NA MAGRETH KINABO – MAELEZO
WAZIRI
wa Ujenzi,Dk. John Magufuli amemtaka mkandarasi wa ujenzi wa Barabara
ya Mabasi yaendayo kasi(DART) yenye urefu wa kilomita 21 na vituo vya
mabasi 29 kutoka Kimara hadi Kivukoni iliyoko Jijini Dares Salaam
kufanya kazi usiku na mchana ili kuhakikisha .
Kauli
hiyo imetolewa na Waziri Magufuli leo wakati alipotembelea miradi hiyo
miwili ili kungalia shughuli za ujenzi ambapo alifurahishwa na kazi
hizo huku akiwataka wamalize kwa muda unaotakiwa.
“Mkandarasi
unatakiwa kufanya kazi usiku na mchana ili kazi ikamilike kabla ya
wakati kampuni yenu ni kubwa kama kuna matatizo yoyote mtuambie sisi
serikali ili tuweze kuyashughulikia,” alisema Waziri Magufuli.
Waziri
Magufuli pia ametoa muda wa siku saba kwa Shirika la Ugavi wa Umeme
Tanzania(TANESCO) na Mamlaka ya (DAWASA) kuondoa miundombinu yao
haraka ili kuepusha ucheleweshaji wa mradi wa DART.
Waziri
wa Magufuli alitembelea ujenzi huo katika maeneo ya Jangwani na Ubungo,
ambapo alisema itagaharimu sh. bilioni 240 na ikijumwuishwa na ujenzi
mwingine wa vituo utagharimu jumla ya bilioni 288 ambazo zimetolewa na
Serikali na Benki ya Dunia.
Awali
Meneja wa mradi , Frank Rohde kutoka kampuni hiyo , alisema
changamoto inayoukumba mradi huo ni ucheleweshaji wa vifaa vya ujenzi
huo kutoka bandarini ambapo vimekaa kwa muda wa siku saba.
Akizungumzia
kuhusu tatizo hilo Waziri Magufuli alisema atazungumza na Wizara ya
Fedha na Mamlaka ya Mapato(TRA) ili vifaa hivyo vitolewe haraka.
Aidha
Waziri Magufuli amemtaka Mkandarasi na Mshauri wa upanuzi wa barabara
ya Mwenge hadi Tegeta kutoka kampuni ya Konoike ya Japan kuhakikisha
wanamaliza ujenzi wa barabara hiyo yenye urefu wa kilomita 12
inayogharimu sh. bilioni 88 kwa muda unaotakiwa na kuacha kusingizio cha
mvua kama wanavyodai kuwa umechelewa kwa asilimia saba.
“Mvua
zilinyesha siku tatu haiwezi kuwa sababu kuna nchi mvua inayesha muda
mrefu kuliko Tanzania na ujenzi wa barabara unaendelea. Sijaridhika na
hiyo sababu ninyi nchi za nje mnaweza kujenga hata mvua ikiwa inayesha.
Ni lazima wafidie muda … kuongeza kazi ya ujenzi hakutakuwa na ongezeko
la muda wala mtaji,” alisisitiza.
Wakati
huohuo Waziri Magufuli alitumia nafasi kuwataka wakazi wa Jiji hilo
waliojenga katika maeneo ya hifadhi za barabara hizo kuondoka wenyewe
kwa kuwa sharia ni msumeno.
“ Tukikuta mradi unakwamishwa sisi tutabomoa.
Akizungumzia
kuhusu mradi DART , Afisa Mtendaji wa DART Cosmas Takule alisema
utatengeneza ajira 80,000 na kusaidia abiria 406,000. Mradi huo
utakamilika katika kipindi cha miezi 36.
Kwa upande wake Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dares Salaam , Mwamtumu Mahiza alitka ajira hizo ziwe kwa vijana wa jiji hilo.
No comments:
Post a Comment