SERENGETI
BARAZA la madiwani wa Halmashauri la Wilaya ya Serengeti Mkoani Mara,limeunga mkono msimamo wa Rais Jakaya Kikwete wa kutaka kujengwa barabara ya lami kutoka Musoma hadi Mto wa mbu.
Kaimu mwenyekiti wa halmashauri ya Serengeti Bw Jumanne Kwiro,akizungumza katika kikao cha dharua za kupitisha bajeti ya ya mwaka 2011/2012 amesema baraza hilo linaunga mkono uamuzi wa Rais Kiwete kuhusu ujenzi wa barabara hiyo kwaajili kuharakisha maendeleo wananchi wa Serengeti na mkoa wa Mara kwa ujumla.
Katika hotuba yake ya kufungua kikao hicho maalumu, ambacho kimefanyika mjini Mugumu,Bw Kwiri amesistita kuwa wanaserengeti wanaunga mkono ujenzi wa barabara hiyo ambayo itafungua milango ya uwekezaji na kuinua uchumi wa eneo hilo.
Amesema hoja ya kwamba kujengwa barabara kwamba kutaharibu mazalia ya nyumbu na kuhatarisha shughuli za uhifadhi katika hifadhi ya taifa ya Serengeti haina msingi kwa madai kuwa wananchi wa Serengeti wamekuwa wahifadhi wazuri kwa miaka mingi hivyo wanaimani kuwa ujenzi wa barabara hiyo hautakuwa na maadhara yoyote kwa wanyama.
Kauli hiyo imeungwa mkono na baraza zima ambalo pia limehudhuriwa na Mkuu wa Wilaya ya Serengeti Lt mstaafu Edward Lenga, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashuri hiyo Bw Kimulika Galikunga na wataalamu wa idara mbalimbli za serikali.
AIDHA KIKAOP HICHO KIMEtumia nafasi hiyo pia kulaani baadhi ya wanaharakati wa mazingira ambao wamekuwa wakipinga ujenzi wa barabara hiyo kwa madai kuwa itakuwa na maadhara yasiorekibishika kwa wanyama pori .
Hata hivyo serikali ya Tanzania imesisitiza mara kwa mara kuwa sehemu ya barabara hiyo ambayo iko ndani ya hifadhi ya Serengeti haitajengwa kwa kiwango cha lami,Ujenzi wa barabara hiyo unalenga kuboresha maisha ya wananchi wanaozunguka hifadhi ya Serengeti Kwa upande wa mikoa ya Arusha na Mara.
,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,
No comments:
Post a Comment