Wednesday, August 10, 2011

HABARI KUTOKA TARIME

TARIME
 
WILAYA ya Tarime mkoani Mara imeagizwa kufanya utafiti wa haraka utakalenga kuongeza vyanzo vya ndani vya mapato ambapo kwa kufanya hivyo kutawezesha halmashauri kupata fedha za kutosha katika kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo vijijini.
 
Agizo hilo limetolewa na katibu tawala mkoa wa Mara Bw Clement Lujaji,wakati wa kikao cha kawaida cha baraza la Madiwa wa halmashauri ya wilaya ya Tarime ambapo amesema maeneo yanayopaswa kuangaliwa na wilaya ya Tarime kwaajili ya kuongeza mapato ni pamoja na kupanua wigo biashara katika mpaka wa Tanzania na Kenya.
 
Katibu tawala huyo wa mkoa wa Mara,amesema miongoni mwa biashara ambazo zinapaswa kuanzishwa katika maeneo hayo ya mpakani ni pamoja minada ya mifugo na bidhaa zake hatua ambayo pia amesema itasadia kuinua hali ya wananchi kiuchumi.
 
Hata hivyo Bw Lijaji,amewataka madiwani wa halmashauri ya Tarime na halmashauri nyingine mkoani Mara,kusimamia kwa karibu matumizi ya fedha za umma zinazotolewa na serikali kwaajili ya utekelezaji wa mirasdi pamoja na kuchukua hatua kwa watendaji wanashindwa kutekeleza wajibu wao.
,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,//,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,//,,,,,,,,,,,,,,,,,,,
 
SERIKALI wilayani Tarime imetangaza mkakati maalum wa utakaowezesha kukabiliana wimbi la wizi wa mifugo kwa kuhusisha wananchi,viongozi wa vitangoji na vijiji vyote vya wilaya hiyo.
 
Mkuu wa wilaya ya Tarime Bw John Henjewele,amesema mkakati huo tayari umepitishwa na kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya,kwa kutaka kila mwananchi mwenye ng’ombe kuweka harama muhimu ya utambuzi pamoja na kujenga mazizi imara yasiyovutia wezi.
 
Amesema wilaya imetangaza kuwa endapo ng’ombe wataibwa katika eneo jambo la kwanza litakalo fanywa na kamati hiyo ni kujiridhisha kwa kuona uimara ya zizi lenyewe na endapo itabaini kutokuwa na zizi linalohitajika polisi watalazimika kumkamata mmiliki,mwenyekiti wa kitongoji na kijiji kisha kuwafikishwa mahakamani kwa kosa kufanya uzembe na kusababisha wizi huo.
 
Hata hivyo mkuu huyo wa wilaya akizungumza katika kikao cha baraza la madiwani la halmashauri ya wilaya ya Tarime,amesema pamoja na hali ya utulivu na amani ambayo imeanza kupatikana wilaya imekuwa ikifanya juhudi za kumaliza mgogoro kati ya wananchi wanazunguka mgodi wa North Mara na wawekezaji hao kampuni ya African Barrick Gold hasa katika kupitia mikataba.
 
Amesema viongozi wa vijiji vinavyozunguka mgodi huo ndio wamekuwa chanzo cha mahusiano mabaya kwa pande hizo mbili kwa vile waliingia mikataba na mgodi bila ya kushirikisha wananchi na uongozi wa wilaya jambo ambalo amesema tayati limeanza kushughulikiwa.
 
Kuhusu malalamiko ya wananchi kuhusu watendaji wa vijiji na kata kushindwa kuwahudumia wananchi katika maeneo yao,mkuu huyo wa wilaya ya Tarime ameita halmashauri kuanza kutaratibu maalum wa kupata taarifa za utendaji wa kazi wa viongozi hao na watakabainika kuwa kikwazo wafukuzwe kazi.
 
Mwisho

No comments:

Post a Comment