Na Moahammed Mhina, wa Jeshi la Polisi -Zanzibar
ZANZIBAR
JUMATANO APRILI 11, 2012 Jeshsi la Polisi Zanzibar limewataka wananchi
kutovunjika
moyo na kuacha kushirikiana na Jeshi hilo katika kukomesha vitendo vya
kihalifu kwa kuwaona watuhumiwa waliokamatwa wakiwa nje kwa dhamana.
Rai
hiyo imetolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi Zanzibar
Kamishna Msaidizi Aziz Juma Mohammed, wakati akitoa elimu juu ya utii wa
sheria bila shuruti na Ulinzi Shirikishi.
Kamanda
Aziz amesema kuwa idadi kubwa ya washukiwa wa wanaokamatwa hutuhumiwa
kwa makosa yanayotoa uhuru wa dhamana kisheria kwa mtuhumiwa.
Amesema
mtuhumiwa anaweza kukamatwa na kupewa dhamana akiwa katika kituo cha
Polisi ama Mahakamani kwani hiyo nayo ni haki ya mtuhumiwa
Hata
hivyo Kamanda Aziz amesema kuwa kila mwananchi hasa waliotendewa
matukio ya kihalifu wanayofursa ya kwenda kituo cha Polisi ama
mahakamani kuulizia maendeleo ya kesi inayomhusu.
Lakini
amesema watuhumiwa wengi wanapopewa dhamana ya Polisi ama ya mahakama
wamekuwa wakitamba mitaani kuwa wametoa hongo jambo ambalo amesema
limekuwa likiongeza idadi ya tuhuma za rushwa katika taasisi za Polisi
na Mahakama.
Amewahimiza
wale wote wanaoshuhudia
matukio ya kihalifu kuwa tayari kwenda Polisi kutoa maelezo yao na
baadaye kwenda Mahakamani kutoa ushahidi wa yale aliyoyashuhudia ili
kuiwezesha Mahakama kutoa uwamuzi wa haki kwa pande zote mbili.
Kamanda
Aziz amesema hakuna mtuhumiwa atakayepatikana na hatia mahakamani
pasipokuwepo kwa ushahidi wa kutosha kuwezesha mahakama kuthibitisha
kosa.
“Ukitoa
maelezo yako Kituo cha Polisi na ukaacha kwenda kuielezea mahakama juu
ya kile ulichokishuhudia haitoshi na hivyo mtuhumiwa anaweza kufutiwa
shitaka lake”. Alisema Kamanda Aziz.
Hivi
sasa Jeshi la Polisi Visiwani Zanzibar kupitia kwa Makamanda wa Polisi
wa Mikoa wakiongozwa na Kamishna wa Polisi Visiwani humo CP. Mussa Ali
Mussa, linaendelea na mkakati wake wa kutoa elimu kwa wananchi juu ya
utii wa sheria bila shuruti pamoja na haki za watuhumiwa.
Mwisho
No comments:
Post a Comment