Mkuu
wa Mkoa wa Tanga, Chiku Galawa (kushoto) akipokewa na Mkuu wa Kitengo
cha Huduma za Fedha zinazofuata Kanuni za Kiislamu ‘NBC Islamic
Banking’ cha Benki ya Taifa ya Biashara, Yassir Masoud alipokwenda
kufungua semina ya siku moja kwa wanawake wajasiriamali waislamu
iliyoandaliwa na NBC mjini Tanga leo. Katikati ni Meneja Tawi la NBC
Tanga Deusdedit Mashalla. Baadhi
wa washiriki wa semina ya siku moja iliyoandaliwa na Benki ya NBC
Kitengo cha Islamic Banking wakiwa katika semina hiyo jijini Tanga leo.
Na Mwandishi Wetu
Benki
ya Taifa ya Biashara (NBC) kupitia kitengo chake cha Huduma za Kibenki
zinazofuata kanuni za kifedha za Kiislamu inatarajia kuanzisha huduma ya
mikopo kwa wafanyakazi ‘Islamic Group Finance’ kabla ya Septemba mwaka
huu.
Akizungumza
wakati wa semina ya siku moja ya wanawake wajasiriamali wa Kiislamu
jijini Tanga jana, Mkuu wa Islamic Banking wa NBC, Yassir Masoud alisema
lengo la kuanzishwa kwa huduma hiyo ni kutoa fursa za mikopo kwa wateja
wao wanaohudumiwa kwa kufuata kanuni za dini hiyo.
Masoud
aliwaambia wanawake waliohudhuria semina hiyo kwamba ili waweze
kujikwamua kiuchumi, wanahitaji kujifunza mbinu za biashara, akisisitiza
kwamba hata mafundisho ya Kiisllamu yanatoa maelekezo kuhusu utafutaji
wa riziki.
”Uislam
umehimiza mambo ya uwekezaji, Uislamu unahimiza masuala ya mali
maandiko yakisema kwamba kutafuta riziki ni sawa na kutafuta fadhila za
Mwenyezi Mungu,” alisema.
Akifungua
semina hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Tanga bibi Chiku Galawa aliwahimiza
wanawake mkoani humo kujizatiti kwenye ujasiriamali ili kusaidia juhudi
za serikali katika kuinua maendeleo yasiyoridhisha ya mkoa huo.
Alisema
kuwa kwa kupitia semina hiyo, NBC imefungua njia mpya yenye matumaini
kwa wanawake wa Tanga, njia ambayo mashirika mengine yanapaswa kuifuata.
“NBC
ni moja kati ya benki kongwe yenye mtanda mpana kuliko zote nchini na
imekuwa mstari wa mbele ikishirikiana na watu mbalimbali katika
kuboresha maisha ya Watanzania,” alisema.
Katika
siku za hivi karibuni, NBC imekuwa ikiwekeza zaidi katika kuelimisha
jamii, hususan wajasiriamali kupitia semina na warsha mbalimbali huku
ikishirikiana na makampuni mengine.
Mwishoni
mwa mwaka jana, benki hiyo iliandaa mkutano wa wajasiriamali wadogo
wadogo wa jijini Dar es Salaam kwa ushirikiano na shirika lisio la
kiserikali linalojishughulisha na vijana, YESi.
NBC
pia ni wadhamini wa Top 100 Midsize Companies Survey ambayo inaendeshwa
kwa ushirikiano na KPMG kuyasaka na kuyazawadia makampuni ya kati
yanayokuwa kwa kasi.
“Sekta
ya Biashara ndogo ndogo na za kati ni muhimu katika kukuza uchumi
nchini, na ni sekta inayoweza kutoa nafasi za ajira kwa wananchi wengi.
NBC wametambua hilo,” alisema.
Aliishukuru
benki hiyo na kuishauri iendelee kutoa mafunzo kwa wahusika wa sekta
hiyo na kuwawezesha wajasiriamali kukuza biashara zao na hatimaye kuinua
uchumi wa nchi.
Rais Kikwete amwapisha Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria na Mabalozi Wapya wanne
Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete,Makamu wa Rais Dkt.Mohamed Gharib Bilal na
Waziri wa Mambo ya Nje Bernard Membe wakiwa katika picha ya pamoja na
mabalozi wapya waliopaishwa leo ikulu jijini Dar es Salaam.aliyesimama
mbele kushoto no Balozi Liberata Mulamula anayekuwa Balozi Mpya wa
Tanzania nchini Marekani.Waliosimama nyuma kutoka kushoto ni Balozi mpya
wa Tanzania Uholanzi Wilson Masilingi,Balozi mpya wa Tanzania katika
visiwa vya Commoro Chabaka Kilumanga,Mwakilishi wa kudumu wa Tanzania
Umoja wa Mataifa Geneva Balozi Modest jonathan Mero na Balozi mpya wa
Tanzania katika falme za Kiarabu(UAE)Mbarouk Nassor Mbarouk.Kabla ya
uteuzi Balozi Liberata Mulamula alikuwa msaidi wa Rais Masuala ya
kidiplomasia na aliwahi kuwa katibu mkuu wa nchi za Maziwa Makuu.(picha
na Freddy Maro) Balozi Kilumanga-Commoro Akiapa Balozi Masilingi-Uholanzi akiapa Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk (UAE) akiapa Balozi Mero-Geneva akiapaJaji Aloycius Mujuluzi akiapa
No comments:
Post a Comment