RORYA
Chama cha
Mapinduzi CCM wilaya ya Rorya Mkoani
Mara kimesema hakitamvumilia mtu yeyote atakaeonyesha dalili ya kuleta
Malumbano na mgawanyiko ndani ya Chama hicho.
Mwenyekiti
wa Chama cha Mapinduzi wilaya ya Rorya Bw Samweli Kiboye ametoa kauli hiyo
katika baraza la vijana wa Chama hicho lililofanyika katika wilaya ya Rorya
mkoani Mara.
Amesema
kumekuwepo na baadhi ya watu ambao wanaleta Malumbano na mgawanyiko ndani ya Chama
na hivyo kusababisha Chama kutofanya shughuli zake kama kawaida na hivyo akiwakumbusha
kama mambo yataachwa Chama cha Mapinduzi kitafanya vizuri katika Chaguzi zinazokuja
"Hatutamvumilia mtu yoyote ndani ya Chama kuendelea kuleta Malumbano na mgawanyiko ndani ya Chama kuruhusu mambo hayo ni kukiua Chama nitapambana nao sasa"alisema Mwenyekiti huyo
Bw Bw Samweli Kiboye - Mwenyekiti
wa CCM Rorya
Katika
hatua nyingine Mwenyekiti huyo amewata vijana hao ambao ni viongozi wa mabaraza
ya Vijana katika Kata wilayani humo, kufanya ziara katika kata zao huku
akiwapongeza Viongozi wa juu wa Chama cha Mapinduzi na kusema kuwa Chama hicho
hakitakubali kuona baadhi ya viongozi wa Chama hicho wanaounga kutukana viongozi wao.
"Tunawapongeza sana Viongozi wetu wa juu ndani ya Chama kwasasa wamerudisha uhai wa Chama,tunampongezasana Rais wetu anafanya kazi nzuri na kama tutaacha Malumbano uchaguzi unaokuja kwetu hakuna shida" aliongeza Mwenyekiti huyo
Baadhi ya wajumbe wa baraza la Vijana UVCCM Rorya
No comments:
Post a Comment