Redds' miss Mara 2012 kupatikana june 29
Na Shomari Binda
Musoma,
Shindano la kumtafuta Redd's miss Mara 2012 litafanyika June 29 huku waandaji wa shindano hilo kampuni ya Homeland Entertainment$Promotion wakidai
asilimia kubwa ya maandalizi ya shindano hilo yamekwisha kukamilika na
kinachosubiliwa ni kumpata mrembo wa Mkoa huo atakaye shiriki katika
shindano la Redd's miss Tanzania 2012.
Akizungumza na waandishi
wa Habari katika kambi ya mazoezi ya warembo wanaotarajiwa kushiriki
katika kinyang'anyiro hicho,mkurugenzi wa kampuni ya Homeland Goldon
Mkama alisema anawashukuru wale wote ambao wameshiliiki kwa namna moja
ama nyingine kutaka kufanikisha shindano la mwaka huu.
Alisema
licha ya ugumu wa shughuli za kuandaa shindano hilo la warembo lakini
anashukuru mpaka sasa kukamilika kwa asilimia kubwa ya maandalizi yake
na kusema kuwa bado kuna nafasi kwa wale wanaohitaji kushiriki kwa namna
moja ama nyingine ili kuweza kufanikisha shindano hilo.
Mkama
alidai kuwa mpaka sasa warembo 8 wameshafika kambini na kuendelea na
mazoezi kwa ajili ya shindano hilo waliopo chini ya msimamizi wa mazoezi
hayo miss Lindi na miss Tanzania namba 3 2011Loveness Flavian ambaye
kazi yake kubwa ni kuhakikisha warembo watakao shiriki shindano la
Redd's miss Mara 2012 wanafanya vizuri.
Muaandaji huyo wa miss
Mara 2012 aiwataja warembo ambao wapo kambini mpaka sasa kwa ajili ya
kushiriki shindano hilo kuwa ni Rose James,Jacline Mzava,Aisha
Bakari,Eugenia Fabian,Jesca Sprian,Justina Thomas,Love Kilasira pamoja
na Hellen Mosha
Aidha mkurugenzi huyo wa kampuni ya Homeland
aliishukuru kampuni ya African Gold Mine (North Mara) kwa kuendela kuwa
mstari wa mbele kwa kutoa udhamini mkubwa kila mwaka katika shindano la
kumtafuta mrembo wa miss Mara.
Aliwataja watu wengine
waliojitokeza kudahamini shindano hilo kuwa ni chuo cha Musoma Utalii
collage,Crdb banki,Coca cola,Maltivilla hotel,Mara security guard,Musoma
club,Msendo mini super market pamoja na mtandao wa Shommibindablogspot $
Bindanews.
Aliongeza kuwa katika kusindikiza shindano hilo
wasanii mahili wa muziki wa bongo freva Profesa J pamoja na Sharo
millionea pamoja na dansa wa twanga pepeta Bokilo Bokilo wanatarajiwa
kunogesha shind
No comments:
Post a Comment