JESHIO LA POLISI ZANZIBAR LAPATIWA MSAADA WA PIKIPIKI KUMI
Na Mohammed Mhina, wa Jeshi la Polisi Zanzibar
ZANZIBAR JUMANNE APRILI 17, 2012. Jeshi la Polisi Zanzibar leo
limepokea msaada wa pikipiki kumi kutoka Kampuni ya Simu za Mkononi ya
Zantel ili kusaidia kutatua tatizo la usafiri kwa Jeshi hilo .
Akikabidhi pikpiki hizo kwa niaba ya kampuni ya Zantel, Afisa masoko wa kampuni hiyo Bw. Mohammed Mussa, amesema
kuwa kampuni yake imeamua kutoa msaada huo ili kuwawezesha askari
Polisi kuweza kufika kwa haraka katika maeneo ya matukio.
Amesema
Kampuni yake inafahamu upungufu wa vitendea kazi unaolikabili Jeshi la
Polisi na kwamba wameona kuna umuhimu wa wao kama Kampuni kulisaidia
Jeshi hilo ili liweze kuwahudumia wananchi kwa haraka zaidi.
Aidha
Kamuni hiyo pia imeahidi kuendelea kulisaidia Jeshi la Polisi katika
masuala ya mawasiliano kama vile radio za mikononi ili kuvisaidia
vikundi vya ulinzi shirikishi katika maeneo mbalimbali visiwani humo.
Akipokea
msaada huo, Mkuu wa Utawala wa Jeshi la Polisi Zanzibar Kamishna
Msaidizi Mwandamizi SACP Keneth Kaseke, amesema pikipiki hizo zitasaidi
kwa kiasi kikubwa katika kukabiliana na matukio ya kihalifu hasa katika
maeneo yenye barabara finyu ya Mji Mkongwe.
Kamanda
Kaseke alikuwa amemwakilisha Kamishna wa Jeshi la Polisi Zanzibar CP
Mussa Ali Mussa, katika hafla hiyo ya kupokea msaada huo wa pikpiki kumi
aina ya MTR zenyethamani ya shilingi milioni 17.
Akizungumza
wakati wa hafla hiyo iliyofanyika Makao makuu ya Jeshi la Polisi
Zanzibar, Kamanda Kaseke ameishukuru kampuni hiyo ya Zantel kwa msaada
huo na isichoke kuendelea kulisaidia Jeshi hilo katika nyanja nyingine.
Kamanda
kaseke pia ametoa wito kwa Makampuni mengine hapa nchini kujitolea
kulisaidia Jeshi la Polisi katiak kupata misaada mbalimbali kwani
amesema bado Jeshi hilo linakabiliwa na upungufu mkubwa wa vitendea kazi
pamoja na samani za ofisi.
No comments:
Post a Comment