Thursday, July 14, 2011

ZAIDI YA WANAFUNZI 3000 T ARIME WANAKAA CHINI

zaidi ya wanafunzi 3000 Inakadiriwa kuwa  wanakaa katika shule nne tofauti  zinazozunguka mgodi wa  dhahabu wa North Mara wakati wa vipindi kutokana na uhaba wa madawati katika shule zao
 
Hali hiyo imebanika baada ya  waandishi wa habari kutembelea baadhi shule  na kushuhudia sehemu ya wanafunzi wakiwa wameketi chini ya vumbi  wakati vipindi vinaendelea.

 aidha shule ambazo inasemekana bado asilimia kubwa ya wanafunzi wanakaa chini ni shule ya ya   Nyakunguru A, Nyakunguru B, Nyamongo na  Nyangoto.
 
katika shule ya msingi Nyakunguru A  mwalimu mkuu Msaidizi wa shule hiyo Otaigo Machera  amesema kuwa Shule hiyo ina jumla ya wanafunzi  668 ina madawati 80 ambapo  Taarifa zinasema hali ni mbaya katika shule ya jirani.
 
AMESEMA SHULE HIYO ILIYOANZISHWA MWAKA 1958 LAKINI MPAKA SASA BADO HALI INAONEKANA KUWA MBAYA ZAIDI KATIKA SHULE HIYO AMBAYO PIA AFISA ELIMU WA WILAYA HIYO ALISOMA KATIKA SHULE HIYO.
 
Katika shule hizo majengo yanaonesha kuchAkAa na hayatumiki kiasi kwamba yanahatarisha maisha ya wanafunzi wanayoyatumia kama viwanja vya michezo,Hata hivyo uongozi wa kijiji cha Nyakunguru unatupiwa lawama kwa kuchelewesha  kukamilika kwa ujenzi  wa jengo la nyumba ya mwalimu miaka mitano sasa.
 
Kampuni ya African Barrick Gold ambayo inamiliki  mgodi wa dhahabu wa North Mara imekuwa ikidai kutumia mamilion ya pesa kuboresha huduma za jamii katika vijiji vinavyozunguka mgodi huo.

No comments:

Post a Comment