Mahakama ya wilaya ya Musoma mkoani Mara
imemuhukumu Bw Liso Chacha kifungo cha miaka mitatu jela baada ya kupatikana na hatia
ya kujitambulisha katika idara mbalimbali zikiwemo za Serikali kama Afisa Mwandamizi wa idara ya Usalama wa Taifa.
Licha ya Kujitambulisha katika idara hizo kama Afisa Mwandamizi idara ya Usalama wa Taifa Makao
Makuu,Mtu huyo alidanganya Viongozi Wakuu wa Mkoa wa Mara na kujipatia huduma
mbalimbali huku akisema ameagizwa na Makao Makuu kufanya kazi Maalum mkoani hapa.
Katika hukumu hiyo Mwendesha
Mashitaka wa Polisi Sajent Stephano Mgaya alisema kuwa June 14 Mwaka huu,Mtuhumiwa
huyo alimpigia Simu Mkuu wa Mkoa wa Mara Bw John Gabriel Tuppa na
kujitambulisha Kama Afisa usalama kutoka Makao Makuu na hivyo ameagizwa Mkoani
Mara kufuatilia Mtandao wa kuuza Risasi kutoka katika kikosi cha Jeshi 27 KJ
Makoko na hivyo kuhitaji msaada kutoka mkoani.
Baada ya Kauli ya mtu huyo,
Mkuu wa Mkoa wa Mara aliwasiliana na Mkuu wa Kikosi cha Jeshi Makoko kwa lengo la kufanikisha Kazi hiyo na kutoa
huduma mbalimbali kwa mtu huyo zikiwemo Malazi katika Nyumba ya Maafisa wa
Jeshi katika eneo la Tembo Beach ambapo
pia Maafisa wa Jeshi la Wananchi ambapo pia waliwasiliana na Mkuu wa Upepelezi
wa Makosa ya Jinai RCO kwaajili ya kutekeleza agizo hilo.
Bw Liso Chacha (AFISA USALAMA FEKI)
Katika kutekeleza Agizo hilo vyombo hivyo vya usalama viliteua baadhi
ya Maafisa na kuambatana na mtu huyo hadi katika Kizuizi cha Polisi kilichopo
Kirumi ili kuweka Mtego na kukamata Magari aliyodai kuwa na risasi kazi ilifanyika
kwa Siku mbili bila Mafanikio.
June 17 Mwaka huu Mtu huyo alifika kwa Waandishi wa habari Mkoani hapa akijitambulisha
kama Afisa Usalama na kutaka msaada wa
wanahabari hao kushirikiana nae katika kufanikisha Kukamata Magari hayo ambapo walimtilia shaka na kutoa taarifa
Polisi.
Akitoa hukumu Hakimu Mkazi Mfawidhi wa
Mahakama ya wilaya ya Musoma Bw Richard Maganga,amesema Mahakama imeridhishwa
na Maelezo ya Mashitaka wakiwemo mashahidi saba kutoka idara mbalimbali ambazo
ni Jeshi la Polisi,Mkuu wa utumishi
idara ya usalama wa Taifa ,Waandishi wa habari na Jeshi la Wananchi wa Tanzania
na hivyo kumtia hatiani mtuhumiwa huyo kwa kujifanya Mtumishi wa idara ya
Usalama wa Taifa na hivyo kwenda jela Miaka mitatu
No comments:
Post a Comment