Friday, May 24, 2013

KIEMBA AKUBALI KUSAINI MSIMBAZI, KASEJA MAZUNGUMZO YAENDELEA, KAPOMBE BADO ANA MKATABA!!

DSC_3196

Na Baraka Mpenja wa Fullshangwe Dar es salaam

Kiungo matata wa wekundu wa Msimbazi Simba, Amri Athman Kiemba amekubali kuongeza mkataba wa kuichezea klabu hiyo kwa msimu ujao wa ligi kuu soka Tanzania bara.

Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Keptein Zacharia Hans Poppe ameimabia FULLSHANGWE kuwa Amri Kiemba wameshazungumza nae na kukubaliana kuongeza mkataba wake jambo ambalo limewapa raha sana kutokana na ubora wa mchezaji huyo aliyekuwa akitajwa kuihama Simba na kujiunga na Yanga msimu ujao.

“Kuhusu Kiemba tumeshaziba midomo ya watu, amekubali kwa moyo mkunjufu kuitumikia klabu yake msimu ujao, ni bonge la mchezaji, tunafurahi kuwa nae katika kikosi chetu”. Alisema Poppe.

Kuhusu nahodha Juma Kaseja, Poppe alisema wanaendelea kuzungumza nae ili kumsainisha mkataba mwingine huku wakikubaliana kuboresha maslahi yake klabuni hapo.

“Kuna watu wanazungumza na Kaseja, nadhani wanaendelea vizuri na mimi nitakutana nae tumalizane, haondoki ng`oo, atakuwepo Simba, cha msingi mashabiki wa Simba wawe watulivu”. Alisema Poppe.

Kuhus suala la Shomary Kapombe, Poppe amewatoa mashabiki wa kuwa mchezaji huyo bado ana mkataba na Simba hadi aprili mwakani na ataendelea kubaki msimbazi.

“Wanamsimbazi wasiwe na wasiwasi, Kapombe ni wetu na kila kitu kipo sawa”. Alisema Poppe.

Poppe alisema baada ya vijana hao kurudi kutoka Morocco wanapokwenda kuitumikia timu ya taifa, watasaini mikataba minono zaidi.

Kwa upande mwingine, Hans Poppe alisema zoezi la kuwasainisha mikataba mipya wachezaji wote wa timu hiyo linaendelea vizuri, ikiwemo wale waliopandishwa kutoka kikosi cha pili, yaani Simba B.

Poppe aliongeza kuwa  mwaka huu wanahitaji kufanya mambo yao kimya kimya ili kuwazuia wale wasiojua kusaka wachezaji ila wakijua Simba wamempa nani wanakimbilia kuwasainisha.

“Tunataka kuongeza wachezaji wengine wapya ili kuongeza nguvu ya kikosi, safari hii tunafanya kimyakimya kuwazuia ndugu zetu wasiojua kutafuta wachezaji na kufanya hesabu

No comments:

Post a Comment