Wednesday, April 11, 2012

                      ALIYOSEMA KANUMBA YAMETIMIA..

 

 Unaweza usiamini lakini ndio ukweli wenyewe..
Nathubutu kusema kuwa Kanumba ni mmoja kati ya wasanii ambao vifo vyao au matukio yatakayotokea wakati wa msiba wao waliyajua..

Katika wimbo wake marehemu Steven Kanumba uitwao 'NITAYAINUA MACHO YANGU' marehemu Kanumba ameongea mambo ambayo bila kupinga yametokea kabisa.

                    STIVEN KANUMBA " THE GREAT "

Marehemu Kanumba katika wimbo huo anasema kwamba "siku nikifa kila mtu ataongea anavyojua, eti kwamba tumepoteza msanii wetu, eti pengo la Kanumba halitazibika.."
Ni kweli na kauli hizo zimesemwa sana katika kipindi chote cha msiba.

Pia kuna maneno yaliyosema " Hata wale wanaonichukia ndio watabeba jeneza langu na kuimba nyimbo za huzuni."
Hiyo nayo ni kweli kwani hakuna asiyejua kuwa Kanumba na Ray walikuwa hawapatani, lakini Ray alikuwa mmoja kati ya watu waliobeba jeneza lake..

No comments:

Post a Comment