MUSOMA
MAMLAKA
YA UDHIBITI WA USAFIRI WA NCHI KAVU NA MAJINI SUMATRA MKOANI MARA IMESEMA
KUANZIA JUNE 30 MWAKA HUU DALADALA ZOTE
ZINAZOBEBA ABIRIA KUANZIA MMOJA MPAKA 14 HAWATAENDELEA KUPEWA LESENI
HUKU GARI ZINAZOBEBA ABIRIA KUANZIA 15
MPAKA 25 WATAPEWA LESINI KWA SAFARI
ZISIZOZIDI KILOMITA 100
AKIONGEA
NA WAANDISHI WA HABARI MJINI MUSOMA LEO,AFISA MFAWIDHI WA SUMATRA MKOANI MARA
KAPTENI MICHAEL EDWARD AMESEMA LENGO LA KUFANYA HIVYO NI KUTOA VISINGIZIO KWA
WASAFIRISHAJI NA KUONDOA MFUMUKO WA BEI UNAOSABABISHWA NA GARI NDOGO ZINAZOENDA
SAFARI NDEFU.
AMESEMA
KUMEKUWEPO NA MALALAMIKO YA MARA KWA MARA KUTOKA KWA WANANCHI MKOANI MARA
KUTOKANA NA WASAFIRISHAJI KUPANDISHA GHARAMA ZA USAFIRI KIHOLELA PASIPOKUJUA
SABABU ZA WAMILIKI HAO WA MAGARI KUFANYA HIVYO.
KAPTENI
MICHAEL EDWARD AMESEMA ANASHANGAZWA NA KITENDO CHA WAMILIKI WA USAFIRI MKOANI
MARA KUPANDISHA GHARAMA BILA KUFUATA MUONGOZO WA SUMATRA KITU AMBACHO NI
KINYUME NA TARATIBU ZILIZOPO,AMESEMA SI KWELI GHARAMA HIZO ZINATO KANNA NA
KUPANDA KWA VIPULI NA MAFUTA KWA HIVI SASA.
AIDHA
KAPTENI MACHAEL EDWARD AMESEMA NI VYEMA TARATIBU ZIKAFUATWA KWA MMILIKI YEYOTE
ANAETAKA KUPANDISHA GHARAMA IKIWEMO KUANDIKA BARUA KWA MAMLAKA HUSKA NA
MUOMBAJI KUTOA TANGAZO LISILIZIDI SIKU ISHIRINI NA MOJA.
KUHUSU
GHARAMA ZA DALADALA MJINI MUSOMA,KAPTENI HUYO AMESEMA KUWA GHARAMA SAHIHI ZA
DALADALA MJINI MUSOMA NI SHILINGI 300 NA SI SHILINGI 400 NA MSAFIRISHAJI
ATAKAEKWENDA KINYUME NA BEI ATAKUWA AMEVUNJA SHERIA.
KWA
UPANDE WA NAULI YA TARIME AMESEMA NAULI HALALI NI SHILINGI ELFU 3000 NA SI
SHILINGI 4000 KAMA BAADHI YA WASAFIRISHAJI WANAVYOFANYA KWASASA,KAPTENI EDWARD
AMEWATAKA WANANCHI KUZIKATAA BEI HIZO HUKU AKITOA WITO KWA WAMILIKI WA MAGARI
YA USAFIRISHAJI KUFUATA SHERIA HUKU AKISEMA SUMATRA MAKAO MAKUU KWASASA
WANASHUHGULIKIA SULA LA BEI NCHI NZIMA.
No comments:
Post a Comment