na afisa ugavi daraja la pili.

Kufuatia hatua hiyo ya serikali ya kuwapangia vituo vipya vya kazi watumishi hao licha ya CAG kubaini kuwa wana tuhuma za kujibu,baadhi ya madiwani wa CCM katika  halmashauri ya Rorya,wametangaza kuwa endapo serikali itashindwa kuchukua hatua ndani miezi mitatu kuanzia sasa wako tayari kukiama chama chao katika kuwatendea haki wananchi.

Hata hivyo ripoti hiyo ya CAG imeipendekeza kwa baadhi ya watumishi kupewa adhabu ya kalipio kali,kuonywa na kukatwa mishahara yao kulingana na makosa waliyobainika kuyafanya.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo wtumishi wa kundi lilitakiwa kufikishwa katika vyombo vya sheria ni Bw Edwin Nyamsekela,Bw Chacha Moseti,Bw Alex Bw Albinus na Samwel Coyhuku CAG akipendekeza kesi ikianza itabidi watumishi hao wasimamishwe kazi mpaka kesi itakapomalizaka.

No comments:

Post a Comment