Thursday, February 9, 2012

HABARI KUTOKA MUSOMA


musoma

Ikiwa ni siku moja baada ya kituo hiki kutangaza hali ya soko la kamnyonge lililopo manispaa ya musoma mkoani mara na wafanyabishara wa soko hilo kutaka kumuona mkuu wa mkoa wa mara, halmshauri ya manispaa ya musoma mkoani mara imeanza mikakati ya kuboresha soko hilo.

akiongea na kituo huki afisa afanya manispaa ya musoma mkoani mara bw peter mtaki amesema kuwa halmashauri hiyo imesikia malalamiko ya wafanyabiahara hao na yatari hatua za awali kuweka bomba la maji eneo hilo zinaendelea.

amesema kufikia leo jioni maji yataanza kutoka katika soko hilo  huku hatua za kuweka umeme zikiendelea  ambapo tayari shirika la umeme tanesco mkoani mara limeishaweka mita ingawa bado hawajaunganisha umeme huo uanze kuwaka.

aidha bw mtaki amewataka wafanyabiashara katika soko hilo kujenga vibanda vyao katika hali ya ubora na kuwataka wafanyie biashara zao katika soko hilo.

amesema manispaa imetenga eneo la kuweka takataka katika pipa ambazo zitakuwa zikizolewa kila asubuhi huku akiwahadi wananchi wa manispaa ya musoma huduma muhimu kupatikana katika soko hilo na watakao kwenda kinyume kuchukuliwa hatua kali za kisheria.

wakiongea baada ya kuboreshewa miundombinu hiyo wafanyabiashara katika soko hilo wamesema kuwa wamefarijika na hali hiyo ingawa wamewataka viongozi hao kukamilisha soko hilo ili liwe na kiwango kinachostahili.

,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,


serengeti

mtu mmoja anayesadikiwa kuwa na umri kati ya miaka 30 na 35 asie fahamika jina na mahali anapo ishi amekutwa kichakani akiwa amefariki katika kijiji cha kenyamonta wilaya ya serengeti mkoani mara

akithibitisha kutokea kwa tukio hilokaimu kamanda msaidizi wa polisi mkoani mara acp robert boaz amesema mtu huyo mwanaume amekutwa kichakani akiwa amekufa huku baadhi ya sehemu katika mwili wake zikiwa zimeliwa na wanyama

akizungumzia tukio hilo kamanda amesema hadi sasa chanzo cha kifo hicho hakijafamika na kuwa jesgi la polisi bado linaendelea na uchunguzi ili kupata uhakika wa kifo hicho ambapo amewataka wananchi waliopotelewa na ndugu yao kutoa taarifa katika katika sehemu zinazohusika

amesema mtu huyo alikutwa amevaa tshirt nyeupe yenye ufito mwekundu na suruali ya kitambaa rangi ya udongo

kamanda amesema kuwa inawezekana mtu huyo alikufa siku mbili kabla ya kukutwa kichakani  na polisi ukiwaumeharibika vibaya na polisi walichukua jukumu la kuuzika mwili huo wilayani serengeti 

amewaasa wananchi kuwa ni vizuri kutembea na vitambulisho ambavyo vinavyoweza kukutambulisha vizuri na pia ni vema kutoa taarifa kwa ndugu zako ni wapi unaelekea ili kuondoa usumbufu kwa ndugu na polisi pia
,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,

musoma

mtoto wa kike mwenye umri wa mwaka mmoja na nusu ameokotwa leo majira ya saa kumi na mbili asubuhi akiwa ametupwa kwenye choo cha bandari maeneo ya iringo mjini musoma

akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kaimu msaidizi wa polisi mkoa wa mara acp robert boaz amesema mtoto huyo ameokotwa akiwa hai na mama wa mtoto huyo bado hajapatikana

aidha kamanda amesema ikiwa kuna taarifa zozote juu ya mama aliyekuwa na mtoto lakini sasa mtoto haonekani basi atoe taarifa polisi ili hatua za kisheria zichukuliwe

pamoja na hayo amesema kwa sasa mtoto huyo yupo katika hospital ya mkoa wa mara na afya yake ni nzuri na pia yuko chini ya serikali na atalelewa na kituo cha kulelea watoto wanaoishi katika mazingira magumu na atapewa mahitaji yote muhimu chini ya dawati la kijinsia huku upelelezi ukiwa unaendelea kumsaka mama wa mtoto huyo

aidha kamanda amewaasa wananchi kuwa ni vizuri kuamua kupata watoto wakiwa tayari kwani kuzaa kuna wajibu wa kutunza mtoto  na pia wazazi wanapogombana watafute njia sahihi za kisheria ili kumaliza matatizo yao  ambyo yanapelekea kupata watoto wa mitaani

,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,

mwanza

mbunge wa nyanghwale hussein nassoro amesema jumla ya wanafunzi 469 waliochaguliwa kujiunga na masomo ya sekondari kutoka kata nne za jimbo hilo wilayani geita mkoani mwanza  hawajaripoti shuleni kwa ajili ya kuanza masomo yao 

amesema hayo wakati wa ziara yake jimboni humo na ametoa muda wasiku tano kukamatwa kwa wazazi  hao iwapo watakuwa hawajawapeleka watoto wao shuleni

mbunge huyo amesema ni vemawazazi hao wakawapeleka shuleni watoto wao ili waendelee na masomo yao kama inavyotakiwa na pia ameahidi kuwalipia ada wanafunzi 25 wanaotoka katika mazingira magumu kwa kila kata

taarifa za watoto hao kutoripoti shuleni zimetokana na malalamiko yaliyotolewa na wadau mbalimbali wa elimu akiwamo ofisa tarafa ya nyangwale susan kisena ambapo amesema takwimu hizo ni za kata 12 na pia inawezekana kuna idadi kubwa ya wanafunzi ambao hawajaenda shule

,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,

No comments:

Post a Comment