Wednesday, May 16, 2012

MUSOMA

WAKUU WAPYA WA WILAYA MKOANI MARA WAMEAPISHWA LEO NA MKUU WA MKOANI WA MARA KATIKA UKUMBI WA UWEKEZAJI MJINI MUSOMA.


WAKUU HAO NI KUTOKA KATIKA WILAYA YA MUSOMA ,WILAYA MPYA YA BUTIAMA,WILAYA YA BUNDA,WILAYA YA TARIME,WILAYA YA SERENGETI NA WILAYA YA RORYA.


AKIONGEA NA VICTORIA FM MARA BAADA YA KUAPISHWA MKUU WA WILAYA YA MUSOMA BW JACKSON MSOME AMESEMA KUWA ANAMSHUKURU MH RAIS KWA UTEUZI WAKE HIVYO ANAOMBA USHIRIKIANO KWA WANANCHI WA WILAYA YA MUSOMA.


AIDHA KWA UPANDE WA MKUU WA WILAYA YA BUNDA BW JOSHUA MIRUMBE AMESEMA ATAHAKIKISHA ANADUMISHA SUALA LA ULINZI NA USALAMA KATIKA WILAYA HIYO HUKU AKIWEKA WAZI VIPAUMBELE VYAKE KUWA NI AFUA,MAJI,ELIMU IKIWA NI NJIA YA KUPUNGUZA UMASKINI KWA WANANCHI.


NAYE MKUU WA MKOA WA MARA BW JOHN GABRIEL TUPPA AKIONGEA NA VICTORIA FM AMESEMA KUWA KWA NAFASI YAKE ATAHAKIKISHA UTEKELEZAJI KATIKA MIPANGO ILIYOWEKWA HIVYO ANAIMANI NA WAKUU WA WILAYA KUISIMAMIA VYEMA.


MKUU WA MKOA AMEWAASA WANANCHI KUWAPA USHIRIKIANO WAKUU HAO WA WILAYA ILI KUTEKELEZA MIPANGO YAO KATIKA JAMII HUSKA,AMESEMA HAKUNA MAENDELEO YANAYOKUJA BILA KUWEPO NA UWAJIBIKAJI.

,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,
HALMASHAURI YA MANISPAA YA MUSOMA INAKUSUDIA KUTUMIA ZAIDI YA SHILINGI BILIONI 1 NA MILIONI 500 KATIKA MIRADI MBALIMBALI YA MANISPAA HIYO.

AKIWASILISHA HOTUBA YA BAJETI YA HALMASHAURI ZA MKOA WA MARA KWA WAJUMBE WA KAMATI YA USHAURI YA MKOA WA MARA RCC KWA NIABA YA KATIBU TAWALA WA MKOA WA MARA,AFISA MPANGO WA MKOA WA MARA BW.MGABE AMESEMA HALMASHAURI YA MANISPAA YA MUSOMA INAKUSUDIA NUNUA GARI LA KUSOMBEA TAKA NGUMU KWA SHILINGI MILIONI 130,KULIPA FIDIA ZA ARDHI KUANZIA MWAKA 2000 MPAKA 2012 KWA ZAIDI YA SHILINGI MILIONI 447.


KATIKA TAARIFA HIYO IMEELZWA KUWA UNUNUZI WA GARI LA MKURUGENZI WA MANISPAA LITAGHARIMU ZAIDI YA SHILINGI MILIONI 150 HUKU UJENZI WA MADARAJA,MAKALVATI NA MITARO YA MAJI MACHAFU UTAGHARIMU KIASI CHA SHILINGI MILIONI 500


AIDHA KATIKA TAARIFA HIYO IMESEMA KUWA UJENZI WA MAKAO MAKUU YA YA HALMASHAURI YA MANISPAA YA MUSOMA ITAGHARIMU KIASI CHA SHILINGI MILIONI 300.

,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,

BAADHI YA VIONGOZI WA DINI NA WAJUMBE WA KAMATI YA USHAURI YA MKOA WA MARA RCC,WAMESEMA SERIKALI INAPASWA KUPUUZA MADAI MBALIMBALI YANAYACHELEWESHA UJENZI WA BARABARA YA MUSOMA HADI ARUSHA KUPITIA SERENGETI NA KIWANJA CHA NDEGE CHA KIMATAIFA KINACHOTARAJIWA KUJENGWA MJINI MUGUMU, KWA KUWA HOJA ZINAZOJENGWA NA BAADHI YA WATU HAZINA MSINGI WOWOTE BALI ZINALENGA KUWANYIMA HAKI WANANCHI WA MAENEO HAYO.


WAJUMBE HAO AKIWEMO ASKOFU WA KANISA KATOLIKI JIMBO LA MUSOMA MHASHAM MICHAEL MSONGANZILA NA KAIMU MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA SERENGETI BW JUMANNE KWIRO,WAMEYASEMA HAYO MJINI MUSOMA KATIKA KIKAO CHA RCC HIVI KARIBUNI ,AMBAPO WAMESEMA KUNA BAADHI YA WATU WA NJE WAMEKUWA WAKITUMIA WATANZANIA WACHACHE KWA KUWALIPA FEDHA ILI KUSHINIKIZA KUTOTEKELEZWA KWA MIRADI HIYO MUHIMU


HATA HIVYO MENEJA WA WAKALA WA BARABARA TANROADS MKOA WA MARA,MHANDISI EMANUEL KOROSO,AKIZUNGUMZA KATIKA KIKAO HICHO,AMESEMA TAYARI UPEMBUZI YAKINIFU WA BARABARA HIYO KUTOKA MUSOMA KUPITIA SERENGETI HADI MTO WA MBU MKOANI ARUSHA,UMEKAMILIKA NA KWAMBA UJENZI WAKE UTAJENGWA KWA AWAMU IKIWA NI KUTEKELEZA AHADI YA RAIS JAKAYA KIKWETE YA KUFUNGUA MAWASILIANO KATIKA MAENEO HAYO NA KUEPUSHA WANANCHI WAKE KUPITIA NCHI JIRANI KWENDA MIKOA YA KASKAZINI MWA NCHI


WAKATI HUO HUO MKUU WA MKOA WA MARA BW JOHN TUPA,AKIZUNGUMZA KATIKA KIKAO HICHO,AMEVITAKA VYOMBO VYA DOLA KUCHUKUA HATUA ZA HARAKA KWA WATENDAJI WA HALMASHAURI ZA MUSOMA,RORYA,SERENGETI NA BUNDA AMBAO WANADAIWA KUSHIRIKIANA NA MAWAKALA WA PEMBEJEO KUIBA PEMBEJEO ZA KILIMO KISHA KUZIUZA NA KUGAWANA FEDHA BADALA YA KUWAFIKISHIA WAKULIMA PEMBEJEO HIZO

,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,

BUNDA


VIJANA WILAYANI BUNDA MKOANI MARA WAMEHIMIZWA KUJITOKEZA KATIKA MCHAKATO WA MAREKEBISHO YA KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA.


AKIWAHUTUBIA WANANCHI WA WILAYA YA BUNDA KATIKA HITIMISHO LA MICHUANO YA ESTHER BULAYA ILIYOFANYIKA KWA WIKI MBILI WILANI HUMO,MHE ESTHER BULAYA MBUNGE WA VITI MAALUM KUTPITIA VIJANA WA CHAMA CHA MAPINDUZI MKOANI MARA AMESEMA KUWA VIJANA WAMEKUWA WAKILALAMIKA KATIKA NYANJA MBALIMBALI HIVYO MUDA UMEFIKA WA KUSHIRIKI KATIKA KUTOA MATATIZO YAO.


AMESEMA KATIBA NDIYO MSINGI WA KILA KITU HAPA NCHINI HIVYO VIJANA WASIBEZE ZOEZI HILO NA LIKAFANYWA NA WAZEE BAADAYE WAANZE KULALAMIKA KITU AMBACHO HAKITAWASAIDIA.


MH BULAYA AMESEMA KUMEKUWEPO NA CHANGAMOTO MBALIMBALI AMABZO ZINAWAKABILI VIJANA NA KUJIKUTA WANAJIINGIZA KATIKA MAMBO YASIYOFAA KATIKA JAMII.

,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,

No comments:

Post a Comment