Baadhi ya wakulima hao wakifanya Mahojiano na AZAM TV
Afisa kilimo kata ya Nyakatende Bw Magesa akisema zao hilo ni mbadala wa Pamba
Kusuasua kwa kilimo cha Pamba na kushambuliwa na Magonjwa kwa zao la Muhogo katika Halmashauri ya Musoma vijijini wilaya ya Musoma mkoani Mara mazao ambayo yalikuwa ya chakula na Biashara kumesababisha viongozi katika halmashauri hiyo kuanzisha kilimo cha Alzeti,Zao ambalo linaelezwa linaweza kuwa mbadala wa Mazao hayo.
Kwa muda mrefu sasa wananchi wa halmashauri ya Musoma vijijini wilaya ya Musoma mkoani Mara wamekuwa wakihangaika katika kilimo cha Pamba kama zao la Biashara na Muhogo kama zao la Chakula lakini mabadiliko ya Tabia nchi na Magonjwa ya Michilizi kahawia na Batoto kwa zao la Muhogo yamekuwa kikwazo kikubwa.
Kufuatia hatua hiyo wananchi hao wamehimizwa kuanzisha kilimo za Alzeti kilimo ambacho kinaelezwa kinaweza kuwa mbadala wa Mazao hayo endapo wananchi hao watafuata kanuni za kilimo.
Hata hivyo licha ya wananchi hao kujikita katika kilimo cha Alzeti bado wanaiomba serikali kuwa karibu katika kuhakikisha kilimo hicho kinakuwa na Tija.
Afisa kilimo katika kata ya Nyakatende Halmashauri ya Musoma vijijin MAREGESI EPHRAIM akaomba Mbunge wa jimbo hilo na viongozi wa halmashauri hiyo kuhakikisha vinapatikana viwanda vidogo vitakavyosaidia wananchi hao baada ya kuvuna Alzeti hiyo.
Mbunge wa Jimbo la Musoma vijiji Mbunge wa jimbo hilo Prof Sopeter Muhongo ambaye pia ni waziri wa Nishati na Madini amesema Alzeti ni zao pekee ambalo litakuwa msaada mkubwa kwa wananchi wa jimbo hilo kufuatia kushuka kwa soko la Pamba na zao la Muhogo kushambuliwa na Magonjwa mbalimbali.