HALI YA UOKOAJI BADO INAENDELEA
Huku kukiwa bado na tarifa zenye utata juu ya idadi kamili ya waliokufa
katika ajali ya meli huko Zanzibar ,mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi
Kavu na Majini (SUMATRA) imesema, meli iliyozama leo, katika kisiwa cha
Chumbe, Zanzibar ilikuwa na abiria 248 wakiwemo watoto 31.
Taarifa
ya mamlaka hiyo hiyo imesema, meli hiyo, Mv Skagit iliondoka katika
Bandari ya Dar es Salaam leo saa sita mchana, ikiwa na mabaharia tisa.
Kwa
mujibu wa Sumatra, meli hiyo, inamilikiwa na Kampuni Seagul Transport,
imasajiliwa na Mamlaka ya Usafiri Baharini Zanzibar (ZMA) na kwamba,
Cheti cha Ubora kimeanza tarehe 24 Agosti, 2011 na kinamalizika 23
Agosti, 2012. Imesema, meli hiyo ilikuwa imeruhusiwa kubeba abiria
wanaoruhusiwa 300 na tani 26 za mizigo.
“SUMATRA
kupitia Kituo cha Utafutaji na Uokoaji (MRCC) ilipata taarifa kuwa
meli ya MV Skagit iliyokuwa safarini kutoka Dar es Salaam kuelekea
Zanzibar ilikuwa inazama katika eneo la karibu na kisiwa cha Chumbe,
Zanzibar, eneo ambalo lipo umbali wa Kilomita za Bahari 13.8 kutoka
Bandari ya Zanzibar” imesema taarifa hiyo.
Kwa
mujibu wa Sumatra, baada ya kupata taarifa hizo, kituo cha MRCC
kilitoa taarifa kwa vyombo vya ulinzi na usalama pamoja na vyombo vya
usafiri wa majini vilivyokuwa karibu na eneo la tukio.
“
Zoezi la uokoaji linaendelea katika eneo la tukio kwa msaada wa vyombo
vifuatavyo: Mv Flying Horse, Mv Kilimanjaro III, Tug Bandari ya
Zanzibar, KMKM, Mv Zanzibar I, Police Patrol Boat, Navy” imesema
taarifa hiyo.
Picha kwa Hisani ya Michuzi Blog
No comments:
Post a Comment