Thursday, July 28, 2011

UJIO KAMILI WA MSANII JOSEFLY KUTOKA TETEMESHA REC

Kijana anayefahamika kwa jina la JOSEFLY kulia ambaye ameshirikishwa na SAJNA katika wimbo wa MGANGA ameachia wimbo wake unaokwenda kwa jina la SIKUTAMANI akiwa amemshrikisha HUSSEN MACHOZI kutoka katika studio bora TANZANIA ya TETEMESHA REC ya jijini MWANZA

"SIKUTAMANI" LYRICS by JOSEFLY


Track Name: SIKUTAMANI
Artists: JOSEFLY FT. HUSSEIN MACHOZI
lyrics composed by: JOSEFLY
arranged by: JOSEFLY
Produced by: KID BWOY
Mixed by: KID BWOY
Studio: TETEMESHA RECORDZ



INTRO:
Josefly..flag pamoja (Josefly)
Sikutamani baby (Hussein machozi)

VERSE 1:
Kama mapenzi ni mvua you make acidic rain, hata niweke umbrella haitawork out baby,
Nishanyeshewa nimetota na ubaridi wa penzi, sio pingu minyororo mi kuikata siwezi,
Toka moyoni najiskia true love sio mapenzi ya kuigiza kesho nenda I don’t love You,
Japo naogopa Love kama mchezo wa mieleka hua napenda tu kuwatch ukijaribu utaaibika,
Sikutamani kisa uzuri ulionao, figure ilojengeka ama jinsi ulivyo na mng’ao,
Sikuhesabu kama pounds au dollar, kesho ukishuka thamani mi nikuone sakara,
Sijavutiwa na miguu au mitindo ya nywele, harufu ya perfume ama ulivojaza wezele,
Sio ma cutwalk, sauti nyororo ya kufanya vocal..ah..ah,
Sio blause ama jeans ama top na tight, hizo lips za kukiss or your beautiful eyes,
Sikuchukui kama order utakuja na expire date, ukipenda mng’ao akififia utaona fake, right!
Nausikiza moyo kama wosia wa mama Jose, usiyafate machokesho utaangukia lawama,
Moyo umekubali, you’re the ONE sio kwa zali, you’re ma lucky star sitaki tena vibatali,

CHORUS:(Hussein Machozi)
Tazama moyo wangu unaongea, na wewe
Sitamani figure yako nakupenda wewe
Tazama moyo wangu unaongea na wewe
Usije kuondoka nikabaki mwenyewe

BRDGE:
Nakupenda kwa moyo, sikutamani baby
Sikulambi kisogo, nakupenda wewe

VERSE 2: (Josefly)
We’ ni zaidi ya pacha kabla sijaliona jua, password ya maisha yangu we unaweza kuifungua,
Mi nakili' we ni mmoja kati ya ndoto zangu, unastahili’ upewe tuzo moja ya maisha yangu,
Nakuona kama story za Once upon a time, am the prince you are princes njoo nikuvishe crown,
You’re the one kati ya elfu kibao walonipita, we ni special kati ya best kibao nilowatupa,
Sitokuita X-GIRL or whatever ..nauhakika,
Wanaokutamani, hao akina flani, wanataka waonje wajue unaladha gani,
Wakutumie kusafisha nyota zao, kupandisha tittle lao, waku knock down wakimaliza shida zao,
Nifate mimi, moshi hauendi chini, Love inatoka moyoni blabla ziko mdomoni..
Tamaa’ inaweza kua ni chanzo cha kuwafanya jamaa,wakupe kila kitu ili mfanye sanaa,
Usiwasikize, watch your steps girl keep yourself busy
Yeah.. Sitokulinda kwa mikuki ,najipanga sikurupuki nakulinda na baya kwa mapenzi lukuki,
Njoo nikuoneshe paradise uisahau shida,sitosema nachelewa baby you’re ma time keeper.

CHORUS:(Hussein Machozi)
Tazama moyo wangu unaongea na wewe
Sitamani figure yako nakupenda wewe
Tazama moyo wangu unaongea na wewe
Usije kuondoka nikabaki mwenyewe

BRDGE:
Nakupenda kwa moyo,sikutamani baby
Sikulambi kisogo,nakupenda wewe

VERSE 3: (Josefly)
Ni obvious macho yanauconnect moyo, hisia nzuri hazifichiki hata akiwa nazo mchoyo,
Kuna tofauti kubwa kati ya love na tamaa, kama urafiki na ujamaa ama utakaso na zinaaa
Hah, am so crazy, kama naukichaa navoflow hizi tenzi,kama nawashwa upupu navojiskia mapenzi
Alright, usinikune kifuani’ ushanikuna ndani ya moyo, pamoja’ kama sanaa na bagamoyo
So, let me call you sunshine mahabuba ma honey, baby’ uko na mimi though I get no money
Usinichore tattoo,nshakuchora ndani ya moyo, sio hard core laini kama mdomo wa kibogoyo
Kwa hii nafasi hautajuta kama unavong’ata kucha sio kidole,unavosikiza ala za gitaa sio kelele

CHORUS:(Hussein Machozi)
Tazama moyo wangu unaongea na wewe
Sitamani figure yako nakupenda wewe
Tazama moyo wangu unaongea na wewe
Usije kuondoka nikabaki mwenyewe

BRDGE:
Nakupenda kwa moyo,sikutamani baby
Sikulambi kisogo,nakupenda wewe

Autro:
Yeah... It’s Josefly
Tetemesha production
 

No comments:

Post a Comment