RAIA WAWILI WA BURUNDI WAKAMATWA NA SILA KIGOMA
IGOMA IJUMAA APRILI 13, 2012.
Jeshi la Polisi mkoa wa Kigoma linawashikilia watu wanne wakiwemo
wawili raia wa nchi jirani ya Burundi kwa tuhuma za kupatikana na silaha
mbili za kijeshi aina ya SMG na risasi mbili.
Kaimu
Kamanda wa Polisi mkoani Kigoma SSP Kihenya wa Kihenya, amewataja Raia
hao wa Burundi waliokamatwa kuwa ni Ndolimana Alfred Ndoli(29), mkaazi
wa Lutana Kiharu na Bosco Yohana Gabriel(35), mkaazi wa Kibimba Giharu
ambao walikamatwa katika kijiji cha Nguruka silaha moja wakiwa na SMG
moja yenye namba 56–2500509
Kamanda
Kihenya amewataja Watanzania waliokamatwa sambamba na Warundi hao kuwa
ni Matata Chubwa Ntasamba(36), mkaazi wa kijiji cha Kitanga Wilaya ya
Kasulu na Ndegeya Medard(28), mkazi wa kijiji cha Kitanga wilaya ya
Kasuliu mkoani Kigoma walikamatwa katika Kitongoji cha Lugongoni tarafa
ya Nguruka wakiwa na magazini mbili za SMG na moja kati ya hizo ikiwa na
risasi mbili.
Amesema
kuwa silaha iyoyo na risasi ilipatikana katika kandokando ya mto
Ruguzye uliopo katika pori la kijiji cha mabama wilayani Kinondo baada
ya kutelekezwa na majambazi wasiojulikana kufuatia msako mkali
unaoendelea mkoani humo wa kutafuta silaha na majambazi wa kutumia
silaha.
Katika
tukio lingine Kamanda Kihenye amesema mkazi mmoja wa Kitongoji cha
Mrusi mjini Kasulu, Elizabeth Kanyungu(46), alikutwa akiwa amejinyonga
kwa kutumia kamba ya katani ndani ya nyumba yake.
Kamanda
Kehenye alisema marehemu alijinyunga majira ya saa 6 usiku kwenye
mkesha wa Pasaka wakati familia yake ikiwa kanisani kushiriki ibada ya
pasaka. Amesema Polisi bado wanachunguza kupata chanzo na sababu za mtu
huyo kujinyonga.
Wakati huo huo,
mkazi mmoja wa kijiji cha Kasangezi wilaya ya Kasulu Zakayo Nkika(37),
alipigwa na wananchi wenye hasira kali hadi kufa baada ya kuwajeruhi
watu saba wa kijiji cha Kasangezi wilaya ya Kasulu kwa kuwakatakata kwa
mapanga.
Marehemu
ambaye alielezwa kuwa alikuwa ni mtumiaji wa dawa za kulezwa aina ya
mihadarati aliuawa na wananchi hao wakati akiwa katika ofisi ya mtendaji
wa kijiji hicho alipokamatwa kwa tuhuma za kuwajeruhi watu saba wa
kijiji hicho bila sababu.
Kamanda
Kihenya amewataja waliojeruhiwa kuwa ni Vicent Mdadili(30), Linus
Joseph(25), Samson Rutabina(45), Shukuru Musunu(30), Kulwa Mathias(27),
Rashid Musunu(35) na John Rumie(55) wote wakaazi wa kijiji cha
Kasangezi.
Majeruhi
wote walikimbizwa katika Hospitali ya wilaya ya Kasulu kwa matibabu na
wawili hati yao ambao ni Samson Rutabina na Shukuru Musunu wameelezwa
kuwa hali zao ni mbaya.
Kutokana
na tukio hilo, kamanda Kihenya amewataka wananchi kuaacha kuchukua
sheria mkononi kwa kuwaua watuhumiwa wa makosa mbalimbali kwani amesema
kwa kuwa kufanya hivyo ni kwenda kinyume na sheria na ni kosa la jinai.
No comments:
Post a Comment