Tuesday, December 3, 2013

"Uhalibifu wa Mazingira bado ni tatizo kubwa katika Jamii"

RORYA
 
Serikali na wadau mbalimbali wa Mazingira nchini  wametakiwa kuchukua hatua za haraka katika kukabiliana na uharibifu wa  Mazingira ambao umekuwa ukiendelea  kutokea katika Jamii na kusababisha athari mbalimbali likiwemo tatizo la njaa.

Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa wilaya ya Rorya Bw Elias Goloyi katika hotuba yake iliyosomwa na Katibu tawala wilaya hiyo Bw Murumbe Daud katikaMaadhimisho ya siku ya elimu endelevu kwaajili ya uhifadhi Mazingira yaliyofanyika katika wilaya ya Rorya Mkoani Mara.

Amesema Mabadiliko ya tabia nchi husababisha athari mbalimbali katika jamii huku Mratibu wa Mradi huo katika bonde la ziwa Victoria kutoka shirika la WWF mkaoni Mara Bw Kelvin Robert amesema kama hali hiyo haitadhibitiwa jamii itakuwa katika hali mbaya likiwemo tatizo la njaa.

  "Kama hali hii itaendelea pasipo Serikali kuchukua hatua za haraka kukabiliana na tatizo hili la uhalibifu wa Mazingira hali itakuwa ngumu sana,maana njaa kila siku  itakuwepo na hata Mvua haitanyesha" alisema Mratibu huyo

Katika hatua nyingine baadhi ya wakazi wa wilaya Rorya wamesema shughuli mbalimbali za kibinadamu zimesababisha uharibifu mkubwa wa Mazingira wilayani humo.

  "Wananchi bado wanapaswa kupewa elimu ya Mazingira kwasababu sehemu kubwa ya uhalibifu wa Mazingira unasababishwa na Binadamu" alisema Mwalimu Mstaafu Benadina Nyambiti

Shirika la WWF limekuwa likitekeleza mpango wa elimu endelevu katika uhifadhi wa Mazingira katika wilaya za Butiama,Bunda,Rorya,Musoma na Tarime Mkoani Mara na katika wilaya za Ilemela na Nyamagana jijini Mwanza na katika nchi za Afrika Mashariki ni pamoja na Tanzania,Kenya,Uganda na Rwanda.

Picha mbalimbali katika Maadhimisho hayo 

Mratibu wa Mradi huo katika bonde la ziwa Victoria kutoka shirika la WWF mkaoni Mara Bw Kelvin Robert

 Baadhi ya Wakazi wa wilaya ya Rorya wakiwa katika Maadhimisho hayo

 Baadhi ya Wakazi wa wilaya ya Rorya wakiwa katika Maadhimisho hayo

 Baadhi ya wadau wa Mazingira wakifuatilia Maadhimisho hayo

 Waandishi wa habari nao hawakuwa nyuma katika kufuatilia Maadhimisho hayo
 Mwl Benadina Nyambita Mdau wa Mazingira Rorya
Katibu tawala wilaya ya Rorya Bw Murumbe Daud akisoma hotuba ya Mkuu wa wilaya hiyo Bw Elias Goloyi

No comments:

Post a Comment