JOSEPH WAMBURA NDUGU WA MAREHEMU NA MAJERUHI AKIWA AMELAZWA WODI LA WANAUME BAADA YA KUPOTEZA FAHAMU MUDA MFUPI TU BAADA YA KUFIKA ENEO LA TUKIO NA KUSHUHUDIA VIFO. |
Julai 14,2013.
Serengeti:WATU wawili wakazi wa
kitongoji cha Kanisani kijiji cha Matare Mamlaka ya mji wa Mugumu wilayani
Serengeti wa familia moja wamekufa na
mmoja kujeruhiwa baada ya kuangukiwa na kifusi wakati wakichimba kokoto.
Tukio hilo limethibitishwa na
polisi,uongozi wa kitongoji na Hospitali teule ya Nyerere ddh limetokea julai
14 majira ya saa 4:10 asubuhi mwaka huu katika eneo la machimbo ya kokoto,wakati
wakiwa wanachimba.
Mwenyekiti wa kitongoji hicho
Juma Mahando amewataja waliofariki kuwa ni Rhobi Mwita Nyantori(45)ambaye
alifia eneo la tukio,Nyahiri Chacha Mwita(41)ambaye amefariki baada ya kupata
huduma na majeruhi ni Wegesa Mwita(39)ambaye amelazwa.
Akisimulia mkasa huo kwa
kugugumia Wegesa ambaye ni majeruhi alisema wenzake walikuwa ndani ya shimo nay
eye akiwa pembeni akisubiri mzigo wa kokoto aweze kutoa nje ghafla walianguliwa
na kifusi chote na kuwafunika.
“Udongo wote umenifunika..kilichosaidia
pembeni kulibaki kama uwazi,lakini waliokuwa ndani humo umewapiga wakiwa
wameinama na kuanguka…watu waliokuwa nje waliona na kupiga kelele wakajitokeza
watu wakatupa msaada…nahisi maumivu makali kiunoni na mbavu”alisema kwa
kugugumia.
Mganga wa zamu dk,Amosi Kittoh
amesema kilichopelekea kifo cha Rhobi ni kuumia kifuani na Nyahiri alipata
madhara makubwa kwenye uti wa mgongo .
Dk ,Kittoh amesema kuwa tukio
hilo limesababisha ndugu wa marehemu hao Joseph Wambura kupoteza fahamu na
wamemlaza wodi ya wanaume kwa ajili ya matibabu.
Akizungumzia machimbo hayo
Mwenyekiti wa kitongoji hicho Mahando alisema novemba 2009 watu wawili wa
familia moja waliangukiwa na kufariki,ikiwa ni mwendelezo wa matukio ya vifo na
serikali ikayafunga.
Hata hivyo alisema watu walikuwa
wakienda kuchimba kama wizi kujipatia riziki,hata hivyo baadhi ya wananchi
walisema serikali inafahamu kuwa machimbo hayo yanaendelea kwa kuwa kokoto
huuzwa hadharani,huku hata viongozi wa wilaya wakiwa ni wateja wao na ndiyo
maana yameendelea kwa kipindi chote bila kuwakamata wahusika.
Mwisho.
BAADHI YA NDUGU WAKILIA BAADA YA KUTAARIFIWA KUFARIKI KWA NYAHIRI CHACHA MWITA(41)
source Mayunga Blog
No comments:
Post a Comment