Thursday, September 13, 2012

WAIPONGEZA HALMASHAURI KUWAPATIA TRECTA.

Dinna Maningo,Tarime.

KIKUNDI  cha Tembo Mazingira kinachojishughulisha na kilimo cha mazao ya chakula na biashara pamoja na uoteshaji wa miche  kilichopo kijiji cha Nyabitocho kata ya Mbogi Wilayani Tarime Mkoani Mara kimesema kuwa kinategemea kupata mazao mengi baada ya  Halmashauri ya Wilaya ya Tarime kukipatia trecta yenye  thamani ya milion 44,207,000 kwa ajili ya shughuli za kilimo.

Wameyasema  hayo wakati wakikabidhiwa trecta na Mkuu wa Wilaya ya Tarime John Henjewele  ambaye alikuwa  mgeni rasmi ,wanakikundi hao wamesema kuwa trecta hiyo itarahisisha shughuli zao za kilimo kwani  itatumika kubeba mazao, mbolea na kulima ambapo   kwa muda mlefu wamekuwa wakilima  kwa kutumia majembe ya mkono (plau).

Afisa kilimo wa Wilaya ya Tarime  Selvanus Gwiboha amesema kuwa kikundi cha Tembo kiliibua mradi wa trecta ambao uliingizwa kwenye bajeti mwaka 2010/2011 ambapo jumla ya 55,000,000 ilitengwa kwa shughuli  hiyo na kwa robo ya nne ya mwaka  wa fedha  2011/12 trecta hilo limenunuliwa kwa thamani  ya milioni 44,207,000 ikiwa na tela, jembe la kulimia na  la harrow na kikundi kiliweza kuchangia  asilimia 20% milioni 11,000,000 na kuweza kupata trecta kupitia mradi wa DADP.

Mkuu wa Wilaya John Henjewele aliyekuwa mgeni rasmi kwa kuwakabidhi trecta amewataka wanakikundi kuonyesha nidhamu umoja na mshikamano katika shughuli mbalimbali za kikundi  ili wapate mapato mengi katika shughuli zao za kilimo.


           WANANCHI MTAA WA STAREHE KUKUMBWA NA MAFURIKO.

Dinna Maningo,Tarime.

WANANCHI wa Mtaa wa starehe mjini Tarime wameiomba Serikali kufukia korongo la starehe ambalo limekuwa kero kwao kwa muda mrefu nakwamba  endapo  lisipofukiwa huwenda kukatokea maafa makubwa hasa  kwa kipindi hiki cha mvua  ya erinino.

Wakiongea na VFM wamesema kuwa  kutokana na  kuwepo kwa mvua kubwa zinazoendelea  kunyesha hivi sasa kuna hatari nyumba zilizopo kando kando mwa korongo zikabomoka baada ya  korongo hilo kujaa maji.

Mwenyekiti wa Mtaa  wa starehe Genkuru Tagaya (CCM) amesema kuwa  kwa muda mrefu tangu mwaka 2005 korongo hilo limekuwa likipigiwa kelele na  viongozi wa mtaa  lakini hakuna hatua zozote za Seikali  zilizochukuliwa  ili kuwanusuru  wananchi waishio pembezoni mwa korongo.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime Fidelis Lumato amesema kuwa  korongo hilo ni kubwa sana na linahitaji kiasi kikubwa cha pesa  ili kuboresha  na hivyo Halmashauri haina pesa  kwa sasa kwakuwa  korongo hilo halikutengewa bajeti yake na hivyo kuwataka kuwa na subira katika kipindi kingine cha bajeti.

No comments:

Post a Comment