MUSOMA
AFISA Uhamiaji Mkoa wa Mara Bw Jacob Sambai anadaiwa kumtishia kwa
Kumchoma Kisu Mfanyakazi mmoja wa Idara Hiyo Moses Malekela kwa
kile kinachodaiwa bosi huyo kuwa na mahusiano ya kimapenzi na
binti ambaye pia ni mfanyakazi wake.(jina tunalo)
Taarifa zinasema kuwa Vitisho hivyo vilitokea Agost
24 Mwaka huu majira ya saa nane mchana baada ya bosi huyo kupokea malalamiko
kutoka kwa afisa mmoja ndani ya ofisi hiyo Sackibu Kabyemela aliyekuwa
akituhumiwa na binti huyo kuwa anatoa taarifa za kuwa na Mahusiano ya Kimapenzi
na bosi huyo
Kufuatia kuwepo kwa Taarifa hizo katika ofisi hiyo
ndipo bosi huyo alipoitisha kikao cha dharura kwa kuwahusisha msaidizi wake DCI
Milinga, maafisa waliohusika na tuhuma hizo pamoja na maafisa wengine kama
mashaidi.
Katika kikao hicho Maafisa hao kila mmoja alijieleza
kwa muda wake huku wakisisitiza kuwa hizo ni taarifa ambazo ziko ofisini na
kila mtumishi wa ofisi hiyo anajua kuwa bosi anatembea mmoja wa Mfanyakazi
katika Idara hiyo
Bosi mimi na mwenzangu tunaotuhumiwa kusambaza uvumi
huo hatukuwepo ofisini kwa muda mrefu,tulikuwa masomoni tuliporipoti na sisi
tukayakuta hayo maneno. Fanya uchunguzi” Alisikika mtumishi mmoja akisema.
Aidha katika hatua Nyingine Ikafika wakati wa mtumishi wa mwisho Moses Malekela
kujieleza ambapo nae akasema, “Bosi, haya ni maneno tu, fanya uchunguzi wa kina
utapata ukweli wake”.
Baada ya Kusikiliza watumishi wote waliokuwepo
katika kikao hicho ndipo Bosi huyo akapandisha jazba na kuvuta droo yake na
kuchomoa kisu kikali na bisibisi na kutaka kumchoma afisa huyo,ndipo alipozuiwa
na msaidizi wake akishirikiana na maafisa wengine waliokuwepo kwenye kikao na
kuamua kuweka kisu chini na kuvua saa yake ya mkononi tayari kwa kumpiga ngumi
afisa huyo huku akisema,” Leo kazi na iishe”
Tafrani hiyo ilichukua takribani dakika kumi ambapo bosi
huyo akitaka kuonyesha umwamba wake lakini busara za msaidizi wake na maafisa
waliokuwepo walifanya kazi ya ziada kumzuia bosi huyo na baada ya kuona
amezidiwa nguvu ndo akamtolea kauli ya vitisho huku akisema “Haina shida,
ntakutafuta mtaani”
Kauli hiyo ilimtisha mtumishi huyo Moses Malekela na kuamua kutoa taarifa kituo
kikuu cha Polisi Musoma kwa RB NO MUS/RB/5872/2012 na vyombo vingine vya ulinzi
na usalama ngazi ya mkoa ili kulinda usalama wa maisha yake.
Akiongea kwa njia ya Simu na Mwandishi wa habari hii
Kamanda wa jeshi la Polisi mkoa wa Mara Kamishina Msaidizi Mwandizi wa Jeshi
hilo Abslom Mwakyoma alisema kuwa tayari suala hilo limefika katika hilo na
linafanyiwa uchunguzi wa kina kabla ya hatua zaidi za kisheria kuchukuliwa
“ Ni kweli
Suala hilo lipo tayari Katika Jeshi letu na tunaendelea kulifanyia uchunguzi wa
kina kabla ya hatua zaidi za kisheria hazijachukuliwa” alisema Kamanda huyo
Naye Afisa Uhamiaji huyo alipoulizwa kwa njia ya
Simu kuhusu Sakata hilo alisema kuwa tayari limefikishwa kwenye Vyombo vya
sheria hivyo ni vyema suala hilo likafanyiwa kwanza Uchunguzi na baadaye tutapata
ukweli.
‘Hayo
unayosema yapo na tayari yapo Polisi hivyo nadhani ni vyema kwanza tukasubiri
tuone baada ya Uchunguzi wa jeshi hilo ndipo ukweli utabainika” alisema Afisa
Uhamiaji huyo
Wakati huo huo kuna taarifa rasmi kuwa bosi huyo
amekuwa na Tabia ya kuwatongoza maafisa wake wa kike na pale wanapomkatalia
huwachukulia hatua kwa kuwahamisha vitengo ama kuwatenganisha wanandoa hao kwa
kuwahamishia vituo vya mbali.
Tuhuma nyingine zinazomkabili bosi huyo, ni pamoja
na kukarabati jengo la ofisi kwa gharama zisizoendana na ukarabati huo, Kufanya
manunuzi ya thamani za ofisi bila kufuata taratibu za manunuzi ya umma.
Mbali na hivyo pia inadaiwa Kuendesha gari STK 2559 yeye mwenyewe bila kibali cha
katibu mkuu wa wizara ya mambo ya ndani na kuliangusha katika maeneo ya Kiabakari
bila ya kuwa na dereva wa serikali na kuitengeneza gari hiyo kwa gharama za
kodi za walalahoi wa bila kufuata taratibu.
Taarifa zaidi
zinasema kuwa baada ya kuitengeneza kinyemela gari hilo,Bosi huyo aliandika
barua TEMESA kwa ajiri ya ukaguzi wa gari hilo na TEMESA wakajibu kukataa
kuikagua kwa barua kumbukumbu NO MUS/STK 2559/249/34 kwa maelezo kuwa
haikufuata taratibu za magari ya serikali yanapopata ajali
“Hayo kwangu
siyo Malalamiko mapya ndugu yangu maana yamekuwepo muda mrefu ila wewe kama
unataka kuuza gazeti kwa habari hiyo wewe andika.Alisema Afisa huyo
Taarifa zaidi zinasema kuwa Malalamiko hayo yote
yalisha tumwa uhamiaji makao makuu na ikawa kimya, na mengine yakatumwa kwa
katibu mkuu ambae alituma tume ya mtu mmoja na kufanikiwa kuwahoji watumishi ambapo mpaka sasa bado hatima yake haijajulikana
No comments:
Post a Comment