UKWELI ni kwamba mamilioni ya watu duniani wanaifahamu nchi ya Brazil,
hususan kutokana na umaarufu wake katika soka. Lakini ni wachache
wanaowafahamu marais waliowahi kushika madaraka katika nchi hiyo kwa
miaka nenda rudi.
Aidha, ni watu wachache wapenzi wa nchi hiyo
ya Kusini mwa Bara la Amerika na ya tano kwa ukubwa wa eneo duniani
ikiwa na watu milioni 192, wanafahamu kwamba rais wake wa sasa ni
mwanamke.
Ni Dilma Roussef, mama mwenye wajihi na umbo la kuvutia kwa wanaume na wanawake licha ya kuwa na umri wa miaka 64 sasa.
Roussef ambaye majina yake kamili ni Dilma Vana Roussef, aliweka rekodi
katika nchi hiyo kwa kuwa mchumi (economist) wa kwanza kushika nafasi
hiyo nchini Brazil.
Dilma, aliyezaliwa Desemba 14, 1947 nchini Brazil na akashika wadhifa wa urais January mosi,2011,ni rais wa 36 wa nchi hiyo tangu Wareno kutoka Ulaya walipoondoka katika nchi hiyo
Rais Roussef ana mtoto mmoja wa kike aitwaye Paula aliyempata akiwa na mwanasiasa Mwenzake Carlos Araujo
No comments:
Post a Comment