Monday, February 27, 2012

HABARI KUTOKA MARA

MUSOMA

KAMPUNI MOJA YA KUCHAMBUA PAMBA NA KUKAMUA MAFUTA YA BIRCHAND OIL MILL YA JIJINI MWANZA, IMEKIRI KUSAMBAZA SEHEMU YA MBEGU ZA PAMBA KWA WAKULIMA WA BAADHI YA MAENEO YA WILAYA SENGEREMA MKOANI MARA AMBAZO ZIMESHINDWA KUOTA KATIKA MSIMU WA KILIMO WA MWAKA HUU.
 
MKURUGENZI MTENDAJI WA KAMPUNI HIYO BW MOHAMED SHARIFF, AMESEMA MBEGU HIZO ZA PAMBA AMBAZO NI SEHEMU YA TANI YA ELFU TANO ZILIZOSAMBAZWA KATIKA MAENEO YANAYOLIMA ZAO LA PAMBA KWA MIKOA YA KANDA YA ZIWA, ZIMESHINDWA KUOTA KUTOKANA NA WAKULIMA WENYEWE KUWEKA MAJI KATIKA PAMBA KWA LENGO LA KUONGEZA UZITO, JAMBO AMBALO LIMESABABISHA PAMBA NA MBEGU ZAKE KUARIBIKA KABLA YA KUREJESHWA KWA WAKULIMA KWAAJILI YA KUPANDWA.

HATA HIVYO AMESEMA TATIZO HILO, IMESABABISHA PAMBA ZAIDI YA TANI MILIONI 7 YENYE THAMANI YA SHILINGI BILIONI 7 KUHARIBIKA NA HIVYO KUWEZA KUUZWA SEHEMU YOYOTE DUNIANI, HUKU KAMPUNI YAKE IKITOA MBEGU NYINGINE KWAAJILI YA KUPANDA AMBAPO AMETUMIA NAFASI HIYO KUWATAKA WAKULIMA WAFIKIRIE KUTOA FIDIA YA HASARA AMBAYO WAMEISABABISHA KWA WENYE VIWANDA.

TAARIFA ZAIDI ZINASEMA KUWA BAADHI YA MAENEO YANAYOLIMA ZAO LA PAMBA KATIKA MIKOA YA KANDA YA ZIWA, UMEBAINI KUWA WAKULIMA WENGI WAMEKUWA WAKIWEKA MAJI KATIKA PAMBA KWA LENGO LA KUONGEZA UZITO KWA MADAI YA KUKABILIANA NA WIZI KATIKA MIZANI JAMBO AMBALO LIMECHANGIA KUHARIBU UBORA WA PAMBA.

 ,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,

WAFANYA BIASHARA WA SOKO LA MWIGOBERO MANISPAA YA MUSOMA MKOANI MARA WAMEITAKA SERIKALI KUBORESHA MAZINGIRA YA SOKO HILO NA KUIMARISHIA ULINZI KUTOKANA NA UPOTEVU WA BIDHAA UNAOTOKEA MARA KWA MARA KATIKA SOKO HILO.
 
WAKIZUNGUMZA NA KITUO HIKI LEO ASUBUHI KATIKA SOKO HILO, WAFANYABIASHARA HAO WAMESEMA KUWA WANAOMBA UONGOZI WA MANISPA KUBORESHEA MAENEO YA SOKO HILO IKIWEMO KUJENGEWA MEZA ZA KUDUMU KWANI MEZA WALIZONAZO NI ZAWATU BINAFSI NA ZINALIPIWA USHURU KIASI CHA SHILINGI ELFU KUMI KWA MWEZI.

AIDHA MKUU WA SOKO LA MWIGOBERO VEDASTUS MANOTI AMESEMA SWALA LA ULINZI KATIKA SOKO HILO SI WA KURIDHISHA KUTOKANA NA WALINZI WALIOPO KUTOTEKELEZA MAJUKUMU YAO KIKAMILIFU.

AMEONGEZA KUWA KUMEKUWEPO NA WIZI WA BIDHAA NA VIFAA VYA WAFANYABIASHARA KATIKA SOKO HILO KITU AMBACHO KINARUDISHA NYUMA JUHUDI YA KUJIKWAMUA KATIKA JANGA LA UMASKINI.

MKUU HUYO WA SOKO AMETUMIA NAFASI HIYO KUIOMBA MANISPAA YA MUSOMA KURUDISHA ASKARI WALIOKUWEPO KATIKA SOKO HILO BAADA YA KUHAMISHA KWANI INASEMEKANA ASKARI HAO WALIWEZA KUDHIBITI SUALA ZIMA LA ULINZI KATIKA SOKO HILO.

,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,

TARIME

WANAFUNZI WA SHULE YA SEKONDARI YA UFUNDI SAMARTAN ILIYOKO CHINI YA KANISA LA KIINJIRI LA KIRUTHELI TANZANIA (KKKT) WAMEWALALAMIKIA WALIMU KUWACHAPA VIBOKO VISIVYOKUWA NA IDADI KATIKA SEHEMU MBALIMBALI ZA MIILI YAO

WAKIONGEA KWA MASIKITIKO NA MWANDISHI WA HABARI HII WANAFUNZI HAO WAMESEMA KUNA BAADHI YA WALIMU WAO WAMEKUWA WAKIWACHAPA VIBOKO MGONGONI NA MIGUUNI WAKATI MWINGINE KUWAPIGA MAKOFI HALI AMBAYO INAWANYIMA FURAHA WAWAPO SHULENI.

BAADHI YA WANAFUNZI WAMEONYESHA KUKATA TAMA KUENDELEA NA MASOMO SHULENI MARA BAADA YA TUKIO LA MWENZAO DAMIAN WA KIDATO CHA PILI KUCHARAZWA VIBOKO VISIVYO NA IDADI PAMOJA NA KUPIGWA MAKOFI BAADA YA KUCHELEWA KUINGIA DARASANI HALI AMBAYO ILIMLAZIMU KUKIMBIA NA KURUKA UZIO WA SHULE KAMA NJIA YA KUJINUSURU.
 
AIDHA WANAFUNZI HAO WAMESEMA KUWA KUENDELEA KUWEPO KWA VIPIGO VIKALI VIMEPELEKEA KUOGOPA HATA KUSIMAMA KUULIZA AU KUJIBU SWALI PINDI WAWAPO DARASANI KUTOKANA NA UWOGA WALIOJENGEWA NA WALIMU WAO.

BAADHI YA WAZAZI WAMEWATAKA WALIMU KUACHA KUWACHARAZA FIMBO SISIZOKUWA NA IDADI KATIKA SEHEMU MBALIMBALI ZA MWILI NA KUONGEZA KUWA KITENDO HICHO KINAWAFANYA WATOTO WAZIDI KUWAOGOPA HALI AMBAYO HUWENDA IKASHUSHA KIWANGO CHA TAALUMA AU WATOTO KUACHA SHULE.
,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,

MWANZA.

MKUU WA MKOA WA MWANZA, INJINIA EVARIST  NDIKILO AMEZIAGIZA HALMASHAURI ZOTE ZA MKOA HUO KUHAKIKISHA ZINAJIKITA ZAIDI KUWAHAMASISHA NA KUTOA ELIMU KWA WANANCHI KATIKA SUALA ZIMA LA KUANZISHA MIRADI UFUGAJI NYUKI KWA KILA WILAYA MKOANI HUMO.

MKUU WA MKOA NDIKILO AMETOA MAAGIZO HAYO WAKATI WA ZIARA YAKE YA SIKU MOJA YA KUTEMBELEA NA KUKAGUA MIRADI MBALIMBALI YA MAENDELEO KATIKA WILAYA YA MISUNGWI MKOANI MWANZA AMBAPO PAMOJA NA MAMBO MENGINE ALIJIONEA UANZISHWAJI WA MRADI WA KUFUGA NYUKI KATIKA KIJIJI CHA NGUDAMA AMBAPO TAYARI MIZINGA YA NYUKI IMESHAANZA KUWEKWA  KUANZA UFUGAJI HUO.

MKUU WA MKOA HUYO AMESEMA KUWA ANATAKA MKOA WA MWANZA UNAKUWA MFANO WA KUIGWA KATIKA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI JUU YA UFUGAJI HUO WA NYUKI HUKU AKIWATAKA MAOFISA NYUKI NA USTAWI WA JAMII WA KILA WILAYA KUACHANA NA TABIA MBAYA YA KUKAA MAOFISINI WAKISUBILI KUPELEKEWA TAARIFA, BALI WAENDE KWA WANANCHI KWA AJILI YA KUTOA ELIMU NA HAMASA HIYO YA KUANZISHA MIRADI YA MIZINGA YA NYUKI.

KWA MUJIBU WA NDIKILO, UFUGAJI WA NYUKI UNACHOCHEA MARADUFU KUINUA VIPATO VYA WANANCHI, KWANI SOKO LA ASALI NA NTA NI KUBWA HAPA DUNIANI, HUKU AKITOLEA MFANO WA AMERIKA KUSINI AMBAPO AMESEMA WANANCHI WA MAENEO HAYO HUKO WAMEPATA MAENDELEO MAKUBWA KWA SABABU YA KUUZA ASALI NA NTA INAYOTOKANA NA UFUGAJI WA NYUKI KATIKA MIZINGA YA KISASA.

AMESEMA AWALI MKOA WA TABORA ULIKUWA UMAARUFU KATIKA SUALA ZIMA LA UFUGAJI WA NYUKI NA UUZAJI WA ASALI NA NTA NDANI NA NJE YA NCHI, LAKINI KWA SASA ASALI YA TABORA IMEANZA KUSHUKA SOKO DUNIANI KUTOKANA NA ULIMAJI MKUBWA WA TUMBAKU AMBAO KIMSINGI NYUKI HUTUMIA MAUA YAKE KUTENGENEZA ASALI YENYE KEMIKALI.

HATA HIVYO, MKUU HUYO WA MKOA WA MWANZA, AMEWATOA WASIWASI WANANCHI JUU YA UPATIKANAJI WA SOKO LA ASALI NDANI NA NJE YA NCHI, NA KWAMBA SERIKALI IPO TAYARI KUANZA KUSAKA MASOKO YENYE UHAKIKA KWA AJILI YA UUZAJI WA ASALI NA NTA DUNIANI.

,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,

Senegal yaelekea duru ya pili ya Uchaguzi

                            Bw Macky Sall analeta upinzani mkali kwa Rais Wade


Mchuano mkali unaendelea katika uchaguzi wa Urais wenye utata nchini Snegal kati ya Rais wa sasa Abdoulaye Wade na waziri mkuu wa zamani Macky Sall.
Taarifa za awali kutoka Senegal ambazo hazijathibitishwa zinaonyesha kuwa kuna mchuano mkali kati ya Rais wa sasa Abdoulaye Wade na waziri mkuu wa zamani Macky Sall na vyombo vya habari vya ndani na Bw Sall vinasema hakuna mgombea aliyefikia 50% inayotakiwa kuepuka duru ya pili.
Rais Wade, 85, anawania kwa awamu ya tatu nafasi hiyo licha ya kutumikia vipindi viwili vinavyoruhusiwa na katiba.
Bw Wade alizomewa wakati alipokwenda kupiga kura Jumapili katika mji mkuu,Dakar.
Walisikika wakipiga kelele: "toka huko, mzee wewe!"
Uamuzi wa Bw Wade wa kusimama tena umesababisha wiki kadhaa za ghasia na vifo vya watu sita ingawa siku yenyewe ya kupiga kura ilikuwa nay a amani kwa sehemu kubwa.
Taarifa za awasli zinaonyesha kuwa Bw Wade na Bw Sall wote wamepata ushindi kati ya kura 20-35%.
Tume ya uchaguzi haijathibitisha bado matokeo hayo ya awali ambayo yametangazwa na vyombo vya ndanikamayanavyoletwa kwenye vituo vya kupigia kura.
Bw Wade alipoteza kura kwenye jimbolakemwenyewekatika eneo la watu wa kati mjiniDakarjirani na Kituo E, Shirika la Habari la Senegal APS limeripoti.
Mchuano kati ya Abdoulaye Wade na Macky Sall

Abdoulaye Wade

  • Umri: 85
  • Mgombea mkongwe wa upinzani
  • Alichaguliwa mara ya mwisho mwaka 2000,kwa ahadi za mabadiliko
  • Ana mipango mikubwa ya miradi ya kuindeleza Senegal
  • Anatuhumiwa kumuandaa mwanawe, Karim, kuchukua nafasi yake

Macky Sall

  • Umri: 50
  • Meya wa mji wa Magharibi wa Fatick
  • Waziri mkuu wa zamani
  • Alipishana na Rais baada ya kumtaka Karim Wade ajibu maswali bungeni
  • Ni mgombea pekee wa upinzani kufanya kampeni kwa nchi nzima.
Kambi ya Bw Wade imesema Rais wa sasa ana uhakika wa ‘kushinda kwa kishindo’ katika duru ya kwanza.
Lakini Bw Sall anaamini anaamini kuwa "duru ya pili ni lazima, tumeshinda sehemu muhimu nchini."
Mtaalamu huyo wa madini mwenye umri wa miaka 51na meya wa mji wa magaharibi wa Fatick, anayewania kwa mara ya kwanza alionya pia kuhusu udanganyifu katika kura.
Mwandishi wa BBC Thomas Fessy mjiniDakaranasema Bw Sall amekuwa mgombea pekee wa upinzani anayeendesha kampeni makini nchi nzima huku wagombea wengine wakijihangaika kuwahamasisha watu kwenye mitaa yenye maandamano.
Iwapo dura ya pili imethibitishwa muungano wa "yeyote isipokuwa Wade" unaweza kuwa ushindi nyuma ya Bw Sall, mwandishi wa BBC anasema.
Mahakama ya Kikatiba yaSenegaliliamua Bw Wade anaweza kuwania tena kwa misingi kuwa awamu yake ya mwanzo haikuhesabiwa kwani ilianza kabla ukomo wa awamu mbili haujawekwa kisheria mwaka 2001.
Mahakama pia ilimzuia mwanamuziki mashuhuri duniani Youssou N'Dour kugombea katika uchaguzi huo.
Bw N'Dour alisema kuwa kumruhusu Bw Wade kuwania tena kunasebabisha mapinduzi ya kikatiba.
Senegal, koloni la zamani la Ufaransa, inaonekana kuwa thabiti kidemokrasia na mfululizo wa uchaguzi tangu uhuru mwaka 1960.
Inabakia nchi pekee ya Afrika Magharibi ambako jeshi halijachukua madaraka
BBC

Sunday, February 26, 2012

TAARIFA KUHUSU DAWA BANDIA YA MALARIA

TAARIFA KWA UMMA
TAARIFA KUHUSU UWEPO WA DAWA BANDIA YA KUTIBU UGONJWA WA MALARIA IITWAYO ELOQUINE (Quinine Sulphate 300mg USP)

Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) ni wakala wa Serikali iliyo chini ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii yenye jukumu la kudhibiti ubora, ufanisi na usalama wa vyakula, dawa, vipodozi na vifaa tiba ili kulinda afya ya jamii.

TFDA inapenda kuutaarifu umma kuwa imebaini kuwepo kwa dawa bandia ya kutibu ugonjwa wa Malaria katika soko. Dawa hiyo inaitwa Eloquine (Quinine Sulphate 300mg U.S.P) na ipo katika makopo ya vidonge 1000 (elfu moja) kila moja. Maelezo yaliyopo katika lebo yanaonesha kuwa dawa hiyo imetengenezwa na kiwanda cha Elys Chemical Industries Ltd cha nchini Kenya.

Hata hivyo, TFDA imebaini kuwa kiwanda cha Elys Chemical Industries Ltd hakitengenezi dawa yenye jina la biashara la ‘ELOQUINE’. Kiwanda hicho kimesajili Tanzania Quinine Sulphate 300mg B.P isiyo na jina la kibiashara. Aidha, kiwanda cha Elys Chemical Industries Ltd kimebainisha tofauti mbalimbali zilizopo katika lebo ya dawa bandia ikilinganishwa na dawa halisi inayotengenezwa na kiwanda hicho iliyosajiliwa na TFDA na hivyo kuthibitisha kuwa kiwanda hicho hakitengenezi dawa hiyo.

Katika kudhibiti usambazaji wa dawa hiyo hapa nchini, hadi sasa TFDA imekamata jumla ya makopo 155 ya dawa hiyo bandia ya Eloquine jijini Dar Es Salaam yaliyokuwa yakisubiri kusambazwa. Aidha, kopo moja lenye vidonge 115 limekamatwa Moshi, Kilimanjaro. Tayari mtuhumiwa mmoja amekwishafikishwa mahakamani na upelelezi wa chanzo na wasambazaji wa dawa hii unaendelea kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi.

Uchunguzi wa dawa bandia katika maabara umebaini kuwa vidonge hivyo havina kiambato hai (active ingredient) cha Quinine Sulphate kwa ajili ya kutibu ugonjwa wa Malaria na hivyo matumizi yake ni hatari kwa afya ya binadamu.


Wafanyabiashara wote wa dawa na wananchi wanatahadharishwa kutozitumia dawa hizi na wale wote waliouziwa dawa hizi wanaelekezwa kuzirudisha dawa hizo katika ofisi za TFDA, vituo vya afya vya Serikali au vituo vya polisi vilivyo jirani nao.

TFDA inapenda pia kuwakumbusha wafanyabiashara wa dawa, wasafirishaji wa vifurushi na wananchi kutoa taarifa haraka iwezekanavyo pale wanapohisi kuuziwa dawa duni, bandia au zilizoisha muda wa matumizi. Taarifa zitolewe ofisi za TFDA makao makuu zilizopo Barabara ya Mandela, EPI Mabibo External, Dar es Salaam na Ofisi za Kanda zilizopo mtaa wa Nkurumah, Mwanza, Mtaa wa Sakina – Arusha, Hosptali ya mkoa ya Dodoma na Jengo la Ofisi ya Mifugo Mkoa wa Mbeya.

Kwa maelezo zaidi wasiliana na:-
MKURUGENZI MKUU
MAMLAKA YA CHAKULA NA DAWA
EPI MABIBO EXTERNAL,
S.L.P 77150, DAR ES SALAAM

Simu: + 255 222 450512/450751/452108
Nukushi: + 255 222 450793
Barua pepe: info@tfda.or.tz
Tovuti: www.tfda.or.tz

Friday, February 24, 2012

HABARI KUTOKA MARA

MUSOMA

WAFANYABIASHARA WA DAGAA KATIKA SOKO LA MWIGOBERO, MANISPAA YA MUSOMA MKOANI MARA, WAMELALAMIKIA KUTOZWA USHURU WA SHILINGI 1000, BADALA YA SHILINGI 300 KWA KILA MZIGO BILA KUPEWA STAKABADHI NA MZABUNI AMBAYE AMEPEWA KAZI YA KUKUSANYA USHURU WA MANISPAA HIYO.

WAKIZUNGUMZA SOKONI HAPO  BAADHI YA WAFANYABIASHARA WAMESEMA KUWA MZABUNI HUYO AMEKUWA AKIPANDISHA USHURU KILA KUKICHA HUKU AKITOA RISTI YA SHILINGI MIA TATU HATUA AMBAYO IMEKUWA IKISABABISHA MGOGORO MKUBWA.

MIONGONI MWA WAFANYABIASHARA HAO BW JOSEPH NYANGASI NA BW SHABAN MATUMBO,WAMESEMA KITENDO CHA KUWATOZA USHURU HUO MKUBWA BILA STAKABADHI KUTOKA SHILINGI MIA TATU ZA AWALI HUKU AKISHINDWA KUBORESHA HUDUMA KATIKA ENEO HILO NI UONEVU NA WIZI MKUBWA UNAOTAKIWA KUCHUKULIWA HATUA NA HALMASHAURI YA MANISPAA YA MUSOMA.

KWA UPANDE MZABUNI HUYO WA UKUSANYAJI WA USHURU DAGAA NA SAMAKI PAMOJA NA MAZAO MENGINE YANAYOUZWA KATIKA SOKO HILO BI ALICE JUMANNE,AKIZUNGUMZIA MADAI HAYO AMESEMA KINACHOFANYIKA NI KUSIMAMIA TARATIBU NA SHERIA KATIKA UKUSANYAJI WA MAPATO.

NAYE  MKURUGENZI WA MANISPAA YA MUSOMA, BW. NATHAN MSHANA AMESEMA USHURU HUO NI HALALI, NA KAMA KUNA MFANYABIASHARA YEYOTE ANAYETILIA SHAKA KIWANGO HICHO AWASILISHE MALALAMIKO OFISINI KWAKE.
,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,

SERENGETI

MKOA WA MARA UMETANGAZA MIKAKATI MITANO YA KUPAMBANA NA KASI KUBWA YA MAAMBUKIZI MAPYA YA UGONJWA WA UKIMWI,IKIWA NI PAMOJA NA KUZUNGUMZA KWA UWAZI,KULAANI NA KUWAFANANISHA KAMA WAUAJI WATU WOTE WANAONEZA VIRUSI HIVYO KWA WENZAO KWA MASUDI.

KAULI HIYO IMETANGAZWA NA MKUU WA MKOA WA MARA BW JOHN GABIEL TUPA,KATIKA KIJIJI CHA NYAGASENSE KATA YA KENYAMONTA WILAYANI SERENGETI,BAADA YA KUZINDUA KITUO CHA KUTOLEA HUDUMA KWA WAGONJWA WALIO ATHIRIKA NA MAAMBUKIZI YA VIRUSI VYA UKIMWI.

MKUU HUYO WA MKOA AKIZUNGUMZA BAADA YA KUZINDUA JENGO HILO NDANI YA KITUO CHA AFYA CHA IRAMBA,AMBALO LIMEJENGWA  KWA USHIRIKIANO WA SHIRIKI LA KUDHIBITI MAGONJWA CDC,AIDS RELIEF  KUPITIA UFADHGILI WA MPANGO WA DHARURA WA RAIS WA MAREKANI WA KUDHIBITI UKIMWI.

AMESEMA MKOA WAKE HIVI SASA UNAONGOZA KITAIFA KWA MAAMBUKIZI MAPYA YA UKIMWI KWA KUWA NA CHA ASLIMIA 7.7, UNAWEZA KUPUNGUZA KASI HIYO ENDAPO KILA MTU ATAJITHAMINI,KUJIPENDA NA KUWAKINGA WENGINE.


KWA UPANDE WAKE MENEJA MWANDAMIZI AIDS RELIEF  DK EKANDUMI KIMOI,AMESEMA SUALA LA TIBA MBADALA MAARUFUKAMA KIKOMBE CHA BABU,LIMEKUWA NA CHANGAMOTO KUBWA AMBAYO IMESABISHA IDADI KUBWA YA WAGONJWA KUSITISHA MATUMIZI YA DAWA HIVYO KUSABABISHA WENGI WAO KUFARIKI DUNIA HUKU WANGINE WAKIWA KATIKA HALI MBAYA

NAYE MTAALAM WA AFYA YA JAMII WA UKIMWI NA KIFUA KIKUU KUTOKA SHIRIKA LA KIMAREKANI LA KUDHIBITI MARADHI NA KINGA DK GODWIN MUNUO,AMESEMA KUJENGWA KWA KITUO HICHO NI UKOMBOZI MKUBWA KWA WANANCHI WA ENEO HILO WANAOFIKIA ZAIDI ELFU 13 HUKU AKITOA WITO KWA WATU WALIO ATHIRIKA KUTUMIA HUDUMA NA TIBA KWA WAKATI NA KUWAHIMIZA NDUGU NA MARAFIKI KUTAMBUA AFYA ZAO MAPEMA.

MIONGONI MWA MIKAKATI AMBAYO IMETAJWA NA MKOA WA MARA KATIKA KUPAMBA NA MAAMBUKIZI YA UKIMWI KUPAMBANA NA MILA ZINAZOCHANGIA ONGEZEKO LA MAAMBUKIZI,ZIKIWEMO ZA UKEKETAJI WANAWAKE,KURITHI WAJANE PAMOJA NA KUHIMIZA TOHARA SALAMA KWA WANAUME NA KUHIMALISHA HUDUMA ZA KUZUIA MAAMBUKIZI KUTOKA KWA MAMA KWENDA KWA MTOTO.
,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,

BUNDA

HALMASHAURI YA WILAYA YA BUNDA MKOANI MARA IMEKANUSHA MADAI KUWA ILITEKELEZA MIRADI CHINI YA KIWANGO NA KUSEMA INAFANYA KAZI KWA KUZINGATIA MIONGOZO ILIYOPO NA KUWATAKA WADAU MBALIMBALI WA MAENDELEO KUFANYA UCHUNGUZI WA KINA KABLA YA KURIPO KWENYE VYOMBO VYA HABARI.

KAULI HIYO IMETOLEWA NA MKURUGENZI MTENDAJI WA HALMASHAURI HIYO CYPRIAN OYEIR  KUFUATIA TAARIFA ILIYOTOLEWA NA ASASI MOJA BINAFSI INAYOSHUGHULIKIA MAENDELEO KUTOAS TAARIFA KWENYE BAADHI YA VYOMBO VYA HABARI KWAMBA HALMASHAURI HIYO  INATEKELEZA MIRADI KATIKA JIMBO LA MWIBARA CHINI YA KIWANGO CHA UBORA.

MIRADI INAYODAIWA KUTEKELEZWA CHINGI YA KIWANGO CHA UBORA NI BARABARA ZA NERUMA HADI CHAMAKAPO YENYE UREFU WA KM 4 NA CHAMAKAPO HADI KARUKEKERE(KM 5) ZOTE ZA JIMBONI HUMO HUKU WALIOLIMA BARABARA YA NAKATUBA NANSULULI YENYE UREFU WA KM 6 WAKIELEZEWA KUIDAI HALMASHAURI HIYO IJARA YAO.

AKIELEZEA MIRADI HIYO OYEIR AMESEMA ILITEKELEZWA KUPITIA MFUKO WA MAENDELEO YA JAMII (TASAF) KWA GHARAMA YA YA SHILINGI MILIONI 31 KILA MMOJA ZILIZOTUMIKA KATIKA SHUGHULI MBALIMBALI ZA MIRADI HIYO IKIWAMO YA KUNG’OA VISIKI;KUSAMBAZA UDONGO;KUSAWAZISHA TUTA LA BARABARA;KUPIMA ENEO LA KUPITISHA BARABARA;KULIMA NYASI;KUUMBA TUTA LA BARABARA NA KUWEKA MITARO YA PEMBEZONI MWA BARABARA.

MBALI NA KUIELEZEA MIRADI HIYO KUWA ILITEKELEZWA CHINI YA KIWANGO CHA UBORA ASASI HIYO PIA YENYE MAKAO YAKE MAKUU JIJINI DAR ES SALAAM ILIDAI KUWEPO KWA BAADHI YA WATU WANAOIDAI HALMASHAURI HIYO UJIRA WAO KAMA MALIPO YA KUSHIRIKI KATIKA KAZI HIYO JAMBO AMBALO MKURUGENZI MTENDAJI HUYO AMELIKANA NA  AKASEMA WOTE WALILIPWA HUKU AKIONESHA NYARAKA ZA MALIPO KWA WAANDISHI.

HATA HIVYO MKURUGENZI HUYO AMESEMA PENGINE ASASI HIYO HAIKUTOFAUTISHA KAZI ILIYOFANYWA KWA MIKONO NA ILE INAYOFANYWA KWA MITAMBO NA  NDIYO SABABU YA  KUSEMA MIRADI HIYO IMETEKELEZWA CHINI YA KIWANGO CHA UBORA JAMBO AMBALO HATA HIVYO AMESEMA LINGEEPUKWA TU KAMA WANGETAFUTA UKWELI WA MAMBO HAYO KUTOKA KWA WATAALAM WA HALMASHAURI NA KUWASHAURI KUFANYA HIVYO ILI KUEPUSHA MIGONGANO KATIKA MAENDELEO.
,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,
RORYA

HALMASHAURI YA WILAYA YA RORYA MKOANI MARA YADAIWA KUTUMIA VIBAYA PESA ZA RUZUKU YA SERIKALI  ZAIDI YA SHILINGI MILIONI 17 KWA MIEZI MITATU YA JULAI HADI SEPTEMBA 2011 ZILIZOTOLEWA KWA AJILI YA VITENGO AMBAPO IDARA SABA ZIMEDAIWA KUTUMIKA TOFAUTI.

TAARIFA KUTOKA UKAGUZI WA NDANI KWA ROBO YA KWANZA MWAKA 2011 HADI 2012 JULAI –SEPTEMBA ZINASEMA KUWA MATUMIZI MABAYA YA FEDHA NDANI YA HALMASHAURI YA RORYA ZIMEKIUKA KANUNI NAMBA 49 PAMOJA NA KUKWAMISHA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZILIZOPITISHWA NA VITENGO HUSIKA.

MATUMIZI MABAYA YA FEDHA YAMEPELEKEA KUKWAMISHA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA VITENGO KUTOKANA NA FEDHA HIZO KUTUMIWA KWENYE  SHUGHULI NYINGINE NA ZINGINE KUTOJULIKANA ZIMEFANYA KAZI GANI NA HIVYO KUSABABISHA VITENGO KUKWAMA NA KWAMBA ZIMEPUNGUZA MORALI YA KAZI.

WAKATI HUO HUO,  KAMPUNI YA NYAKILANG'ANYI IMEKIUKA MKATABA AMBAO ILIINGIA NA HALIMASHAURI YA WILAYA YA RORYA  KWA AJILI YA UJENZI WA HOSTEL YA NYANDUGA AMBAPO HALMASHAURI HIYO ILITOA ZAIDI YA SH.MILIONI 2OO KWA AJILI YA UJENZI WA HOSTELI.

HABARI ZAIDI ZINAELEZA KUWA MKANDARASI ALITAKIWA KUKABIDHI JENGO HILO MAY 30 MWAKA 2011 LAKINI MPAKA UKAGUZI UNAMALIZIKA MKANDARASI BADO HAJAKABIDHI JENGO HILO ILI HALI ZILIKUWA SIKU ZAIDI 100 ZIMEPITA NA WANAFUNZI BADO WANAKOSA HUDUMA.

,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,

TARIME

WILAYA YA TARIME MKOANI MARA INAKABILIWA NA UPUNGUFU WA WALIMU WA SHULE ZA MSINGI HALI INAYOSABABISHA BAADHI YA SHULE KUENDELEA KUWA NA UPUNGUFU WA WALIMU NAHIVYO KUSHUSHA KIWANGO CHA TAALUMA KWA WANAFUNZI.

KAIMU OFISA ELIMU GIDION MUHOCHI AMESEMA WILAYA INAKABILIWA NA UPUNGUFU WA WALIMU 229 HALI INAYOSABABISHA BAADHI YA WALIMU KUWA NA VIPINDI VINGI MADARASANI AMBAPO WILAYA HIYO INAJUMLA YA SHULE ZA MSINGI ZA SERIKALI 126.

MUHOCHI AMESEMA KUWA  WILAYA ILIKUWA NA UPUNGUFU WA WALIMU  341 NA KUWA KWA MWAKA HUU WILAYA YA TARIME IMEPEWA WALIMU 117 NA KATI YA HAO WALIORIPOTO NI 112 AMBAPO WALIMU 5 BADO KATIKA SHULE WALIZOPANGIWA.

AIDHA MUHOCHI AMESEMA KUWA WALIMU WOTE WALIORIPOTI TAYARI WAMESHAPATIWA FEDHA  ZA KUJIKIMU WAKATI WA KURIPOTI KATIKA VITUO VYAO VYA KAZI NA KWAMBA KWA KILA MWALIMU AMEPATIWA  SH.LAKI 2 NA ELFU 10,000.
,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,

HABARI KUTOKA KANDA YA ZIWA

MUSOMA

HALMASHAURI YA MANISPAA YA MUSOMA MKOANI MARA,IMEOMBWA KUZIONDOA GEREJI ZOTE AMBAZO ZIMEJENGWA PEMBENI MWA ZIWA VICTORIA KUTOKANA NA KUTIRIRISHA OVYO MAJI YA MABAKI YA MAFUTA NDANI YA ZIWA HILO JAMBO AMBALO LIMEDAIWA LIMEKUWA LIKISABABISHA UCHAFUZI MKUBWA WA MAZINGIRA.

WANANCHI HAO WAMESEMA KUWA BAADHI YA WATU WAMEANZISHA GEREJI BUBU KARIBU YA MAENEO YOTE YA MWALO WA MWIGOBERO HUKU WAKITUMIA GEREJI HIZO KUOSHEA MAGARI HATUA AMBAYO IMEKUWA IKICHANGIA KUINGIZA MAJI YA MABAKI YA MAFUTA NDANI YA ZIWA NA HIVYO KUSABABISHA UCHAFUZI MKUBWA WA MAZINGIRA.

HATA HIVYO WANANCHI HAO WAMESEMA MANISPAA YA MUSOMA INAPASWA KULAUMIWA KWA UCHAFUNZI HUO MKUBWA WA MAZINGIRA KUTOKANA NA KUFUMBIA MACHO SUALA HILO HUKU WAKITAMBUA WAZI KUWA MABAKI HAYO YA MAFUTA KUINGIZWA KATIKA MAJI YA ZIWA HILO YANAWEZA KUWA NA ATHARI KUBWA KWA BINADAM WANAOTUMIA MAJI HAYO PIA KUHARIBU MAZALIA YA SAMAKI.

KWA UPANDE  WAKE MWENYEKITI WA KIKUNDI CHA KUTUNZA HIFADHI YA MIAMBAO YA MAJI KATIKA MANISPAA YA MUSOMA BW OBED KASWAMILA,AMESEMA UCHAFUNZI WA MAJI YA ZIWA UMEANZA KUSHAMILI KUTOKANA NA UZEMBE MKUBWA WA MAAFISA WA MAZINGIRA KATIKA MANISPAA YA MUSOMA NA MAENEO MENGINE MKOANI MARA KWA KUSHINDWA KUSIMAMIA SHERIA ZILIZOWEKWA .
,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,

MWANZA.

MELI NDOGO YA MIZIGO YA PASIFIC, IMEZAMA KATIKA ZIWA VICTORIA, AMBAPO MTU MMOJA AMERIPOTIWA KUFARIKI DUNIA, HUKU WENGINE 15 WAKIOKOLEWA NA WAVUVI NDANI YA ZIWA HILO.

MELI HIYO INAYODAIWA KUMILIKIWA NA MTOTO WA MMILIKI WA KAMPUNI YA MELI ZA NYEHUNGE JIJINI MWANZA, IMEZAMA JANA MAJIRA YA SAA 3 ASUBUHI, IKIWA INATOKA KATIKA KISIWA CHA GHANA WILAYANI UKEREWE KWENDA JIJINI MWANZA, NA IMEZAMA ENEO LA BWIRO WILAYANI UKEREWE.

TAARIFA ZINAELEZA KWAMBA, MELI HIYO ILIKUWA IMESHEHENI MIZIGO YA DAGAA, PAMOJA NA MAKRETI YA SODA NA BIA  AMBAPO INAELEZWA KUWA  CHANZO CHA KUZAMA NI DHORUBA KALI, AMBAPO MELI HIYO ILISHINDWA KUMUDU MAWIMBI HAYO MAKUBWA.

KWA MUJIBU WA TAARIFA HIZO, AMBAZO PIA ZIMETHIBITISHWA NA JESHI LA POLISI MKOANI MWANZA PAMOJA NA MAMLAKA YA UDHIBITI WA USAFIRI WA NCHI KAVU NA MAJINI NCHINI (SUMATRA), KANDA YA ZIWA, ZIMEELEZA KWAMBA, MELI HIYO YA PASIFIC ILIZIDIWA MAWIMBI MAKALI NDANI YA ZIWA HILO, HIVYO KUZAMA MAJI KABISA.

HILI NI TUKIO LA PILI AMBAPO JUMAPILI WIKI ILIYOPITA, BOTI MOJA YA ABIRIA ILIZAMA KATIKA ZIWA VICTORIA, WAKATI IKITOKA MAISOME KWENDA KAHUNDA WILAYANI SENGEREMA MKOANI MWANZA, AMBAPO WATU 35 WALIHOFIWA KUFA MAJI, INGAWA BAADAYE JESHI LA POLISI LILIDAI HAKUNA ALIYEFARIKI DUNIA BAADA YA ABIRIA HAO KUOKOLEWA.

MBALI NA HAYO, HIVI KARIBUNI WATU KADHAA WALINUSURIKA KUFA MAJI BAADA YA BOTI MBILI WALIZOKUWA WAKISAFIRIA KUGONGANA USO KWA USO NDANI YA ZIWA VICTORIA KATIKA ENEO LA MUSOMA VIJIJINI MKOANI MARA.

AKITHIBITISHA KUZAMA KWA MELI HIYO YA PASIFIC HAPO JANA  OFISA MKAGUZI WA SUMATRA KANDA YA ZIWA, BW. ALFRED WARIANA AMESEMA, NI KWELI MELI HIYO IMEZAMA NDANI YA ZIWA HILO IKIWA NA SHEHENA KUBWA YA MIZIGO.
,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,

Friday, February 17, 2012

Walimu wapya Rorya waandamana

Na Waitara Meng’anyi, Rorya.

ZAIDI ya walimu wapya  40 wameandana na kulala katika ofisi za Halmashauri ya Wilaya Rorya zilizoko Ingiri juu kushinikiza kulipwa pesa yote ya kujikimu ya siku saba.

Hali hiyo imekuja baada ya walimu hao kubaini kuwa katika Wilaya zingine wenzao walilipwa kiasi tofauti na wao.

Wakizungumza na waandishi wa habari mapema asubuhi jana walimu hao walieleza kuwa kulipwa pesa ya siku nne kunawafanya washindwe kuandaa maisha yao mapya vizuri na pesa hiyo haitatoshi kulingana na mazingira yalivyo Wilayani humo.

“Tuliamua kutembea kwa miguu na kuja kulala hapa ili uongozi uone kuwa hatukubaliani ha kiasi hicho cha pesa ya kujikimu wanachokitoa kwetu” alisema mmjoja wa walimu hao ambaye hakutaka jina lake kutajwa gazetini.

Walisema kuwa kati ya walimu 160 walioajiriwa katika Halimashauri hiyo wakiwemo walimu wachache wa shule za sekondari, baadhi yao walipokea kiasi cha shilingi 140,000 ambacho ni cha siku nne na waliobaki walikataa wakidai walipwe pesa yote ya siku saba.

“Mimi nina mke na sina chombo cha ndani hata kimoja wakinipa shilingi 140,000/- kitanisaidia nini na  bei ya vitu iko juu nitaishije sina kitu ndani? Alihoji Mwalimu Musa Abdi.

Kutokana na maandamano hayo uongozi wote wa Wilaya hiyo ulifanya kikao na walimu hao na kuwaomba wapokee kiasi hicho ambachokipo na watalipwa kwa kuwa hakuna pesa ya kutosha katika halmashauri hiyo.

Afisa elimu wa Wilaya hiyo Michael Igogo alisema kuwa wanafanya mazungumzo na RAS na TAMISEMI kuona namna ya kutatua tatizo hilo linalowakabili, na kuongeza kuwa hoja yao ni ya msingi.

“Hoja zao ni kuwa kwa nini hawalipwi pesa zote kama Wilaya zingine, lakini Wilaya hizo zina mapato makubwa.Hata hivyo tumeamua kuwalipa sawa wote shilingi 245,000/-“ alisema Igogo.

Ofisa huyo aliongeza kuwa kati ya walimu waliopangiwa Wilayani humo wengine walipelekewa pesa zao vituoni mwao ili kuondoa usumbufu wa wao kufuatilia pesa hizo ofisini badala ya kuwahudumia wanafunzi.

“Hawa ni wale waliochelewa kuripoti na kutokana na kuwa hatuna pesa za kutosha tumeamua kuwapa kiasi hicho cha siku nne halfu tutawamalizia kiasi cha siku tatu baada ya kurekebisha mambo” alisema afisa Elimu huyo.

Thursday, February 16, 2012

MWALIMU AKATWA PANGA ,APORWA FEDHA ZA KIKUNDI

Serengeti
Februari 16,2012.

MWALIMU wa shule ya msingi Majimoto kata ya Busawe wilayani Serengeti
Bhoke Mwita amenusurika kufa baada ya kuvamiwa na mtu anayedhaniwa
kuwa jambazi na kumkata sehemu mbalimbali za mwili
kwa panga kisha kuchukua tsh,300,000=za kikundi cha kuchangiana.

Tukio hilo la kusitikisha linadaiwa kutokea februari 15,majira ya saa
3 usiku mwaka huu mita chache toka nyumbani kwa mwalimu
,limethibitishwa na polisi na uongozi wa kijiji hicho.

Mwenyekiti wa serikali ya kijiji hicho Johannes Masirori aliliambia
gazeti hili kuwa mwalimu huyo alikatwa sehemu mbalimbali za mwili
ikiwemo,shavu la kushoto,mikono ya kushoto na kulia kisha akachukua
fedha hizo na simu na kukimbia.

“Mwalimu ni mweka hazina wa kikundi cha kuchangiana wanawake kiitwacho
upendo alikuwa akitoka kukusanya fedha hizo ili akabidhi
leo(jana)akikaribia kwake ndipo akawekwa chini ya ulinzi na kijana
aliyetambuliwa kwa jina la Magocha Kiring’ani akiomba fedha na
simu”alisema mwenyekiti.

Alisema kabla hajajua nini kimetokea ndipo alianza kumkata maeneo
mbalimbali kwa panga,licha ya kupiga kelele lakini hazikusikika kwa
kuwa kulikuwa na muziki eneo hilo.

“Inaonekana kuwa alikuwa anamfuatilia kwa kuwa baada ya kumweka chini
ya ulinzi kitu cha kwanza alisema anaomba fedha na simu,na kweli
alifanikiwa kuchukua fedha hizo,lakini simu alidondosha na  iliokotwa
na wananchi waliojitokeza baadae”alisema.

Alisema mtuhumiwa huyo inadaiwa kabla ya kumfanyia unyama mwalimu
alikutana na mama mmoja aliyetajwa kwa jina la Mtabu na kumwamru kukaa
chini,lakini alipomlika akamtambua na kumtaja kwa jina alikimbia na
kwenda eneo jingine ambalo alikutana na mwalimu na kumfanyia unyama
huo.

“Huyo mtuhumiwa anakaa kijiji cha Nyamakhobiti jilani na hapa ,aliwahi
kufungwa kwa uharifu,na baada ya kutoka alikutwa na tuhuma ya ubakaji
akawa amekimbia ,na anaonekana usiku tuna inadaiwa anaishi porini
akijificha ‘alisema.

Alisema jamii kwa kushirikiana na polisi wanamsaka kuhakikisha
wanamkamata kutokana na kukithiri kwa vitendo vinavyohatarisha maisha
ya watu.

Kuhusu hali ya mwalimu alisema baada ya kushonwa majeraha yake katika
zahanati ya Majimoto anaendelea vizuri .

Polisi wilayani hapa wanaendelea na msako wa mtuhumiwa huyo huku
wakiomba jamii ambayo inaishi naye itoe ushirikiano waweze kumtia
nguvuni.

Mwisho.

MWALIMU AKATWA PANGA ,APORWA FEDHA ZA KIKUNDI

Serengeti
Februari 16,2012.

MWALIMU wa shule ya msingi Majimoto kata ya Busawe wilayani Serengeti
Bhoke Mwita amenusurika kufa baada ya kuvamiwa na mtu anayedhaniwa
kuwa jambazi na kumkata sehemu mbalimbali za mwili
kwa panga kisha kuchukua tsh,300,000=za kikundi cha kuchangiana.

Tukio hilo la kusitikisha linadaiwa kutokea februari 15,majira ya saa
3 usiku mwaka huu mita chache toka nyumbani kwa mwalimu
,limethibitishwa na polisi na uongozi wa kijiji hicho.

Mwenyekiti wa serikali ya kijiji hicho Johannes Masirori aliliambia
gazeti hili kuwa mwalimu huyo alikatwa sehemu mbalimbali za mwili
ikiwemo,shavu la kushoto,mikono ya kushoto na kulia kisha akachukua
fedha hizo na simu na kukimbia.

“Mwalimu ni mweka hazina wa kikundi cha kuchangiana wanawake kiitwacho
upendo alikuwa akitoka kukusanya fedha hizo ili akabidhi
leo(jana)akikaribia kwake ndipo akawekwa chini ya ulinzi na kijana
aliyetambuliwa kwa jina la Magocha Kiring’ani akiomba fedha na
simu”alisema mwenyekiti.

Alisema kabla hajajua nini kimetokea ndipo alianza kumkata maeneo
mbalimbali kwa panga,licha ya kupiga kelele lakini hazikusikika kwa
kuwa kulikuwa na muziki eneo hilo.

“Inaonekana kuwa alikuwa anamfuatilia kwa kuwa baada ya kumweka chini
ya ulinzi kitu cha kwanza alisema anaomba fedha na simu,na kweli
alifanikiwa kuchukua fedha hizo,lakini simu alidondosha na  iliokotwa
na wananchi waliojitokeza baadae”alisema.

Alisema mtuhumiwa huyo inadaiwa kabla ya kumfanyia unyama mwalimu
alikutana na mama mmoja aliyetajwa kwa jina la Mtabu na kumwamru kukaa
chini,lakini alipomlika akamtambua na kumtaja kwa jina alikimbia na
kwenda eneo jingine ambalo alikutana na mwalimu na kumfanyia unyama
huo.

“Huyo mtuhumiwa anakaa kijiji cha Nyamakhobiti jilani na hapa ,aliwahi
kufungwa kwa uharifu,na baada ya kutoka alikutwa na tuhuma ya ubakaji
akawa amekimbia ,na anaonekana usiku tuna inadaiwa anaishi porini
akijificha ‘alisema.

Alisema jamii kwa kushirikiana na polisi wanamsaka kuhakikisha
wanamkamata kutokana na kukithiri kwa vitendo vinavyohatarisha maisha
ya watu.

Kuhusu hali ya mwalimu alisema baada ya kushonwa majeraha yake katika
zahanati ya Majimoto anaendelea vizuri .

Polisi wilayani hapa wanaendelea na msako wa mtuhumiwa huyo huku
wakiomba jamii ambayo inaishi naye itoe ushirikiano waweze kumtia
nguvuni.

Mwisho.

HABARI KUTOKA MARA


MUSOMA


MAKAMU WA SHULE YA SEKONDARI YA MKONO AMETOA WITO KWA WAZAZI NA WALEZI HALMASHAURI YA MUSOMA MKOANI MARA KUTOA USHIRIKIANO KWA WALIMU NA KUZIAMINI SHULE ZA KATA KWANI NI NZURI TOFAUTI NA INAVYODHANIWA

AKIZUNGUMA NA KITUO HIKI LEO OFISINI KWAKE BW. AMANI MALIMA AMESEMA KUWA SHULE HIZO NI NZURI KWA SASA KWANI SERIKALI IMEBORESHA ELIMU KATIKA SHULE ZA KATA HAPA NCHINI

MAKAMU WA SHULE HUYO AMESEAM KUWA SHULE HIYO INAKABILIWA NA CHANGAMOTO MBALIMBALI IKIWA NI PAMOJA NA UKOSEFU WA MABWENI MAABARA NA HUDUMA YA MAJI.

KULINGANA NA CHANGAMOTO HIZO DIWANI WA KATA YA BISUMWA MAGINA MAGESA AMBAYE NI MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA MUSOMA AMESEMA KUWA KUTOKANA NA MATATIZO HAYO SERIKALI IPO KATIKA MKAKATI WA KUTATUA  CHANGAMOTO HIZO KATIKA SHULE ZOTE ZA KATA ZILIZOPO MKOANI MARA

AIDHA AMEONGEZA KUWA WAZAZI NAWALEZI WAJITOLEE KUSHIRIKIAN NA WALIMU ILI KUONGEZA MAFANIKIO MAKUBWA KATIKA KATA YAO
,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,


WALIMU NA WAZAZI NCHINI WAMELAUMIWA KUWA CHANZO CHA KUPOROMOKA KWA MAADILI AMBAYO HUPELEKEA KUPATIKANA KWA MATOKEO MABAYA YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE HAPA NCHINI.

WAKICHANGIA KWA NJIA YA SIMU NA MITANDAO YA KIJAMII KATIKA KIPINDI CHA BIG BREAFAST LEO ASUBUHI WANANCHI KUTOKA SEHEMU MBALIMBALI MKOANI MARA NA NJE YA MKOA WA MARA WAMESEMA KUWA WALIMU WAMEKUWA CHANZO KWA KUKIUKA MAADILI YA KAZI ZAO.

WAMESEMA INASHANGAZWA KUONA MWALIMU ANASHAWISHIKA KUMUOMBA MZAZI FEDHA KWA KIGEZO CHA KUMSAIDIA MTOTO AFAULU KATIKA MTIHANI HUSKA KITU AMBACHO HUPELEKEA KUWA NA WAHITIMU WASIOJUA KUSOMA NA KUANDIKA.

MBALI NA HIVYO BAADHI YA WANANCHI WAMESEMA KUWA WAZAZI NDIYO CHANZO KWA KUWASHAWISHI WALIMU KUKIUKA MAADILI YA KAZI YAO HUKU WENGINE WAKISEMA KUWA WALIMU WANASHINDWA KUTIMIZA WAJIBU WAO.

AIDHA WAMEONGEZA KUWA WALIMU WAMESHINDWA KUWAANDAA WANAFUNZI KATIKA KUKABILIANA NA MTIHANI NA HIVYO KUWAJENGEA MAZINGIRA YA KUWAONYESHA MTIHANI KITU KINACHOPLEKEA WATOTO KUACHA KUJISOMEA.

WANANCHI HAO WAMESHAURI KUWA NI VYEMA KILA UPANDE WAKATIMIZA WAJIBU WAO KWA UKAMILIFU KITU AMBACHO KITASAIDIA KUPUNGUZA MATOKEA MABAYA HAPA NCHINI.

MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE MWAKA HUU ZAIDI YA WANAFUNZI 3000 WAMEFUTIWA MATOKEO YAO KUTOKANA NA UDANGANYIFU ULIOFANYIKA KATIKA CHUMBA CHA MTIHANI

,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,


Tuesday, February 14, 2012

HABARI KUTOKA MARA


BUNDA
WAKAZI WA KITONGOJI CHA MBUGANI KILICHOKO KATIKA MAMLAKA YA MJI MDOGO WA BUNDA MKOANI MARA WAMEITAKA HALMASHAURI YA WILAYA YA BUNDA KUSITISHA MARA MOJA MAOMBI YA KANISA LA ANNE BAPTIST LA MJINI HUMO YA KUTAKA LIMILIKISHWE EKARI 93 ZA ARDHI NA KUTISHIA KWENDA KUMWONA WAZIRI MWENYE DHAMANA KAMA HAITOFANYA HIVYO.
UAMUZI HUO WA WAKAZI HAO UMEFIKIWA KATIKA MKUTANO WA HADHARA ULIOFANYIKIA KATIKA KITONGOJI HICHO NA KUHUDHURIWA NA OFISA ARDHI WA HALMASHAURI HIYO DENIS MASAMI ULITOKANA NA KILE WALICHOSEMA KUTOSHIRIKISHWA KWAO KATIKA MCHAKATO MZIMA WA MATUMIZI YA ARDHI HIYO
KATIKA TAMKO LAO LILILOSOMWA NA FORTUNATUS MARO WAKAZI HAO WAMESEMA KITENDO CHA IDARA YA ARDHI YA WILAYA HIYO CHA KUTOWASHIRIKISHA WAKAZI WA ENEO HUSIKA AMBAO KISHERIA NDIO WAMILIKI WA ARDHI YA ENEO HILO KATIKA KUGAWA SEHEMU HIYO YA ARDHI NI UKIUKWAJI WA SHERIA UNAOPASWA KUEPUKWA NA MAMLAKA HUSIKA ILI KUEPUSHA MIGOGORO YA ARDHI NDANI YA JAMII.

MARO ALIYEKUWA AKISOMA TAMKO ALIENDA MBALI ZAIDI PALE ALIPOSEMA HUENDA MAOFISA WA IDARA YA ARDHI WILAYANI HUMO WAMEPEWA RUSHWA KUTOKA KWA WATU WA KANISA LA ANNE BAPTIST ILI WAWAMILIKISHE KINYEMELA ENEO HILO BILA KUWASHIRIKISHA WANANCHI NA KUSEMA KAMWE HAWAKO TAYARI KUYAVUMILIA MAMBO KAMA HAYO.
KAULI YA HIYO YA MARO ILIUNGWA MKONO NA MWENYEKITI WA KITONGOJI HICHO ARISTARIKO BULAYA ALIYEONESHA MSHANGAO WAKE JUU YA MAAMUZI YA IDARA HIYO YA ARDHI YA KUYAKUBALI MAOMBI HAYO YA KANISA HILO HUKU ARDHI HIYO INAYOMILIKIWA NA WAKULIMA IKIWA BADO HAIJAPIMWA BILA HATA KUWASHIRIKISHA WANANCHI NA KUITAKA IDARA HIYO ISITISHE MAOMBI HAYO MPAKA IAFIKIANE NA WAKAZI HAO.
KWA UPANDE WAKE OFISA ARDHI WA WILAYA HIYO DENIS MASAMI AKIJIBU TUHUMA HIZO AMESEMA WANANCHI WA KITONGOJI HICHO HAWAKUWEZA KUSHIRIKISHWA KATIKA UPIMAJI HUO KWA SABABU ENEO HILO LILILOMO NDANI YA ENEO LA MAMLAKA YA MJI MDOGO WA BUNDA KISHERIA NI MALI HALALI YA MAMLAKA HIYO ..
MAPEMA AKIONGEA KATIKA MKUTANO HUO MWAKILISHI WA KANISA HILO LENYE MAKAO YAKE MAKUU NCHINI MAREKANI MANG'ALARYA MASUBUGU AMESEMA KANISA LAKE LILIFUATA TARATIBU ZOTE ZA ARDHI LIKIWEMO KUTUMA MAOMBI KWA MAANDISHI NA KWAMBA KANISA HILO LITALIPA GHARAMA ZOTE ZA FIDIA ZA WENYE MASHAMBA IKIWA WATAKUBALIWA.
,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,

MUSOMA


WAKAZI WA MANISPAA YA MUSOMA MKOANI MARA WAMETAKIWA KUZINGATIA KANUNI, SHERIA NA TARATIBU ZINAZOWEKWA NA MANISPAA ILI  KUUFANYA MJI HUO KUWA SAFI NA MANDHARI INAYOVUTIA

WITO HUO UMETOLEWA NA MKURUGENZI WA MANISPAA YA MUSOMA NATHAN MSHANA WAKATI AKIONGEA NA KITUO HIKI  LEO ASUBUHI OFISINI KWAKE KATIKA MANISPAA YA MUSOMA MKOANI MARA

AMESEMA MANISPAA IMEANZA KUFANYA MCHAKATO WA KUWEKA MJI WA  MUSOMA KATIKA HALI YA USAFI KWA KUWEKA MAPIPA YA TAKA SEHEMU MBALIMBALI YA MJI ILI KUZUIA WATU KUTUPA TAKA HOVYO

AMEWATAKA WAFANYA BIASHARA WOTE MKOANI MARA KUWA NA MAPIPA YA TAKA KATIKA MAENEO YA BIASHARA LENGO LIKIWA NI KUZUIA TAKA KUZAGAA KATIKA MAENEO YA BIASHARA ZAO

MKURUGENZI HUYO AMESEMA KUWA KWA SASA BARAZA LA MADIWANI NA WAKUUU WA IDARA SABA WAPO KWENYE SEMINA KATIKA MANISPAA YA MOSHI KWA MADHUMUNI YA KUJIFUNZA  NA KUIMARISHA SHERIA NDOGONDOGO ZINAZOWEKWA NA MANISPAA ILI KUDHIBITI TATIZO LA UCHAFU KATIKA MANISPAA YA MUSOMA

,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,

BUNDA

MKUU WA WILAYA YA BUNDA FRANSIC ISAAC AMESEMA KUWA HATUA YA SERIKALI WILAYANI HUMO KUWAZUIA WAKAZI WA KATA YA BUNDA STOO MJINI HUMO KUJENGA SEKONDARI YAO ILITOKANA NA SABABU KADHAA IKIWAMO YA KUTOKUELEWANA KWAO SEHEMU YA  KUIJENGEA SHULE HIYO.
AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI KWA NIABA YA MKUU HUYO WA WILAYA AFISA TARAFA WA TARAFA YA SERENGETI  JUSTINE LUKAKA AMESEMA KUWA MARA BAADA YA WAKAZI HAO KUAZIMIA KUJENGA SHULE YAO YA SEKONDARI MGOGORO WA SEHEMU YA KUIJENGEA SHULE HIYO ULIZUKA MIONGONI MWAO.
KWA MUJIBU WA OFISA TARAFA HUYO MVUTANO HUO WA SEHEMU YA KUIJENGA SHULE HIYO UNATOKANA NA MUONEKANO  MBAYA WA JOGRAFIA YA KATA HIYO UNAOIGAWA KATIKA SEHEMU MBALIMBALI ZINAZOONESHA KANA KWAMBA SIYO KATA MOJA NA HALI ILIYOPELEKEA WAKAZI WA KILA SEHEMU KUTAKA IJENGWE KATIKA ENEO LAO NA HIVYO KUZUSHA MGOGORO MIONGONI MWA.
MBALI NA HILO PIA AFISA TARAFA HUYO AMESEMA MKUU WA WILAYA ALIFIKIA HATUA YA KUWAKATALIA KUJENGA SHULE YAO YA SEKONDARI KWA KUWA HOJA HIYO ILIKUJA HUKU BARAZA LA MADIWANI LA HALMASHAURI YA WILAYA HIYO LIKIWA LIMESHAPITISHA AZIMIO LA KUONGEZA VYUMBA VYA MADARASA 88VINAVYOHITAJIKA  KATIKA SHULE 24 ZA SEKONDARI ILI KUWAWEZESHA WATOTO WOTE 5325 WALIOFAULU NA KUOSWA NAFASI WAENDE SEKONDARI MAPEMA MWEZI UJAO.
LUKAKA AMESEMA MKUU WA WILAYA ANAWASISITIZIA WAKAZI WA KATA HIYO KUENDELEA KUCHANGIA BILA SHURUTI UJENZI WA SHULE ZA SEKONDARI ZA RUBANA NA DR.NCHIMBI WALIZOZIJENGA KABLA YA KUTENGWA KUWA KATA MWAKA 2009 NA AMBAPO WATOTO WAO WANAENDELEA KUSOMEA .
HIVI KARIBUNI WAKAZI HAO WALIRIPOTIWA KUGOMA KUCHANGIA UJENZI WA SHULE HIZO KAMA SHINIKIZO LA KUITAKA SERIKALI WILAYANI HUMO IWARUHUSU WAJENGE YA KWAO HALI ILIYOPELEKEA MKUU WA WILAYA HIYO KUAMURU KUKAMATWA NA KUWAFIKISHA MAHAKAMNI  WENYEVITI  WAWILI WA VITONGOJI WAKITUHUMIWA KUCHOCHEA MGOMO HUO.
,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,