Sunday, August 14, 2011

HABARI KUTOKA WILAYANI BUNDA

LICHA ya Serikali kuwahakikishia wakazi wa mji wa Bunda kuwa watasherehekea miaka hamsini ya uhuru wa Tanganyika wakiwa na maji ya kutosha ahad hiyo imebairika baada kuelezwa wavumilie hadi mwezi Juni mwakani .


Akiongea mara baada ya kuutembelea mradi wa maji unaotekelezwa na Serikali mjini Bunda,Mkurugenzi wa maji mijini katika wizara ya maji na umwagiliaji Mhandisi Yohana Mwonjesa amesema hatua ambayo imefikiwa katika utekelezwaji wa maradi huo inatia moyo.


Hata hivyo mhandisi Yohana amesema kwa kuwa tatizo la maji limekuwa likiwatesa wakazi wa mji huo kwa muda mrefu na dhamira ya serikali ni kuhakikisha kuwa wanaondokana nalo kabisa basi itawalazimu kuivumilia serikali hadi mwezi Juni mwakani pale itakapoukailisha kabisa mradi huo.


Amesema kuwa ili kutimiza ndoto hiyo ya serikali, ameitaka mamlaka ya maji mjini Bunda (BUWSA) kusimika mashine na mabomba katika mfumo wa zamani wa maji unaotumiwa kwa sasa ili kuuwezesha kuongeza kasi ya kusukuma maji mengi zaidi kwa wakati kwa ajili ya kutumiwa na wakazi hao huku akiiagiza iongeze mtandao wa mabomba kwa wakazi.


Mapema akitoa taarifa kwa mkurugenzi huyo meneja wa mamlaka ya maji mjini Bunda (BUWSA) mhandisi Idd Swai alisema hadi sasa mradi huo utakaoighjarimu serikali zaidi ya shilingi bilioni 32 hadi utakapokamilika uko katika hatua ya pili ya utekelezwaji wake.


Mhandisi Swai amesema katika awamu hizo mbili kazi za usanifu,ujenzi wa matenki na nyumba za pampu za kusukumia maji pamoja na nyumba za watumishi,ununuzi wa mabomba zimeshafanyika na kukamilika huku kazi za kuchimba mitaro na kutandaza mabomba kutoka kwenye chazo kilichoko umbali wa km22 kutoka mjini bundaa pamoja na ujenzi wa chujio zikingojea awamu ya tatu.

 ,,,,,,,,,,,,,,,,,,//,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,//,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,         

VIKUNDI vya wakulima,wafugaji na wafanyibiashara ndogondogo vya kata ya Sazira wilayani Bunda katika mkoa wa Mara vimeunda mtandao kwa lengo la kujihakikishia urahisi wa upataji elimu juu ya uzalishaji wenye tija pamoja na uhakika wa masoko hali itakayowawezesha kujikwamua na umasikini.


Akiongea katika hafla ya uzinduzi huo makamu mwenyekiti wa mtandao huo Bw Yohana Matata, amesema uundwaji wa mtandao huo wenye vikundi 22 na wanachama 355 ni matokeo ya wajasiriamali hao kuchoshwa na ukosefu wa elimu ya kutosha juu ya uzalishaji wenye tija.



Amesema kupitia mtandao huo wanachama watapata urahisi wa kupata elimu hiyo kwa ukaribu kutoka kwa wataalam wa ugani na maofisa biashara hali itakayowawezesha wajikwamue na umasikini wanaokabiliwa nao tofauti na kukaa kila kikundi kivyake hali inayowawia vigumu wataalam hao kuwafikia kwa urahisi.

Kwa mujibu wa makamu mwenyekiti huyo mbali na kupatiwa elimu juu ya uzalishaji wenye tija pia wanachama wa mtandao huo watafundishwa namna ya kutambua fursa zilizopo katika maeneo yao na kuzitumia katika kujiokoa na dimbwi la umasikini pamoja na kuelimishwa umuhimu wa vyama vya kuweka na kukopa(SACCOS) ili waweze kukopeshana na kuinua mitaji yao.

Naye ofisa msimamizi wa shirika binafsi la VI-Agroforestry linalojishughulisha na kilimo mseto wilayani hapa linaloratibu vikundi hivyo Bw Kennedy Kitori amesema lengo la mtandao huo ni kuendeleza juhudi binafsi zilizooneshwa na wakulima wa kata hiyo katika kutafuta elimu ya uzalishaji wenye tija pamoja na masoko ili waondokane na umasikini na kwamba shirika hilo kwa ushirikiano na serikali litahakikisha kuwa mtandao huo unapatiwa wataalam husika mara kwa mara.


Kwa upande wake mgeni rasmi katika hafla hiyo Stafa Nashon ambaye ni ofisa Usafi na Mazingira wa wilaya ya Bunda licha ya kuwapongeza wakulima hao kwa uamuzi wao wa kuunda mtandao huo lakini aliwataka kuzingatia kwa umakini elimu ya uhifadhi mazingira kwa kupanda miti na kuepukana na kila kitendo cha kuyaharibu ili kuvutia mvua iliyo tegemeo kubwa la wakulima na wafugaji.

Mwisho

No comments:

Post a Comment