Baadhi ya wananchi
wa Vijiji zaidi ya 10 vinavyopitiwa na barabara ya
Balili Manchimweru wilaya ya Bunda mkoani Mara wameipongeza Serikali kwa
kuipandisha hadhi barabara hiyo kuwa chini ya TANROAD na pia kuitengeneza kwa
kiwango cha Changalawe.
Sauti za
wananchi hao zimesikika mbele ya waandishi wa habari wakati wa Matengenezo ya
barabara hiyo yenye urefu wa km 41 kupitia Kampuni ya ukandarasi ya Keres
Tanzania LTD.
Wamesema
kabla ya ujenzi huo barabara hiyo ilikuwa kero hasa nyakati za Mvua lakini
kukamilika kwa barabara hiyo
kutarahisisha mambo mengi katika maisha yao ya kila siku
Kwa upande
wake Fundi Mchundo wa barabara hiyo Bw Charles
Joseph amesema mradi huo wenye thamani
ya zaidi ya shilling Milion 300 ulitakiwa kukamilika ndani ya miezi sita lakini
kutokana na Mvua zilizokuwa zikinyesha ulichelewa kukamilika na hivyo
kukamilika mwishoni mwa mwezi julai.
Kutengenezwa
kwa barabara hiyo kunafuatia malalamiko ya Mara kwa Mara ya Wananchi hao hasa
nyakati za Mvua na hivyo kutengezwa kwa kiwango cha Changalawe ni faraja kwa
wakazi wa Vijiji hivyo
No comments:
Post a Comment