MRADI MKUBWA WA MAJI KUGHARIMU MILIONI 30 BUNDA
BENKI YA DUNIA KWA KUSHIRIKIANA NA SERIKALI YA TANZANIA,IKO
KATIKA HATUA ZA MWISHO ZA UKAMILISHAJI WA MRADI MKUBWA WA MAJI KUTOKA ZIWA
VICTORIA AMBAO UTAGHARIMU ZAIDI YA
SHILINGI BILIONI 30 NA HIVYO KUWEZESHA MJI WA BUNDA NA VITONGOJI VYAKE ZIKIWEMO
TAASISISI MBALIMBALI KUPATA MAJI YA
UHAKIKA,SAFI NA SALAMA.
HAYA YAMESEMWA MJINI BUNDA NA MWAKILISHI WA WIZARA YA MAJI
NA UMWAGILIAJI MHANDISI BONIPHACE MWITA,WAKATI AKITOA TAARIFA ZA UTEKELEZAJI WA
AWAMU YA PILI YA MRADI HUO,UNAFANYWA NA KAMPUNI YA UJENZI YA NYAKIRANG’ANI KWA
WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS MAHUSIANO NA URATIBU MH STEPHEN WASSIRA,AMBAYE
AMETEMBEA NA KUKAGUA MAENDELEO YA MRADI HUO.
KWA UPANDE WAKE MH
WASSIRA,AKIZUNGUMZA BAADA YA KUFANYA UKAGUZI HUO,AMESEMA MRADI HUO UNAJENGWA NA
SERIKALI KWA USHIRIKIANO NA BENKI YA DUNIA NI UTEKELEZAJI WA AHADI YA RAIS
JAKAYA KIKWETE KWAAJILI YA KUWAPATIA
MAJI YA UHAKIKA WANANCHI WA MJI WA BUNDA AMBAO WAMEKUWA WAKIKABILIWA NA TATIZO
KUBWA LA UKOSEFU WA HUDUMA HIYO MUHIMU.
NAO BAADHI YA WANANCHI WA WILAYA YA BUNDA,WAMEISHUKURU
SERIKALI KWA UAMUZI WAKE WA KUTEKELEZA MRADI HUO,AMBAPO WAMESEMA KUKAMILIKA KWA
MRADI HUO MKUBWA KUTAWAWEZESHA KUONDOKANA NA TATIZO LA MUDA MREFU LA UKOSEFU WA MAJI
Mji wa Bunda unavyoonekana
No comments:
Post a Comment