Thursday, January 19, 2012

KIKAO CHA KAMATI YA USHAURI YA MKOA WA MARA RCC CHAMALIZIKA LEO

Katika Kikao cha kamati ya mkoa wa Mara kilichomalizika leo mkoani hapa kimeagiza shule zote za msingi mkoani Mara  kuanza kutoa chakula cha katika shule hizo ili kumwezesha mtoto kusoka katika mazingira salama katika kufikiri,Katika kikao hicho mkuu wa mkoa wa Mara ambaye ndiyo mwenyekiti wa kikao hicho ameipongeza wilaya ya serengeti kwa kuanzisha utaratibu huo  na kuweza kufanikiwa  kwa asilimia kubwa.

 Wajumbe wa mkutano huo wakiwa makini katika kikao hicho leo mchana
  Ukumbi safiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii
                 Umakini ni jambo muhimu katika jambo lolote
         Mkuu wa mkoa wa Mara Bw John Gabriel Tuppa akiongea jambo katika kikao hicho,na hapo chini ni picha ya wanahabri wakiwa mitamboni katika kuifahamisha jamii kutoka kushoto ni Anna Mroso katikati Mwana wa Afrika na Mwisho Geroge Marato wa ITV


  Kuna wakati hali ilikuwa tete ukumbini hivyo tulitoka nje katika kuwacliana na watu wengine
 Moja ya mambo ambayo pia yalijadiliwa hii leo ni pamoja na kuongelea suala la kujengwa kwa hospital ya kwangwa ili iwe hospital ya rufaa ya mkoa wa Mara ambapo hazina walisema hawana fedha lakini wana Mara kwa kauli moja wamesema wataungana katika ujenzi huo,aidha mganga mkuu akisoma taarifa katika kikao hicho amesema harambee kubwa itafanyika jijini Dar es salaam ikiongozwa na Rais wa Tanzani Jakaya Mrisho Kikwete

No comments:

Post a Comment