Wednesday, February 16, 2011

ZAIDI YA MILIONI 400 KUREKEBISHA MIUNDOMBINU MUSOMA

MUSOMA

Zaidi ya shilingi milioni 400 zinatarajiwa kutumika katika ujenzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika Halmshauri ya manispaa ya musoma mkoani mara huku milioni 212 zikitoka awamu ya kwanza ya miradi hiyo

Makubaliano hayo yamefanyika leo katika ukumbi wa manispaa ya Musoma mjini mjini hapa ambapo mkurugenzi wa manispaa hiyo Bw Nathan Mshana amezitaka kampuni hizo kujenga kwa kiwango miradi waliyopewa ili ziweze kupata miradi mingine ambayo itakuwa ikiratibiwa na Halmshauri hiyo.
Mkurugenzi wa manispaa ya Musoma Bw Nathan Mshana kulia na kushoto ni Meya wa Manispaa ya Musoma  ALEX kISURURA

Alisema masharti ya mikataba hiyo inajieleza wazi hivyo mkandarasi atakayekiuka makubaliano hayo halmashauri hiyo haitasita kumchulia hatua mkandarasi yeyote kulingana na makubaliano yaliyopo,mkurugenzi huyo ameongeza kuwa halmshauri yake itakuwa ikifuatilia hatua kwa hatua ujenzi wa miradi hiyo na kama kutakuwa na kasoro mkandarasi huska atairekebisha kasoro hiyo kabla ya kuendelea na ujenzi

  'Katika hili hatutamsubiri mtu mpaka aboronge mradi ndio tumsimamishe hivyo tutakuwa tukiikagua miradi hiyo mara kwa mara hivyo katika mikataba hiyo tunaamini itenda vizuri maana hata fedha zitakuwa zikilipwa kwa awamu na hili cheti kitoke kwa kampuni hiyo lazima tujirizishe kwanza na mradi uivyotengenezwa" alisema mkurugenzi huyo
Aidha mkurugenzi huyo alisema kuwa kuna fedha ambazo hazitatolewa kwa mkandarasi ili kuhakikisha mradi huo utachukua muda mrefu na kama watahakikisha mradi huo utachukua muda mrefu mkandarasi atapewa fedha zote pamoja na hivyo Mshana alisema kuwa kama mkandarasi ataenda kinyume na makubaliano kuna kiasi cha fedha kitakatwa katika makubaliano hayo

Naye mstahiki Meya manispaa ya Musoma Alex Kisurura alisema kuwa mkandarasi ambaye hatokidhi vigezo hatua kali zitachukuliwa dhidi yake  kwani fedha zinazotumika katika miradi hiyo ni fedha za wananchi,alisema kuwa wakandarasi hao wanatakiwa kufanya kazi kwa ushirikiano na wananchi wa sehemu huska.
Meya huyo aliwataka wananchi kutoa taarifa na maoni katika Halmashauri hiyo kulingana na utendaji wa wakandarasi hao ili wasije wakalalamika baada ya mkandarasi kumaliza kazi na kulipwa fedha ambazo zinatoka mifukoni mwao,Mbali na hivyo Kisurura aliwataka wakandarasi hao kutofanya kazi kwa mazoea na katika hilo hawatomkubalia mtu yeyote.

  "Tatizo lililokuwepo ni kwamba wakandarasi hawa walikuwa wanafanya kazi kwa mazoea hivyo hatutamuonea mtu huruma katika hilo maana fedha zinazotumika ni za wananchi na hivyo tunawataka wananchi nao watoe ushirkiano kwa kutoa taarifa na maoni ili tuhakikishe miradi hiyo inakwenda vizuri"

Katika hatua nyingine kaimu injiania wa Manispaa hiyo Mohamed Etanga aliwaasa wakandarasi hao kuwa makini na ugonjwa wa ukimwi hasa huko wanakokwenda kufanya kazi kwani kumnekuwa na desturi hasa pale watu wanapokuwa kwenye mkusanyiko kusahau suala zima la Ukimwi.

  "Kuna suala nilikuwa nimesahau maana watu wanapokuwa kwenye site wanasahau kabisa suala zima la Ukimwi,hivyo tuwe makinin na Ukimwi maana hapa Manispaa kuna wataalam ni vyema mkashirikiana nao katika kupambana na ukimwi ikiwemo kutoa semina sehemu hizo

Nao baadhi ya wawakilishi katika makampuni hayo walisema kuwa kupata mradi katika Halmshauri ni kazi ngumu hasa kwasasa ambapo baadhi ya wakandarasi wamekuwa wakifanya kazi chini ya Kiwango hivyo hiyo ni changamoto katika utendaji huo wa kazi.
Katika Makubaliano hayo jumla ya kampuni tano zilitiliana sahihi na Halmashauri ya Manispaa ya Musoma ambapo ni kampuni ya G&G ambao wamepewa kurekebisha barabara za Bweri,Mwisenge,Buhare,Nyakato,Kamnyonge na Makoko zenye jumla ya kimoleta 20.5,Mhin and Brothers Ltd  ambayo ilipewa barabra ya Nyasho shuleni ikiwa ni kujenga maeneo ya kupitisha watu na maji,Nyabweki Construction ambao wamepewa kurekebisha barabara za mjini kwa kiwango cha changalawe ambapo barabara hizo ni Rutiginga,Karume,Kawawa,Kenedy,Uhuru,Lumumba,Kusaga,Jamathin,Amani,Ghandi na Iringo.

Zingine ni kampuni Zubben Co LTD ambayo imepewa kutengeneza barabara ya Nyakato kwa kiwango cha Changalawe huku Sakm Engineering wakipewa kutengenza miferji ya MwisengeMwisho

No comments:

Post a Comment