Monday, August 15, 2011

MWANA WA AFRIKA IKIWA INATIMIZA MWAKA MMOJA,ASANTENI WADAU

Habari wana wa Afrika,Shukrani kwa ushirikiano wenu wadau kwa takribani mwaka mzima tangu nimeanzisha blog hii ya MWANA WA AFRIKA,Blog hii imenisaidia kujua mambo mbalimbali na pia kupata marafiki kutoka sehemu mbalimbali Tanzania na nje ya Tanzania.


Katika blog hii kuna habari  mbalimbali za kuelimisha,kusisimua, kuhuzunisha, kufurahisha, lengo likiwa ni kukuhabarisha na kutoa changamoto mbalimbali lengo likiwa ni kuijenga nchi yetu ya Tanzania,blog hii inatumia lugha mbili ambazo zinatumika Tanzania na dunia kwa ujumla yaani yaani Kiswahili na Kiingereza ingawa kiswahili kinapewa kipaumbele zaidi

Nimeanzisha blog hii August  21 mwaka jana nilipokuwa jijini Dar baada ya kuamini kuwa naweza kuanzisha chombo changu ambacho nitakitumia katika suala zima la kuupasha umma,kutoa maoni mbalimbali lengo likiwa kulijenga taifa letu,Mwana wa Afrika ni blog ambayo  unakuletea habari za kisiasa, kijamii na burudani na pia ni blog amabyo haifungamani na upande wowote zaidi ya maslahi ya Tanzania na watu wake na wala haina ushabiki na chama chochote cha siasa hapa nchini na Duniani kwa ujumla

Blog ya Mwana wa Afrika kwasasa bado itaendelea kuboreshwa zaidi lakini pia wewe mdau unakaribishwa  katika kuitumia blog hii ikiwa ni pamoja na kutuma picha au habari za matukio lengo likiwa  ni kuufahamisha umma wa Watanzania,hatutato habari ambazo zitaonekana kuwa za uchochezi juu ya jambo fulani,kumkashfu au kumkejeli mtu na pia habari za vitisho bali tutatumia habari za kiungwa zenye kuleta tija kwa jamii.

Asanteni wadau kutoka nchi mbalimbali ambao mnatembelea blog hii na nawaahidi kamwe sitawaangusha katika kuwapasha habari,Mungu awape nguvu

Afrika Itanjengwa na Waafrika
 Mwana wa Afrika

No comments:

Post a Comment