Shirika la Viwango nchini TBS limewataka Wajasiriamali nchini kuhakikishia bidhaa zao zinakuwa na
ubora unaostahili ili kupata soko la uhakika ndani na nje ya nchi.
Afisa uhusiano wa Shirika hilo Bi Roida Andusamile alisema
Wajasiriamali wengi nchini wamekuwa wakikosa Soko la uhakika la ndani na nje
kutokana na bidhaa zao kutokuwa ubora kuanzia wanapozalishia bidhaa hizo.
"Ili kupata alama ya ubora kuna vitu vya kuangalia ikiwemo hata eneo la kuzalishia bidhaa huska hivyo basi ni changamoto kwa wajasiriamali kuhakikisha wanazalisha bidhaa zao katika hali ya ubora"alisema Andusamile
Amesema ili kupata
alama ya ubora wajasiriamali hao utambulisho na shirika la viwanda vidogo Sido na
kusema kuwa katika shirika hilo la viwango hakuna urasimu kama inavyodhaniwa na
kuongeza kuwa liko mbele katika kutoa elimu
kwa Wajasiriamali hao.
Baadhi ya wajasiriamali ambao wanashiriki katika Maonyesho
hayo ya Kanda ya Ziwa ya Viwanda vidogo yaliyoandaliwa na shirika linaloratibu
viwanda hivyo Sido kwa Mwaka 2013 waliothibitishwa na TBS walieleza faida
walizopata baada ya kuthibitishwa.
" Kwa kweli tbs imetusaidia sana maana kwa sasa bidhaa zetu tunauza hata nje ya nchi na pia kwenye Supermarket mbalimba hapa nchini"
Kufua hatua hiyo Wajasiriammali hao waliwataka wenzao kuhakikisha wanapata alama ya tbs kwani itasaia kuinua kipato chao lakini pia kuboresha bidhaa zao
Maonyesho ya Kanda ya Ziwa ya Viwanda vidogo Sido yaliyoanza
Novemba 27 mwaka huu yataitimishwa Desemba 2 katika
No comments:
Post a Comment