Monday, April 30, 2012

            JESHI LA POLISI MUSOMA NGANGARIIIIIIII
ASKARI wa Jeshi la Polisi Kituo cha kati Musoma wakiwaonesha waandishi
wa habari dawa za kulevya aina ya Mirungi iliyokamatwa, pamoja na dawa
za Binadamu aina ya Alu, Amoxiline, Dawa za usingizi, SP, Qunin Syrup,
dawa za Kifua Kikuu kutoka nchini Kenya kuingia nchini kupitia sirari
wilayani Tarime katika kampuni tofauti za mabasi ya Zacharia na Batico
zikiwa zimehifadhiwa kwa mbinu mpya mithili ya mafuta ya kupikia,





Kulia ni Mkuu wa Kituo cha Polisi kati Musoma, Babu Sanare. (Picha na Thomas Dominick)
ASKARI POLISI MMOJA MKOANI KIGOMA AFARIKI KATIKA AJALI YA PIKIPIKI 

Na Pardon Mbwate na Felister Chubwa wa Jeshi la Polisi Kigoma

KIGOMA JUMATATU APRILI 30, 2012. Askari Polisi mmoja wa Kikosi cha Mawasiliano cha Jeshi la Polisi Mkoani Kigoma Kostebo Shaban Hamisi Gobeka(37), amefariki dunia papo hapo baada ya pikipiki aliyokua akiendesha kuacha njia na kugonga mti kushoto pembeni mwa barabara ya Lumumba mjini Kigoma.

Kamanda wa Polisi Mkoani Kigoma Kamishns Msaidizi ACP Frasser Kashai, amesema kuwa ajali hiyo ilitokea jana majira ya saa 12.15 jioni katika mtelemko mkali eneo la Lubengela wakati askari huyo akiendesha pikipiki yenye namba T.757 BYY aina ya Toyo akitokea Mwanga kuelekea Kigoma mjini.

Kamanda Kashai amesema wakati wa ajali hiyo Kostebo Gobeka mwenye namba F. 1561 alikuwa amempakia kijana mwingine aitwaye Filbert Kibuka(25) mkazi wa Mwanga mjini Kigoma ambaye yeye amejeruhuwa vibaya na amelazwa katika Hospitali ya mkoa Maweni kwa matibabu zaidi na hali yake imeelezwa kuwa ni mbaya.

Amesema ingawa Polisi bado inachunguza chanzo cha ajali hiyo, lakini imebainika kuwa imesababishwa na mwendo kasi uliotokana na kukatika kwa bleki ya pikipiki hiyo huku ikiwa kwenye mteremko mkali.

Kamanda Kashai amesema Konstebo Gobeka alikuwa ni dereva wa kutumainiwa wa pikipiki za Polisi na alipata mafunzo ya uendeshaji wa pikipiki ambapo kabla ya kuhamishiwa kikosi cha mawasiliano ya Polisi mkoani hapo, marehemu alikuwa ni miongoni mwa askari waliokuwa wakiendesha pikipiki za doria mkoani Kigoma na hakuwa na kumbukumbu zozote za ajali. 

Hata hivyo Kamanda Kashai amesema Jeshi la Polisi limempoteza Askari shupavu na mchapakazi lakini pia amesema pikipiki aliyopatanayo ajali Askari huyo haikuwa mali ya Jeshi la Polisi. 

Sunday, April 29, 2012

        BISUMWA SI SALAMA KATIKA SUALA LA USALAMA

WANANCHI WA KATA YA BISUMWA KATIKA HALMASHAURI YA MUSOMA VIJIJNI WAMSEMA KUWA HALI YA  USALAMA KATIKA ENEO HILO SI NZURI KUTOKANA NA MATUKIO YA KUTISHIA AMANI YANAYOTOKEA KATIKA ENEO HILO.
WAKIONGEA NA VICTORIA FM HAPO JANA KATIKA ENEO HILO BAADHI YA WANANCHI WAMESEMA KUWA MATUKIO HAYO YANATOKANA NA VIJANA KUKOSA KAZI YA KUFANYA NA HIVYO KUJIKUTA WANAJIINGIZA KATIKA MATUKIO YA UHALIFU.

WAMESEMA KUMEKUWEPO NA WIZI WA MIFUGO NA BAADHI YA WAKAZI KUBOMOLEWA NYUMBA ZAO NYAKATI ZA USIKU KWA LENGO LA KUIBA KITU AMABCHO KINALETA MASHAKA KATIKA MAISHA YA WAKAZI WA ENEO HILO
WANANCHI HAO WAMEWATAKA VIONGOZI KUWA MSTALI WA MBELE KATIKA KUPAMBANA NA SUALA HILO IKIWA NI NJIA YA KUIWEKA JAMII SALAMA NA PIA KUWAWEZESHA VIJANA WA ENEO HILO KUJISHUGHULISHA KATIKA UJENZI WA TAIFA.

NAO VIJANA WA ENEO HILO WAKIONGEA NA KITUO HIKI WAMESEMA KUWA SI KWELI WAO NDIYO CHANZO CHA UHALIFU KATIKA ENEO HILO BALI UHALIFU UNAOFANYWA KATIKA ENEO HILO  HUSABABISHWA NA VIJANA KUTOKA NJE YA ENEO HILO.

WAMESEMA VIJANA WENGI WANAONEKANA KAMA WAHALIFU KUTOKANA NA MUDA MWINGI KUSHINDA WAMEKA VIJIWENI BILA KUJISHUGHULISHA NA HIYO INATOKANA NEO HILO KUKOSA VYANZO MBALIMBALI VYA KUTOA AJIRA.



NAYE MWENYEKITI WA MTAA WA NYABEKWABE MWITA MASHOGU AMEKIRI KUWEPO KWA UHALIFU HUO INGAWA LAWAMA ZIKAELEKEZWA KWA JAMII KUTOKANA NA JAMII HIYO KUSHINDWA KUTOA TAARIFA KATIKA UONGOZI WA KIJIJI HICHO.

AMESEMA JAMII INAPASWA KUBADILIKA KWA KUTOA TAARIFA SEHEMU HUSKA NA PIA KUTOWAFICHA WAHALIFU KATIKA MAENEO YAO
Mripuko kwenye kanisa mjini Nairobi, Kenya, umeuwa mtu mmoja na kujeruhi wengine kadha.

 Polisi wanasema mripuko huo katika kanisa la God's House of Miracle kwenye mtaa wa Ngara, ulisababishwa na guruneti.

 Kumetokea mashambulio kadha ya maguruneti nchini Kenya tangu mwaka jana pale serikali ilipotuma wanajeshi Somalia kupambana na wapiganaji wa Kiislamu, Al-Shabaab.


Saturday, April 28, 2012

                          NAJUA KESHO NAWEZA NISIWEPO KWANI HAPA DUNIANI C KWETU 
 Leo tupo kesho hatupo haina maana leo umalize kila kitu sababu kesho haupo na wala haina maana leo usifanye cha kukusaidia kesho sababu hutokuwepo na wala haikuzuii kutosaidia maskini na yatima sababu kesho wao hawatakusaidia bali upendo wako ndiyo njia yako huko uendako,tujaribu kuishi kama vile kesho tutaonana.Weekend Njema

Friday, April 27, 2012

TUNDU LISSU ASHINDA KESI YAKE YA UBUNGE SINGIDA

Tundu Lissu akimwaga chozi baada ya kushinda kesi yake ya Ubunge

KAMATI KUU YA CCM YAMRIDHIA RAIS KUVUNJA BARAZA LA MAWAZIR

Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi CCM, Nape Nnauye akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar leo,Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, mtaa wa Lumumba, Dar es Salaam, kuhusu maamuzi ya kikao cha Kamati Kuu ya CCM iliyokutana leo mjini Dar es Salaam, ambapo pamoja na mambo mengine imeridhia Rais Kikwete kuvunja Baraza la Mawaziri.

Rais amepokea taarifa na maazimio ya Kamati ya wabunge wa CCM na Kamati ya uongozi ya wabunge wa CCM juu ya kilichotokea kwenye bunge lililopita mjini Dodoma.

Taarifa hizo zimewasilishwa kwenye kamati kuu na kujadiliwa.

Pamoja na taarifa hizo kamati Kuu imepokea taarifa ya jinsi Rais alivyojipanga kuchukua hatua za kuwawajibisha mawaziri na watendaji wa serikali na wale wa mashirika ya umma waliobainika kuhusika na ubadhirifu ulioinishwa na taarifa ya Mkaguzi na mdhibiti mkuu wa hesabu za Serikali, Kamati za kudumu za bunge na wabunge bungeni.

Kamati Kuu imeamua yafuatayo;1. Kamati Kuu inatambua na kuheshimu haki na wajibu wa wabunge kujadili utendaji wa serikali yao.Inapongeza juhudi za serikali kuhakikisha kuwa ripoti ya mkaguzi na mdhibiti mkuu wa hesabu za serikali inajadiliwa kwa uwazi na hivyo kuibua mapungufu yaliyojadiliwa.

2. Kamati Kuu imeridhika na imebariki uamuzi wa Rais KULISUKA UPYA BARAZA LA MAWAZIRI na taasisi zingine zilizoanishwa katika ripoti hizo. Imesisitiza utekelezaji wa uamuzi huo ufanywe mapema iwezekanavyo.

Aidha kamati Kuu imeipongeza Kamati Teule ya baraza la wawakilishi Zanzibar iliyoundwa kuchunguza utendaji katika sekta mbalimbali kwenye serikali ya mapinduzi Zanzibar kwa taarifa yao.Kamati Kuu inawapongeza wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kwa jinsi walivyojadili taarifa hiyo na pia Kamati Kuu inaipongeza Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa kuipokea taarifa na kuanza kuifanyia kazi


                           HUKUMU YA TINDU LISU LEO
 
KESI inayomkabili mbunge wa Singida mashariki kwa tiketi ya CHADEMA, Tundu Lissu, iliyofunguliwa mjini Singida kupinga ushindi uliomweka madarakani, itatolewa kesho ijumaa (Aprili 27, mwaka huu).
 
Hukumu itatolewa na Jaji Moses Mzuna, anayesikiliza kesi hiyo, iliyofunguliwa na makada wawili wa CCM, Shabani Itambu na Pascal Hallu.
 
Kesi hiyo imekuwa kivutio sana kwa wananchi wengi wa mkoa Singida na nchini kwa ujumla, kutokana na umaarufu wa mbunge huyo machachari.
Jaji anayesikilia shauri hilo mjini Singida, anatoka mahakama kuu kanda ya Kilimanjaro.
Walalamikaji wa kesi hiyo, iliyofunguliwa mahakama kuu kanda ya Ddoma, wanatetewa na wakili Godfrey Wasonga, kjtoka mkoani Dodoma, na Lissu amejisimamia mwenyewe.
Kesi hiyo ilianza kusikilizwa Machi 12, 2012, kufuatia makada wawili wa CCM, kupinga ushindi wa Lissu kwa madai kuwa uchaguzi huo uligubikwa na dosari nyingi.
Katika mahojiano na Lissu, amesema vyovyote mahakama itakavyo hukumu, anajivunia kuimarisha demokrasia na kuwa mbunge wa kwanza kutoka upinzani, kwenye historia ya mikoa ya kanda ya kati.
Amesema, kanda hiyo ilijulikana sana kuwa ngome ya CCM, lakini amefanikiwa kuchaguliwa na wananchi ili awatumikie.
                                    CHADEMA YASHINDA CHATO KWA KISHINDO

katika Mkoa mpya wa Geita, CHADEMA kimepata ushindi wa kishindo katika uchaguzi mdogo wa wenyeviti wa serikali za vijiji baada ya kuibwaga CCM kwa kupata vijiji vinane kati ya 11 vilivyokuwa vikishindaniwa.

Uchaguzi huo mdogo wa kuziba nafasi zilizoachwa wazi na baadhi ya viongozi waliokuwepo awali jimboni humo kutokana na sababu mbalimbali, ikiwa ni pamoja na vifo  ambao ulifanyika hivi karibuni uliwafanya baadhi ya Wana CCM kujiunga na CHADEMA mara baada ya matokoeo kutangazwa akiwamo aliyekuwa mgombea wa CCM wa Kijiji cha Minkoto.

Nafasi zilizogombewa zilikuwa zikishikiliwa na viongozi wa CCM kabla ya baadhi yao kujiuzulu, kuhamia vyama pinzani na wengine kuhama makazi yao na kwenda maeneo mengine.

Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari,  msimamizi msaidizi wa uchaguzi huo, Sodio Nyuga alisema CHADEMA kimefanikiwa kutwaa nafasi 8 za vijiji dhidi ya tatu zilizonyakuliwa na CCM .

Hata hivyo, CCM ilijifariji kwa kutwaa uenyekiti katika vitongoji 28 na CHADEMA kikipata nafasi 10, wakati wajumbe wa serikali za mitaa CCM kilijipatia wajumbe 92 na CHADEMA 46.

Katibu wa CHADEMA wa Wilaya ya Chato, Mange Sai, alisema ushindi uliopatikana ni ukombozi mkubwa kwa wananchi wa wilaya hiyo kwa kuwa baadhi ya vitongoji CHADEMA ilipitisha wagombe pasipo kuwa na upinzani wa chama tawala jambo ambalo linaonyesha wazi kukubalika kwa chama hicho kwa wananchi.

Alisema kuwa CHADEMA kilitegemea kuibuka kidedea katika uchaguzi huo mdogo kutokana na wapiga kura kuchoshwa na ahadi mbalimbali za serikali ya CCM ambazo zimekuwa hazina utekelezaji na badala yake baadhi ya viongozi wamekuwa wakijinufaisha kwa maslahi yao binafsi huku wakiwaacha wananchi wakitaabika.

Thursday, April 26, 2012

                                         TUDUMISHE MUUNGANO WETU

 Habari wana wa Afrika,Habari Tanzania,nikiwa kama mmilikiwa blog ya Mwana wa Afrika napenda kuchukua nafasi kuwapongeza Watanzania wote katika kusherekea Miaka 48 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar,si kazi ndogo kudumisha Muungano wetu mpaka kufikia hatua hiyo kwani tumeshuhudia nchi nyingi duniani zinashindwa kuheshimu muungano wanaokuwa nao na kuamua kuuvunja lakini kwetu TUMESHINDA, Eeeeeh Asante Mungu

Pamoja na hayo na mambo mengi katika Muungano wetu bado kuna baadhi ya watanzania wanamtazamo tofauti katika Muungano huo kutokana na kile kinachosemekana baadhi ya sehemu kutonufaika na muunngano huo.

 Katika Muungano wetun kuna mambo mengi ambayo Viongozi wetu walikubaliana kuwa kama sehemu ya Muungano kitu ambacho ni kizuri na cha kupongezwa,baadhi ya sehemu hizo ni kama Mambo ya nje,Jeshi,Polisi,Mamlaka ya dharura,Uraia,Uhamiaji,Biashara ya nje,Utumishi wa umma,Kodi ya mapato, orodha,Bandari, Usafiri wa anga, Posta na Simu.

Hayo ni mambo mengi na ambayo kwa pamoja viongozi wetu waliamua kwa kauli moja  kusema kuwa tushirikiana katika hayo,napenda kuchukua nafasi  hii kama mtanzania halisi,mtiifu na mzalendo kwa nchi yangu kusema kuwa muda umefika Viongozi wetu wamalize tatizo ambalo linaonekana kuwepo kwenye suala la Muungano

Napenda kutoa pongezi kwa Rais mstaafu wa Zanzibar Aman Abed Karume kwa Amani aliyoiacha Zanzibar kwa ushirikiano mkubwa na Katibu mkuu wa Chama cha Wananchi CUfMaalim Self Sharff Hamad,naweza kusema hali iliyokuwepo Zanzibar kabla ya maridhiano ilikuwa inatia shaka katika Muungano wetu

Rai yangu kwa viongozi Muungano ni urithi pekee ambao wazee wetu Mwl Julius Nyerere na Mzee Abed Aman Karume wametuachia hivyo hatuna budi kuuenzi kwa mikono miwili,ili tuuenzi Muungano huo lazima viongozi wawasikilize wananchi nn wanasema juu ya Muungano wao na je wanataka uwe vp ili tuendelee kuudumisha.

Pamoja na hivyo pia ni vyema viongozi wakatathimini Raslimali za nchi zinawanufaisha nchi wote wa Bara na  Visiwani,naamini kama tutaondoa kero hizo bila shaka  Muungano wetu utakuwa wa mfano Duniani.Yapo mengi ila tuanzie hapo kwa leo

                                                                                   Augustine Mgendi
                                                                                  Mwana wa Afrika
                                                                   Wako katika Kudumisha Muungano   wetu            

SERENGETI
Mwanaume mmoja wa wilaya ya Tarime mkoani Mara,anadaiwa kuitelekeza familia yake yenye watoto wanne walemavu aliowazaa na mke wake wa ndoa kwa madai
ya kukwepa mkosi, jambo ambalo limemlazimu mwanamke huyo kuishi maisha ya kutegemea misaada ya majirani kwa ajili ya mahitaji ya watoto wake.

Bi Esther Chacha mkazi wa kitongoji cha Songambele kata ya Sabasaba wilayani Tarime,amesema baada ya kuzaa watoto watano, wanne wakiwa ni walemavu, mme wake huyo ambaye amemtaja kwa jina la Chacha Merengo,aliikimbia familia hiyo na kuoa mke mwingine kisha kwenda kuishi mjini Mugumu Wilayani Serengeti,kwa madai kuwa hawezi kutunza watoto wasio na faida.

Aidha mama huyo ameiomba Serikali na wasamalia wema, kumsadia kutunza watoto hao wenye ulemavu ikiwa ni pamoja na kumsomesha mtoto mmoja ambaye amebahatika kuzaliwa bila ya kuwa na ulemavu katika familia hiyo,ambaye kwa sasa anasoma darasa la saba katika shule ya msingi ya Mturu katika kata ya Rebu ambayo imekuwa akihitunza tangu mwaka 2005 alipachwa na mme wake

Nao baadhi ya majirani wa mama huyo,Bi Esther Eliah na Bi Rose Yohana,wameomba watu ambao wataguswa na mateso anayopata mama huyo katika kulea watoto hao kutoa msaada ambao utamuwezesha kuwatunza watoto wake.

Hata hivyo mme wa mama huyo Bw Chacha Merengo,alipotafutwa kwa njia ya simu kwa zaidi ya mara nane ili kuthibitisha madai hayo hakuweza kupatikana kutoka na simu yake ya mkononi muda wote kuwa imezimwa na juhudi za kumtafuta bado zinaendelea.
               MATUKIO MBALIMBALI KATIKA SHEREHE ZA MUUNGANO


                                       SHEREHE ZA MUUNGANO ZAENDELEA UWANJA WA UHURU

   Amri jeshi Mkuu wa majeshi ya Ulinzi na Usalama nchini  rais Jakaya Kikwete akiingia uwanja wa uhuru                                                                 
               
Majaji katika mahakama maalum kuhusu vita nchini Sierra Leone, leo watatoa hukumu dhidi ya aliyekuwa Rais wa Liberia Charles Taylor kwa kuhusika na vita hivyo vilivyodumu miaka 10.
Charles Taylor
Taylor anasema kesi hiyo ni njama ya kisiasa
Taylor anakabiliwa na mashtaka 11 ikiwemo ubakaji na mauaji ya raia wa Sierra Leone.
Ikiwa atapatikana na hatia atakuwa rais mstaafu wa kwanza kuhukumiwa na mahakama ya kimataifa.
Kiongozi huyo wa zamani anadaiwa kufadhili waasi wa RUF.

Zaidi ya mashaidi 100 wamefika mbele ya mahakama hiyo lakini Bw Taylor amekanusha kuhusika na uhalifu huo wakivita na anadai kuwa kesi hiyo ni njama ya kummaliza kisiasa.

Hukumu ya majaji hao inasubiriwa kwa hamu sana na raia nchini Sierra Leone ambao jamaa zao waliathirika sana wakati wa vita hivyo.

Inakadiriwa kuwa zaidi wa watu elfu 50 waliuawa na wengine wakiwemo wanawake na watoto walibakwa na kukatwa mikono au miguu na waasi wa RUF ambao upande wa mashtaka unasema walipata usaidizi wa silaha kutoka kwa Bw Taylor.

Wakati wa vita hivyo, mwendesha mashtaka anasema kuwa Taylor alikuwa kiungo muhimu katika biashara haramu ya almasi kutoka Sierra Leone.

Kesi hii iliodumu miaka mitatu na nusu, hata hivyo huenda isi kamilike leo kwani pande zote wanauhuru wa kukata rufaa ikiwa hukumu hiyo haitawaridhisha.

Cape Town-Afrika Kusini yasema matatizo ya Afrika yasuluhishwe na Waafrika wenyewe

Afrika Kusini imesema matatizo ya Afrika yanaweza kusuluhishwa na waafrika wenyewe. Hayo yamesemwa jana na waziri wa uhusiano wa kimataifa na ushirikiano wa nchi hiyo Bi Maite Nkosazana-Mashabane alipokuwa akilihutubia bunge.

Bi Nkosazana-Mashabane amezitaka nchi za Afrika kujitegemea katika kusuluhisha migogoro, kupata maendeleo endelevu ya kiuchumi, kuongeza mwingiliano wa kimataifa na kuzidisha biashara kati ya nchi hizo. 

Waziri huyo ametoa wito kwa nchi za bara la Afrika kuinua demokrasia na utawala bora, na kuhakikisha elimu, usalama wa chakula, afya, makazi na ajira vinapatikana kwa watu wote. 

Aidha, Nkosazana-Mashabane amesisitiza nafasi ya Umoja wa Afrika katika kuziongoza nchi hizo kutimiza malengo yake. Ameutaka Umoja huo kujitahidi zaidi katika kuleta maendeleo barani Afrika, ikiwa ni pamoja na kupambana na umaskini, kutokuwa na usawa pamoja na maendeleo duni.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI  

 SERIKALI IWAWAJIBISHE MAWAZIRI WANAOTUHUMIWA KWA UFISADI


Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) unapenda kuwapongeza wajumbe   wa  Kamati za  Kudumu za Bunge za Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC), Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC),  Kamati ya Hesabu za Serikali Kuu, Ardhi Maliasili na Utalii kwa  kusimamia vema na kudhibiti matumizi mabaya ya fedha za serikali zinazotokana na walipa kodi na kuwasilisha ripoti  zao Bungeni ambazo zimeibua uozo mkubwa na kujenga mjadala mpana unaotaka uwajibikaji kwa wanaohusika.

Tunawapongeza pia baadhi ya wabunge  walioshiriki katika mijadala  kwa kuzijadili ripoti hizo kwa undani bila kujali urafiki, itikadi za kisiasa,  hasa ile ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa  kuibua  uozo uliojificha na kusimamia maslahi ya Taifa.

Tumeshuhudia mara kadhaa kupitia vyombo vya habari  wabunge wakiacha itikadi zao za kisiasa na kusimamia kwa dhati dhana ya kushinikiza uwajibikaji katika vyombo vinavyohusika kutokana na ufisadi kama Richmond, Dowans nk. Hata hivyo, TGNP kwa muda mrefu  tumekuwa tukipinga ubadhirifu wa fedha za umma  na kudai haki ili kutokomeza ufisadi uliokithiri, lakini bado ufisadi umezidi kushamiri hasa katika Wizara  na taasisi za umma. Sisi kama wanaharakati tunasema kuendelea kwa ufisadi  ni aibu kwa serikali iliyoko madarakani, TGNP tuko mstari wa mbele  kushinikiza rasilimali za taifa ziwanufaishe wananchi wote, hasa walioko pembezoni, kamwe hatutanyamazia aina yoyote ya ubadhirifu na matumizi mabaya ya fedha za miradi ya wananchi zilizotengwa kwa ajili ya maendeleo ya wananchi.

Tumeshuhudia wanawake na wasichana wakiendelea kuwa maskini na kukumbana na mifumo kandamizi kwa  kukosa haki za kufikia huduma za msingi kama vile   maji, barabara, afya, elimu, kilimo, utawala bora n.k. Fedha zinazopotea zinatokana na kodi za wananchi na jamii ina haki ya kuhoji uwajibikaji na wahusika wanatakiwa kuchukuliwa  hatua za kisheria. 

Tunawapongeza wabunge wote walioshiriki kwa dhati katika zoezi la kusaini kusudio la kutaka viongozi waliotajwa/kutuhumiwa  kwenye ripoti hizo kuwajibika.

Ili kuonesha dhana ya uwajibikaji na utawala bora unaozingatia misingi ya haki za binadamu, tunaitaka serikali kufanya  yafuatayo:
  • Kuwawajibisha mara moja Mawaziri, Manaibu waziri na watendaji wakuu wa serikali na mashirika ya umma ambao wametajwa kuhusika na matumizi mabaya ya fedha za umma au kushindwa kusimamia rasilimali za Taifa.
  • Rais awafute kazi watendaji wanaotumia vibaya fedha za umma na kuwaongezea wananchi umasikini, ili iwe fundisho kwa watendaji wa serikali wenye tabia kama hiyo na wachukuliwe hatua za kisheria.
  • Serikali iboreshe mifumo ya kusimamia rasilimali za nchi yetu ili wananchi wote waweze kufaidi keki ya taifa kwa sababu mara zote serikali imekuwa ikisema Tanzania hatuna rasilimali lakini  hali halisi ni kwamba rasilimali za taifa zinaliwa na mafisadi wachache wa ndani na nje ya nchi.
  Imetolewa na : Anna Kikwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji TGNP

                    MASHUJAA WA MUUNGANO MWALA 1964



Toka kushoto juu ni Bi Sifaeli Choma aliyebeba kibuyu kilichokuwa na udongo  wa Tanganyika na kumkabidhi Mwalimu. Anayefuata ni Bw Omar Hassan Mzee aliyebeba chungu kikubwa ambacho ndicho kilichobeba udongo wa Tanganyika na Zanzibar ambao ulipochanganywa tu ndipo Muungano ukawa umezaliwa, na  kulia ni Bi Khadija Rajab Abbas, aliyebeba kibuyu chenye udongo wa Zanzibar. Mara zoezi hilo lilipokamilika ndipo jina Tanzania likaanza kutumika rasmi. Picha ndogo ya kati inaonesha waasisi wa Muungano wakipita mitaani kusherehekea siku hiyo ya kihistoria, huku wananchi wakiwa wamejipanga barabarani jijini Dar es salaam kuwashangilia wakitokea uwanja wa Uhuru.
 ......................................................................

RAIS Jakaya Mrisho Kikwete leo anatarajia kuwa mgeni rasmi katika madhimisho ya miaka 48 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zitakazofanyika katika uwanja wa Uhuru Dar es Salam.

 Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kaimu Mkuu wa mkoa wa Dar es Salam jana,Bi.Mwamtumu Mahiza alisema kuwa sherehe hizo zitaanza majira ya saa mbili asubuhi ambapo milango ya uwanja huo itafunguliwa kuanzia saa 12 asubuhi.

 ''Sherehe hizi za kiistoria za Muungano zilizo asisiwa na waasisi wetu Baba wa Taifa Julius Nyerere na Hayati Habeid Amani Karume zinatarajia kufana"alisema Bi Mahiza, akiongeza kuwa  viongozi mbalimbali wa vyama na Serikali watahudhuria  katika sherehe hizo akiwemo Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt.Mohamed Shein. 

Alisema kuwa katika kipindi cha miaka 48 Serikali imepata mafanikio makubwa ya kujivunia  katika nyanja mbalimbali zikiwemo za maendeleo ya jamii,uchumi,siasa ulinzi,usalama pamoja na uhusiano wa kimataifa. Kauli mbiu ya mwaka huu ni miaka 48 ya Muungano  shiriki kikamilifu katika sensa na mchakato wa mabadiliko ya katiba.

''Sherehe hizi zitapambwa na gwaride ,halaiki na ngoma kutoka mikoa mbalimbali Tanzania,ambapo pia aliwaomba  SUMATRA na wamiliki wa vyombo vya usafiri kuelekeza magari yao katika kuelekea uwanja wa Uhuru ili kurahisisha usafiri kwa wananchi wa Dar es Salaam"alisema. 

Aliwaomba watanzania kudumisha Muungano kwa ajili ya kizazi cha sasa na kijacho wache kusikia maneno ya mitaani kwa kuwa viongozi waliopita wasisi wetu waliomba tudumishe muungano huo. 

Source Michuzi

                               REAL MADRID YAFA KIUME HISPANIA

               Wachezaji wa Real Madrid wakiwa na huzuni baada ya Ronald kukosa penalt
                                       Utamu wa ushindi kwa Buyern Munich

Wednesday, April 25, 2012

                                                 SIMBA NA VIONGOZI WANASIMBA

TGNP YATAKA MAWAZIRI WANAOTUHUMIWA KWA UFISADI TANZANIA WAWAJIBISHWE

                                          TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

 
SERIKALI IWAWAJIBISHE MAWAZIRI WANAOTUHUMIWA KWA UFISADI
 
Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) unapenda kuwapongeza wajumbe   wa  Kamati za  Kudumu za Bunge za Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC), Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC),  Kamati ya Hesabu za Serikali Kuu, Ardhi Maliasili na Utalii kwa  kusimamia vema na kudhibiti matumizi mabaya ya fedha za serikali zinazotokana na walipa kodi na kuwasilisha ripoti  zao Bungeni ambazo zimeibua uozo mkubwa na kujenga mjadala mpana unaotaka uwajibikaji kwa wanaohusika.
Tunawapongeza pia baadhi ya wabunge  walioshiriki katika mijadala  kwa kuzijadili ripoti hizo kwa undani bila kujali urafiki, itikadi za kisiasa,  hasa ile ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa  kuibua  uozo uliojificha na kusimamia maslahi ya Taifa.
Tumeshuhudia mara kadhaa kupitia vyombo vya habari  wabunge wakiacha itikadi zao za kisiasa na kusimamia kwa dhati dhana ya kushinikiza uwajibikaji katika vyombo vinavyohusika kutokana na ufisadi kama Richmond, Dowans nk. Hata hivyo, TGNP kwa muda mrefu  tumekuwa tukipinga ubadhirifu wa fedha za umma  na kudai haki ili kutokomeza ufisadi uliokithiri, lakini bado ufisadi umezidi kushamiri hasa katika Wizara  na taasisi za umma. Sisi kama wanaharakati tunasema kuendelea kwa ufisadi  ni aibu kwa serikali iliyoko madarakani, TGNP tuko mstari wa mbele  kushinikiza rasilimali za taifa ziwanufaishe wananchi wote, hasa walioko pembezoni, kamwe hatutanyamazia aina yoyote ya ubadhirifu na matumizi mabaya ya fedha za miradi ya wananchi zilizotengwa kwa ajili ya maendeleo ya wananchi
Tumeshuhudia wanawake na wasichana wakiendelea kuwa maskini na kukumbana na mifumo kandamizi kwa  kukosa haki za kufikia huduma za msingi kama vile   maji, barabara, afya, elimu, kilimo, utawala bora n.k. Fedha zinazopotea zinatokana na kodi za wananchi na jamii ina haki ya kuhoji uwajibikaji na wahusika wanatakiwa kuchukuliwa  hatua za kisheria.
 Tunawapongeza wabunge wote walioshiriki kwa dhati katika zoezi la kusaini kusudio la kutaka viongozi waliotajwa/kutuhumiwa  kwenye ripoti hizo kuwajibika.
Ili kuonesha dhana ya uwajibikaji na utawala bora unaozingatia misingi ya haki za binadamu, tunaitaka serikali kufanya  yafuatayo:
  • Kuwawajibisha mara moja Mawaziri, Manaibu waziri na watendaji wakuu wa serikali na mashirika ya umma ambao wametajwa kuhusika na matumizi mabaya ya fedha za umma au kushindwa kusimamia rasilimali za Taifa.
  • Rais awafute kazi watendaji wanaotumia vibaya fedha za umma na kuwaongezea wananchi umasikini, ili iwe fundisho kwa watendaji wa serikali wenye tabia kama hiyo na wachukuliwe hatua za kisheria.
  • Serikali iboreshe mifumo ya kusimamia rasilimali za nchi yetu ili wananchi wote waweze kufaidi keki ya taifa kwa sababu mara zote serikali imekuwa ikisema Tanzania hatuna rasilimali lakini  hali halisi ni kwamba rasilimali za taifa zinaliwa na mafisadi wachache wa ndani na nje ya nchi.

 

                                 YANGA YASHINDA 4-1 DHIDI YA  JKT ORJORO JIJINI  ARUSHA
           

                MWENYEKITI WA MTAA AJIUZULU NA KUHAMIA CHADEMA 

Habari na Ezekiel Kamanga, Mbeya.
 
Wimbi la Wenyeviti wa Mitaa kujuzulu kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM), na kuhamia CHADEMA limeingia katika sura mpya, baada ya Mwenyekiti wa Mtaa wa Ilolo Kati Bwana Ngambi K Ngambi naye kujiuzulu.

Tukio hilo limetokea Aprili 24 mwaka huu katika Mkutano wa hadhara uliofanyika katika mtaa huo na kuhudhuriwa na baadhi ya madiwani wa CHADEMA jijini Mbeya wakiwemo madiwani wa Kata za Mwakibete, Forest, Sinde ambaye alikuwa Mwenyekiti wa Mkutano huo.
 
 
Akifungua mkutano huo Diwani wa Kata ya Sinde Mheshimiwa Fanuel Kyanula, alitoa taarifa ya maendeleo ya ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Sinde ambapo kila mwananchi alikuwa akichangia shilingi 3,000 badala ya shilingi 10,000 za awali.

Aidha mchango huo umesaidia kumalizia kabisa ujenzi wa madarasa hayo, amewashukuru wananchi kwa kuitikia wito wa kuchangia mchango huo bila usumbufu na kipingamizi cochote.

Diwani Kyanula akielezea matumizi ya mchango huo umeweza kukidhi kazi ya upigaji wa sakafu na uwekaji wa nyaya za umeme, hatua hiyo ambayo Mkurugenzi wa Halmashauri alitoa pongezi kwa na usimamizi mzuri hadi kufikia kukamilika kwa ujenzi huo.

Naye Diwani wa Kata ya Mwakibete Bwana Lucas Mwampiki amempongeza mwenyekiti huyo wa mtaa Bwana Ngambi na kwamba ni kiongozi mchapa kazi, hodari na hivyo wao kwa sasa wamempata Kamanda ambaye ataongoza mapambano dhidi ya ubadhilifu.
 
 

Kwa upande wake Bwana Gambi amesema kujiunga kwake CHADEMA ni hiari yake na wala hajalazimishwa na mtu bali ni kuchoshwa ba ukandamizaji ambavyo vilikuwa vikifanywa na CCM naye kwa kuwaonea huruma wananchi aliokuwa akiwaongoza.

Katika mkutano huo watu kadhaa walikabidha Kadi za CCM wakiwemo Rose Mwashilindi (50), Atusekelege Asumbisye (52), ambaye alikuwa balozi wa mtaa huo na Samson Mwakibole.

Katika hadhara hiyo Mwenyekiti wa CHADEMA wilaya ya Mbeya Bwana John Mwambigijaaliwapongeza waliohamia kwa hiari yao kujiunga na Chama hicho na kudai kina watu makini ndio maana kimekua kikipata mafanikio siku hadi siku na kutamba 2015 wataichukua dola.

Kuhama kwa Ngwambi aliyekuwa Mwenyekiti wa mtaa wa Ilemi ni pigo kubwa kwa CCM kwa kipindi cha hivi karibuni kwani Mwenyekiti wa mtaa wa Ilemi Bwana James Joseph Mbela naye alihamia CHADEMA akidia amechoshwa na ufisadi uliokithiri ndani ya CCM.
WATUPA MPANGO WAKE WA MAENDELEO, PIA WAJIPANGA KUKWAMISHA BAJETI, CHADEMA WAANDAA MAANDAMANO

 Daniel Mjema, Dodoma na Editha Majura, Dar

KITENDO cha Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kushindwa kuzungumzia shinikizo la baadhi ya wabunge kutaka mawaziri wanane wajiuzulu, kimeonekana kuwakera wawakilishi hao ambao sasa wameamua kuibana Serikali huku wakiapa kukwamisha bajeti za mawaziri hao katika Bunge lijalo la Bajeti.


Jana walianza kuonyesha makali baada ya kukataa mapendekezo ya Mfumo wa Mpango wa Mabadiliko wa Maendeleo wa Taifa kwa mwaka 2012/2013 wakisema hauna jipya na umetayarishwa kwa mfumo uleule kwa miaka 15 mfululizo.

Juzi, Pinda aliahirisha Bunge bila kugusia shinikizo la wabunge hao kutaka Serikali iwawajibishe Waziri wa Fedha, Mustafa Mkulo; Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja; Waziri wa Uchukuzi, Omar Nundu; Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk Cyril Chami; Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Hadji Mponda; Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Profesa Jumanne Maghembe; Waziri wa Maliasili na Utalii, Ezekiel Maige na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Tamisemi), George Mkuchika.


Wakizungumza na kwa nyakati tofauti jana, wabunge hao, wengi wao wakiwa ni wa CCM, walisema silaha pekee waliyobaki nayo ni kukwamisha Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2012/2013 katika kikao kijacho cha Bunge.
 
Wabunge hao pia wameonya kwamba kutojiuzulu kwa mawaziri hao kutaiweka CCM njia panda katika Uchaguzi Mkuu wa 2015 kwani hoja ya ufisadi ndiyo iliyowafanya wenzao wengi wasirudi bungeni.
 
“Silaha kubwa tuliyobaki nayo sasa ni kura ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu na nakuambia kama ile karatasi ingerudi upya leo idadi ya wabunge wa CCM ambao wangetia saini ingetikisa nchi,” alisema James Lembeli wa Kahama (CCM).
 
Lembeli alisema anashangaa kuona mawaziri waliotakiwa kujipima wenyewe na kuandika barua za kujiuzulu wakigoma kufanya hivyo na Serikali kupuuza hoja hiyo akisema, hatashangaa kuona Watanzania wakiingia mitaani.
 
“Kitendo cha Waziri Mkuu kutosema chochote kuhusu kujiuzulu kwa mawaziri hao wakati akihitimisha Bunge ni kuiingiza nchi kwenye mgogoro mkubwa. Serikali ifahamu kuwa, ipo madarakani kwa ridhaa ya wananchi,” alisema.
 
Lembeli alisema wananchi walipokea kwa shangwe taarifa ya mawaziri hao kutakiwa kujiuzulu lakini, kitendo cha Waziri Mkuu kuwaacha na kuikwepa hoja hiyo alipokuwa akiahirisha Mkutano wa Bunge juzi, kitaongeza chuki ya wananchi dhidi ya Serikali yao kwa kuwa wataamini inawakumbatia mafisadi.
 
 
“Inakuwaje hawa mawaziri wanane tu watake kuitumbukiza nchi kwenye machafuko? Uwaziri ni dhamana aangalie huko kwenye vijiwe na mitaani watu walivyoshangilia kusikia wametakiwa kujiuzulu leo wanagoma, unamgomea nani?” alihoji Lembeli.
 
Lembeli alisema anaamini Rais atafanya uamuzi mgumu na wa haraka kabla ya Bunge la Bajeti vinginevyo Waziri Mkulo na mawaziri wengine watakuwa na wakati mgumu ambao haujawahi kuonekana katika kupitisha bajeti za wizara zao.
Mbunge mmoja wa Viti Maalumu kwa tiketi ya CCM kutoka Kanda ya Ziwa, alisema ukimya wa Rais Kikwete na kiburi cha mawaziri wake wenye tuhuma za kweli kugoma kujiuzulu, kumezidi kukifanya chama hicho tawala kuporomoka umaarufu.

Mbunge wa Ludewa, Deo Filikunjombe (CCM), alisema Rais Kikwete anapaswa kuheshimu maoni na maelekezo ya wabunge na kusema hata kutaka mawaziri wajiuzulu ni utaratibu tu wa kistaarabu.

“Sisi Wabunge 76 tuliosaini hoja ya kutaka Waziri Mkuu ang’oke tumejitoa sadaka kwa maslahi ya nchi lakini naamini wakati wa kumpigia kura Waziri Mkuu, wengi zaidi watatuunga mkono kwa jinsi walivyokerwa na jambo hili,” alisema.
 
“Bunge safari hii limeisha kimyakimya, Spika alipowahoji wanaoafiki hoja ya Waziri Mkuu ya kuliahirisha Bunge waliosema siyo ndiyo waliokuwa wengi na kama ulifuatilia Bunge lilikuwa kimya si kawaida… Rais anatakiwa alione hilo,” alisema.
 
Mbunge wa Kinondoni, Iddi Azzan (CCM), alisema amesikitishwa na hatua ya mawaziri hao kugoma kujiuzulu na kwamba kwa hali ilivyo, busara ya kawaida inataka mawaziri hao wajiuzulu.
 
“Kwa busara ya kawaida wote wanaotuhumiwa kwa wizara zao kufanya madudu wangeacha uroho wa madaraka na kujiuzulu ili kuitikia kilio cha wabunge na Watanzania kwa sababu upepo huko nje sio mzuri hata kidogo,” alisema Azzan.
 
Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina (CCM) alisema taifa limeghafilika kwa sababu wananchi wengi nchi nzima walikaa kwenye luninga na kusikiliza redio juzi jioni wakitarajia Waziri Mkuu angetamka moja kwa moja kuwang’oa mawaziri hao.
 
“Jana kwenye baa na vijiwe ilikuwa kama vile kuna mechi ya kukata na shoka... kwa jinsi idadi kubwa ya wananchi walivyofuatilia hotuba ya Waziri Mkuu lakini mwisho wa siku akawaacha solemba,” alisema.
Nape, Mukama

Baadhi ya wabunge wa CCM waliosaini barua ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu wamedai kuwa Katibu Mkuu wa chama hicho Wilson Mukama amewatisha.

Kanji Lugola wa Mwibara alidai jana kwamba usiku wa kuamkia Jumapili, siku moja baada ya kusaini hati hiyo alipokea simu kutoka kwa Mukama akimtolea maneno makali kutokana na hatua yake hiyo.

“Alizungumza maneno mengi ya vitisho kwa mfululizo bila hata kunipa nafasi ya kujieleza, akasema, ‘nakuja huko wewe na huyo mwenzako mliosaini mtanitambua,’ kuona hivyo tukaondoka Dodoma usiku huohuo,” Lugola alieleza.

Alisema walisafiri hadi Dar es Salaam na kwamba walihudhuria kikao cha Bunge cha Jumatatu iliyopita wakitokea mafichoni.Alipotakiwa kuthibitisha madai hayo Mukama alisema: “Siwezi kutoa habari kwa simu.”

Alipopigiwa tena na kuombwa afuatwe ofisini alisema, “Kwa leo haitawezekana maana niko njiani natokea Dodoma sasa hivi nimefika Gairo, kama unaweza njoo kesho.”

Lugola alidai wakati akipokea vitisho hivyo kutoka kwa Mukama waliokuwa wamesaini kwa upande wa CCM walikuwa yeye na Filikunjombe, baadaye alifuatia na Nimrod Mkono.

                       JOHN MNYIKA ATEMA CHECHE KWA PINDA. 

Katibu Mwenezi wa Chama cha Demakrasia na Maendeleo Mh. John Mnyika  amesema leo mjini Dodoma kuwa  Waziri Mkuu Mizengo Pinda anapaswa kuagiza timu ya wataalamu aliyoiunda kufuatia mkutano wake wadau wa viwanda vya nguo kufanya uchunguzi maalum kuhusu kiwanda cha nguo cha Urafiki.
Mnyika amesema kuwa ukaguzi huo wa Timu ya Wataalamu kwa maagizo ya Waziri Mkuu Pinda utachangia katika kunusuru Kiwanda cha Nguo cha Urafiki dhidi ya udhaifu wa kiutendaji, ufisadi dhidi ya mali za kampuni, kulinda maslahi ya wafanyakazi na kushughulikia kasoro katika mchakato wa ubinafsishaji.
Katika hotuba yake ya kuahirisha bunge tarehe 23 Aprili 2012 Waziri Mkuu Pinda alieleza taifa kuwa kufuatia mkutano wake na wadau wa tarehe 23 Machi 2012 ameunda kamati ya wataalamu ya kuangalia changamoto zinazokabili viwanda vya nguo nchini ili kuviwezesha kuchangia kwenye mapato ya nchi na katika kuongeza ajira.
Hatahivyo Mnyika amesema ni muhimu Waziri Mkuu Pinda na timu ya wataalamu hao wakazingatia kuwa matatizo ya kiwanda cha urafiki ni zaidi ya changamoto za kawaida kwa kuwa ni matokeo ya kasoro katika mchakato mzima wa ubinafsishaji, udhaifu wa kiutendaji wa miaka mingi pamoja na ufisadi uliokithiri unaohitaji uchunguzi maalum.
Kutokana na hali hiyo Mnyika ametoa wito kwa Serikali kuingilia kati kupitia Wizara ya Fedha hususani Ofisi ya Msajili wa Hazina na Shirika Hodhi la Mali za Mashirika ya Umma (CHC) na Wizara ya Viwanda na Biashara kuchukua hatua zinazostahili juu ya kiwanda cha Urafiki.
Aidha, kamati ya kudumu ya Bunge ya Viwanda na Biashara kuchukua hatua za kuisimamia serikali ili kuharakisha hatua za kunusuru kiwanda hiki ili kuonyesha pia mfano wa hatua zinazopaswa kuchukuliwa kuhusu viwanda vingine. Hata hivyo mpaka sasa hakuna hatua kamili zilizochukuliwa na Wizara na Mamlaka husika hivyo Waziri Mkuu Pinda anapaswa kuingilia kati kusukuma hatua kuchukuliwa baadala ya kutoa kauli za ujumla kwamba serikali inalinda viwanda vya ndani.

               Bastola ya Kanumba yasakwa,baada ya Wiki mbili ya kifo

Bastola ambayo inadaiwa ilikuwa ikitumiwa kihalali na staa wa filamu barani Afrika, Steven Charles Kanumba, inasakwa na Jeshi la Polisi Tanzania.

Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi, Kinondoni, Dar es Salaam, ACP Charles Kenyela amesema kuwa anafuatilia kumbukumbu za silaha hiyo, kwani haijarejeshwa kwenye jeshi lake.

Kenyela alisema juzi kuwa anafuatilia juu ya umiliki huo na baada ya hapo, jeshi la polisi litawahoji ndugu wa msanii huyo kuhusu kurejesha bastola hiyo jeshini.



“Bastola ni mali ya serikali. Kuna hatua ambazo hufuata mpaka mtu aruhusiwe kumiliki bastola,” alisema Kenyela na kuongeza:“Endapo mmiliki halali wa silaha hiyo atafariki dunia, ndugu zake lazima waikabidhi kwa jeshi la polisi na baada ya hapo, kama kuna ndugu anataka aimiliki tena, inabidi afanye maombi upya na atakapokidhi vigezo ndiyo ataruhusiwa.

“Kutokana na hali hiyo, bastola ya Kanumba lazima irudi kwetu haraka na kama kuna ndugu yake yeyote anataka kuimiliki, itabidi awasilishe maombi.”
Kenyela aliongeza kuwa hivi sasa anafuatilia kumbukumbu za jeshi la polisi ili awe na uhakika kama kweli msanii huyo alikuwa anamiliki silaha hiyo.

“Tukithibitisha tutawahoji ndugu zake pamoja na wengine wanaohusika ili tuwe na taarifa za hiyo silaha. Ila kwa sasa tunafanyia kazi taarifa hizi kwa kupitia kumbukumbu za jeshi,” alisema.
Kenyela alitoa ufafanuzi huo baada ya kuulizwa na mwandishi wetu kama jeshi lake limeshapokea bastola ambayo alikuwa anaitumia Kanumba enzi za uhai wake.

NDUGU WANASEMAJE?
Mama mzazi wa Kanumba, Flora Mtegoa, alipoulizwa na paparazi wetu kuhusu bastola inayodaiwa kutumiwa na mwanaye alipokuwa hai, alikuwa na haya ya kujibu:
“Sijaiona hiyo bastola humu ndani tangu nimefika hapa. Sijui ipo wapi na sijui kama kweli Kanumba alikuwa anamiliki hiyo silaha.
“Najua sheria za silaha hiyo, kwa hiyo ingekuwepo ningeiwasilisha polisi haraka. Baba yangu alikuwa na silaha hiyo, alipofariki dunia tuliikabidhi kwa jeshi la polisi.”

NANI ANAJUA ILIPO?
Taarifa zinaonesha kuwa mdogo wa Kanumba, Seth Bosco alikuwa karibu zaidi na marehemu lakini kwa sababu umiliki wa silaha hiyo ni siri, siyo rahisi kujua ilipo.
Mtu mwingine ambaye alikuwa karibu na marehemu mpaka nyakati za mwisho za uhai wake, kama ripoti zinavyoonesha ni muigizaji Elizabeth Michael ‘Lulu’ (pichani), ingawa naye inawezekana hajui kutokana na unyeti wa silaha yenyewe.

BASTOLA NA KANUMBA
Akiwa hai, Kanumba aliwahi kuripotiwa mara kadhaa kumiliki silaha hiyo, japo haikufafanuliwa kama ni kihalali au batili.
Kanumba aliripotiwa kwa mara ya kwanza kumiliki bastola miaka minne iliyopita, akidaiwa kuichomoa baada ya kuvamiwa na kundi la watu aliohisi wanataka kumteka.
Licha ya stori hiyo kuandikwa gazetini na nyingine ambazo zilimhusisha na umiliki wa bastola, bado Kanumba hakuwahi kufafanua chochote kuhusu silaha hiyo.

IPO WAPI?
Je, aliiacha sehemu ambayo hakuna mtu anayeweza kupafikia?
Aliirejesha kabla mauti hayajamkuta ndiyo maana haionekani?
Je, Kuna mtu aliiwahi baada ya kifo chake kwa kuona ni dili?
Kanumba alifariki dunia Aprili 7 na kuzikwa Aprili 10, 2012 kwenye Makaburi ya Kinondoni, Dar es Salaam.
CHELSEA YASONGA MBELEEEEE KWA JUMLA YA MBAO 3--2,YATOKA SARE 2-2 BARC

Tuesday, April 24, 2012

  Waandamana nusu uchi kulalamikia polisi

 Kundi la wanawake wamevua nguo, nusu uchi kulalamikia kitendo cha polisi wa Uganda anayedaiwa kumdhalilisha kingono mwanasiasa wa upinzani. Kanda ya video imeonyesha polisi akimtomasatomasa matiti Bi Ingrid Turinawe wa chama cha upinzani cha Forum for Democratic Change (FDC) baadaya kumkamata kuzuia maandamano ya wiki jana.

Naibu kamishina wa polisi Andrew Kaweesa ameomba radhi na kuahidi kufanya uchunguzi kutokana na tukio hilo. Tangu uchaguzi mkuu mwaka 2011 ambapo rais Yoweri Museveni alishinda Uganda imeshuhudia maandamano ya upinzani ambapo wafuasi wengi wameishia celi za polisi.


Tukio la wiki jana lilipelekea kuwepo ghadhabu ya umma ambapo pia lalama zilitanda kupinga kukamatwa kwa Bi Turinawe ambaye ni kiongozi wa tawi la wanawale katika chama cha FDC kinachoongozwa na Kizza Besigye.

Mwandishi wa BBC Siraj Kalyango amesema wanawake hao waliandamana hadi kituo cha polisi wakiwa vifua wazi na kupeperusha mabango yaliokuwa na maandishi,”utahisi vipi ikiwa sehemu zako nyeti zitafinywa”.Wanawake sita walikamatwa baada ya kukataa kufunika vifua vyao, lakini wakaachiwa huru bila masharti yeyote.
ASKARI POLISI WANNE WAFUKUZWA KAZI KIGOMA KWA KUOMBA NA KUPOKEA RUSHWA

JESHI la Polisi mkoani Kigoma leo limewafukuza kazi askari wake wanne kwa tuhuma za kudai na kupokea rushwa ya dola 300 za Kimarekani kutoka kwa raia mmoja wa China kinyume na maadili ya Jeshi hilo .

Kamanda wa Polisi mkoani Kigoma Frasser Kashai amewataka mwenye namba E.3890 CPL Admirabils Malaso(43), G. 814 PC Waziri Juma Rashidi(30) G. 3012 PC Makasi Edwin(25) na  G. 3322 PC Elias Zakaria(24) ambao wote walikuwa wakifanyia kazi katika kituo cha Polisi Uvinza wilaya ya Kigoma
Vijijini.




Kamanda Kashai amesema kuwa mnamo Aprili 1, 2012 majira ya saa 5.00 usiku askari hao wakiwa zamu katika kituo hicho cha Polisi Uvinza, walipokea taarifa kwa njia ya simu ya mkononi kutoka kwa dada mmoja aitwaye Mary Kapele(26) akiwaeleza kuwa yuko katika nyumba moja ya kulala wageni ya Manchester na alikuwa na Raia mmoja wa Kichina mmoja wa wasimamizi wa ujenzi wa barabara ya kutoka Kigoma Uvinza na kwamba waende kumshika ugoni ili wajipatie fedha na baadaye kugawana na dada huyo.

Askari hao walikwenda katika nyumba hiyo ya kulala wageni na kumkamata Mchina huyo aitwaye Mafutao War, akiwa pamoja na dada huyo kisha wakamtaka atoe fedha kama malipo ya kumshika ugoni na ndipo walipopewa kiasi cha dola 300 za kimarekani na shilingi 10,000 za Kitanzania na kumuachia. Kamanda kashai amesema kuwa mlalamikaji Bw. War alikuwa ni mkandarasi wa ujenzi wa barabara ya Kigoma Uvinza.

Kamanda Kashai alisema baada ya kuona tukio hilo, raia wema walitoa taarifa Polisi mkoani Kigoma ambapo askari hao walikamatwa na baada ya uchunguzi kufanyika walibainika kuwa walihusika na tukio hilo na ndipo waliposhitakiwa kijeshi na kupatikana na hatia ya kufanya Kitendo kibaya kinyume na mwenendo mwema wa Jeshi la Polisi.

Amesema kufuatia hukumu hiyo ameamua kuwafukuza kazi kwa fedheha ili iwe fundishi kwa askari wengine kufuata utaratibu na sheria katika utendaji wa kazi zao za kila siku.

Kamanda Kashai amesema Koplo Admirabils Malalo ambaye alizaliwa Julai 1, 1969 katika kijiji cha Kilando wialaya ya Nkasi mkoani Rukwa,   alijiunga na Jeshi la Polisi Julai 26, 1991 na hadi anafukuzwa amelitumikia Jeshi hilo kwa muda wa miaka 11, Kostebo Waziri Juma Rashidi alizaliwa  Julai 1, 1982 katika kijiji cha Maisaka wilaya ya Babati mkoani Manyara, na alijiunga na Jeshi la Polisi Februari  05, 2007 na hadi kufukuzwa kwake alikuwa amelitumikia Jeshi la Polisi kwa muda wa miaka mitano.

Amesema Konstebo Makasi Edwin ambaye alizaliwa Februari 28, 1987 huko kwenye eneo eneo la Mabatini mjini Mwanza la na kujiunga na Jeshi la Polisi Juni 28, 2009 amelitumikia Jeshi hilo kwa muda wa miaka mitatu na Konstebo Elias Zakaria ambaye alizaliwa  mwaka Julai 1, 1988 huko katika eneo la Nguvumali mjini Tanga na alijiunga na Jeshi la Polisi Juni 28, 2009 ambaye naye pia amelitumia Jeshi hilo kwa muda wa miaka mitatu tu.

Kamanda kashai amesema kuwa Jeshi la Polisi halitasita kumchukulia hatua kali za kisheria na hata kumfukuza kazi askari yeyote atakayebainika kwenda kinyume na maadili ya Jeshi hilo iki ni pamoja na kujihusisha na vitendo vya utovu wa nidhamu, uhalifu ukiwemo wa kudai na kupokea rushwa.

Taarifa hii ni kwamujibu wa Afisa Habari Mkuu wa Jeshi la Polisi Zanzibar , Inspekta Mohammed Mhina.