Tuesday, April 10, 2012

          TUMEJIFUNZA NINI KATIKA MSIBA WA KANUMBA (THE GREAT) SISI VIJANA?

Ndugu zangu watanzania poleni sana kwa msiba wa ndugu yetu tuliyempenda sana kupitia nafasi yake ya uigizaji,Najua mmechoka sana kutokana na shughuli hiyo ya kumweka Ndugu yetu katika Nyumba yake ya Milele ambapo watu wanasema hataonana c kweli Mtaonana na Kanumba tu ipo siku naamini hivyo.Tukiwa bado katika maombolezo ya msiba huo tumejifunza nn sisi tuliobaki na ambao ck zote tunasema cc wasanii ni kioo cha Jamii? Waliohudhuria katika mazishi hayo c wehu au labda hawakuwa na kazi za kufanya bali wameumia kwa kukosa kile ambacho walizoea kukipata kupitia Filamu za Kanumba "THE GREAT" nami pia nitakosa sana aina fulani ya uigizaji wa Kanumba.






Kanumba kazikwa hivyo kwa sababu nyingi sana baadhi ni kwamba

1.Ni mmoja ya msanii ambaye hakuwa na skendo ambazo zilikuwa zinaleta picha mbaya katika jamii na katika Tasnia hiyo ya Filamu na hata pale waaandishi walipotaka kuuza Gazeti aliwakemea huyo ni msanii makini sana
2.Hakuwa mbinafsi kwani tumeshuhudia vijana wengi kawaibua katika Filamu zake mbalimbali
3.Hakuwa na Majivuno Kwa kiwango alichokuwa amefika Kanumba leo angetafuta watu fulani wa kuongea nao lakini hakuwa hivyo
4.Alipenda jamii ndiyo maana aliweza kutoa misaada mbalimbali kwa makundi tofauti
5.Hakukatishwa na Maneno ya watu wasiopenda mafanikio ya wenzao
6.Aliipenda sana nchi yake kwa dhati na popote alipenda kusema natoka Tanzania
7.Kanumba hakubagua huyu wala yule ndiyo maana kazikwa na watu wengi wa rika tofauti
8.Alikuwa kiongozi kwa wenzake.
9.Alichukia umaskini.
10.Kanumba alijipenda

Hayo ni baadhi ya mambo ambayo niliyajua kwa Kanumba baada ya kuwa na Mafanikio ya haraka katika tasnia ya Filamu,nilitamani sana kufika katika mazishi lakini sikuweza,aaaaah Kanumba ipo siku nitafika kwenye kaburi lako japo niseme neno ambalo siku zote nilipenda nikwambie lakini sikuweza kukutana nawe na hilo neno ni hili hapa HONGERA KAKA KWA KAZI ZAKO hili neno sijakwambia lakini ipo siku nitakwambia tutakapokutana katika uzima wa Milele

No comments:

Post a Comment